Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Wewe utakuwa ni yule afande, nina mashaka na wewe Ila siwezi kukufatilia hizo maokoto ulizotupiga ulizinywea pombe na mbuzi choma kule kwa mrombo πŸ˜‚