Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Kweli binadamu wengi ni kipengele, kwa jinsi hii stori yako inavyotia aibu hakutakiwa kuihadithia ukiwa proud namna hiyo.

Kuoa mwanamke ambaye hana pakwenda ni nzuri for man's ego. Na kwanini mkeo hana nauli? 🤦‍♀️🤦‍♀️
Inatia aibu kwangu au kwake?
Wapi nimesema hana pa kwenda? (laiti ungejua kipato chake na famikia yake ilivyo usingeongea haya, au ulizani ana njaa na kwao hapaeleweki ndio maana ukasema hivyo??)

- Hakuwa na nauli kwa sababu, baaba ya kutofautiana aliondoka na hela kidogo, akaitumia kwa nauli ya kwenda na chakula mchana. Hakukumbuka kuchukua card za benki, mimi niliitwa akiwa polisi jioni yake. Hapo unategemea angetoa wapi hela?
 
as anger management consultant hua nashauri sana wateja wangu kuwalamba vibao wanao wakwaza ukimdunda mkwazaji una release dopamine unakua stress free hii inakuepusha na kumuua huyo bwege huko mbeleni au wewe mwenyewe kujiua au kua mlevi kupindukia kupambana na stress mtu akikwaza usisite kumlamba mambata usiangslie umri jinsia wala cheo as longer as amekuuzi na yuko within proximity mkutanisshe na shambulii la kudhuru mwili
😀 😀 😀 😀 Nimecheka mpaka machozi yametoka .....vayolensi
 
Ndio, binadamu wa kike au wakiume tunapaswa kuwa na akiba muda wowote, kwenu hukuambiwa kuhusu kukanyaga nyanya za watu kipindi unakua?

Au umejilea mtaani.
Acha hasira dada.
Kukosa hela mfukoni ni kawaida, inategemea mazingira yaliyopelekea hivyo.
Kwa hiyo wewe ukiwa huna hela huwezi kutoka kwa kuogopa kukanyaga nyanya za watu?
 
Inatia aibu kwangu au kwake?
Wapi nimesema hana pa kwenda? (laiti ungejua kipato chake na famikia yake ilivyo usingeongea haya, au ulizani ana njaa na kwao hapaeleweki ndio maana ukasema hivyo??)

- Hakuwa na nauli kwa sababu, baaba ya kutofautiana aliondoka na hela kidogo, akaitumia kwa nauki ya kwenda na chakula mchana. Hakukumbuka kuchukua card za benki, mimi niliitwa akiwa polisi jioni yake. Hapo unategemea angetoa wapi hela?
Angepanda boda akifika penye hela achukue alipe. Mbona simple sana.
 
Mimi nilimchapa vibao mke wangu akiwa mjamzito kisa kunitukania mama yangu. Akaenda Polisi, wakanipigia simu, nikachukua zangu karatasi tatu na kalamu nikaandika taraka kabla sijafika kituoni. Nikabeba simu, hela kama fifte zile karatasi.

Kituoni nafika, nimesimama mbele ya meza, naulizwa wewe ndio flani, wewe unamjua huyu, sijajibu zunguka huku, kofi la mhongo, vua mkanda, kiatu, saa wakanitupa sero, nikakabidhi hela, simu na zile karatasi kwenye bahasha.
Mwanamke wakamwambia rudi nyumbani ilikuwa jioni mida ya saa 10 hivi.

Mida ya saa 12 jioni naitwa sero, kumbe mke wangu amekuja kuniletea chakula na amenisamehe eti niachiliwe kimemuuma.
Afande wa zamu akasema, mpaka aje afande alienipigia simu. Ex Wife akawaambia yameshaisha, waniachie. Wakamwambia wewe umeleta mambo polisi kuna utaratibu wake, ungekuwa unataka msamehe huyu bwana usingekuja huku. Huyu atalala ndani mpaka akamilishe dhamana. Wakanitupia tena sero, nikakataa kula nikamwambia Afande hicho chakula arudi nacho huyo mwanamke.

Yule mama akalia sana pale nje, wakamfukuza wakamwambia aje asubuhi. Mtoto wangu wa miaka miwili namsikia analia baba, baba, mi nipo sero.
Kukakucha, Akawahi sana yule mama saa 12, kaleta chai. Polisi wana utaratibu wao, wakachomoa watu wa kwenda mahakamani, badae saa mbili mbili mlango unafunguliwa naitwa mimi, nafika CRO chumba cha mashitaka nawakuta jamaa, washikaji, mshua na wafanyakazi wangu wamekuja kunichomoa.

Basi tukaitwa ofisini kwa mkuu wa kituo, Afande mmoja Mwanamke ndie akasikiliza ishu yetu. Nikaonywa sana kupiga mke, kwamba ni jinai na ile ishu ningefungwa kwa kujeruhi, mambo mengi niliambiwa pale kibabe sana na yule Maza afande.

Wakanirudisha chumba cha Mashitaka, chukua vitu vyako, anataka kunikabidhi zile karatasi nikamwambia mpe huyu ndio zake anafungua kusoma ni taraka, kilio kikubwa mno na kugalagala chini. Polisi wakamwambia kama amekupa taraka nenda mahakamani ili ukapate haki zako.

Wana wakanichukua, wakanipeleka gesti, nikaoga kutoa nuksi nikaletewa nguo zingine nikavaa.

Yule mama akanipeleka mahakamani, na mimi sikurudi home, napigiwa simu na Mwenyekiti kuna samansi ya mahakamani.
Nikaenda mahakamani nikakiri kumpa taraka yule mama, wakaainisha vitu vya ndoa. Nyumba ya ndoa na viwanja viwili. Mimi nikawaambia nyumba ya ndoa ibaki ya watoto, viwanja viwili nampa moja chake moja changu. Nilikuwa na pesa akiba kama 1.5 M nikawambia mahakama nampa laki 7 na vyombo vyote vya ndani aondoke navyo.
Nyumba ikapangishwa, pesa ya mtoto mdogo nikaambiwa nitalipa hamsini kila mwezi. Mtoto mkubwa akabaki shule. Kwisha.

Mali zote nilikuwa naandikisha kampuni ambayo aliikuta yule mama. Nikaokoa mali kibao kupigwa pasu. Gari, trekta, vyote alidai mahakamani vikaonekana ni vya kampuni ambayo kaikuta na nipo mimi, mzee na mdogo wangu hiyo ilikuwa 2019. Mwanamke alikomaa sana kila kitu kiuzwe, kumbe mimi nilikuwa nafanya biashara chini ya Kampuni. Mali zangu ukinitafuta mimi hunikuti unaikuta kampuni. Tukavutana sana mahakamani, ikaonekana nimemuoa kampuni kaikuta na hajawahi kuingizwa kwenye kampuni kwa hisa au kwa kufanya kazi. Ana kazi yake nina biashara zangu. Pia nilipeleka Usia na mirathi ya mama yangu ambae katika mgao wa mirathi ya mama ndipo tulikubaliana mimi, baba na wadogo zangu tufungue kampuni na yeye nikamuoa miaka 10 baadae.

Nikaokoa mali mzee, vinginevyo ilikuwa ni pasu kwa pasu. Chezea mwanamke akiwa mjinga ila akiwa anajitambua ni hatari sana mbele ya sheria jameni. Mwanamke aliweka mpaka wakili kutaka mali zile.

Pole sana Mzee mwenzangu. Mke mbele ya sheria achukuliwi kama mke wako anachukuliwa kama "Separate entity" yaani anakufunga laivu laivu. 😁
Ulipambana sana
 
Mimi kuna mmoja aliwahi nipeleke, nikaitwa dawati la jinsia, nikaenda.
Wakaanza ngonjera na vitisho kuwa nimempiga. Nikawaambia aeleze vizuri kosa ni lipi, aksema hakuwapikia watoto alikuwa anajisikia vibaya. Akaulizwa kama alitoa taarifa kwangu, akakataa.

Kimwanamke kimoja kikaanza, hata kama hakupikia watoto, huna haki ya kumpiga. Nikamuuliza unao ushahidi kama nimempiga, akasema mimi nimepokea malalamiko, nina uwezo wa kukuweka lockup. Nikamwambia, majadilianao yameishia hapa, nipelekeni mahakamani.

Basi wakachachamaa kuwa nina kiburi, watamsaidia mke wangu na watanipa fundisho, nikasema nasubiri. Kimbembe ikawa mke wangu hataki niwekwe lockup. Maana anajua jinsi nilivyokuwa na react sikuwa natania, ndoa ingeisha. Wakamwambia aandike maelezo, mimi nawekwa lockup then mahakamani. Wife akawajibu sina ushahidi mahakamani, na sitaki awekwe lockup maana hana kosa. 😂

Kilichoendelea ni yeye kukoswa kofi na kidada kimoja, eti unatusumbua. Kidogo akaja OCD akasikiliza marumbano, akawambia msizunje ndoa za watu, huyu dada anampenda mmewe, waacheni huru.

Kurudi home hana hata nauli, anatembea kwa miguu. Nikampa nauli ya daladala, nikapanda boda boda nikaondoka. Home nikawachukua watoto nikaondoka nao kwenda matembezi bila kumpa taarifa. Jioni hatukurudi, 😂😂 ngoja niishie hapa story ndefu na inachekesha mwishoni.
Bado mpo pamoja?
 
Niliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.

Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.

Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.

Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.

Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.

Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.

Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughurikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.

Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.

Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.

Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.

Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
Kama ulimuacha apo ndio ulicheza kama pele
 
Angepanda boda akifika penye hela achukue alipe. Mbona simple sana.
Simple kupitia story sio reality.
-kumbuka ametoka kuzodolewa na wadada wenzake polisi, amepanic, unategemea atakuwa na utulivu wa akili kufanya uamuzi huo.
- kumbuka polisi nili demand nipelekwe mahakamani, (hatukumaliza kwa amani) yeye angekuwa na uhakika gani kuwa nitamruhusu kuingia ndani achukue hela alipe boda boda?
 
Niliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.

Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.

Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.

Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.

Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.

Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.

Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughurikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.

Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.

Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.

Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.

Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
"kishikaji" au ulihonga?
 
Afande alinifuata korokoroni alfajiri akanipa njia ya kujinasua kwenda mahakamani nayo ni kumpa 50k, nilimuelewa na ndivyo tulivyomalizana kishikaji kwa kumpa afande hiyo hela,
Afande alichukua pesa kukuweka ndani toka kwa mkeo, na akachukua 50k toka kwako kukutoa nje. Usifikiri alikusaidia sana hapana, ni vile ungeenda mahakaman asingepata kitu
sijui afande alivyomwambia mke wangu, Ila my wife aliniambia tu kuwa kafuta kesi hivyo twende nyumbani.
Subir kwanza, ina maana ni yf wako mdio alikufuata tena kwamba twende nyumban nimefuta kesi? Kwamba huruma ilimrudia ? Ahahaha.
 
Mimi mke wangu alichukua 3M ya biashara akamkopesha shoga yake anaedaiwa kwenye mikopo nyonya damu wakati shoga yake hana kazi yoyote itakayo msaidia kulipa hilo deni.
Ikabidi niende polisi mwenyewe nikawaambia polisi waniweke ndani maana nikibaki nje ntamuua wife.
Vere good mkuu kuliko kuua
 
Back
Top Bottom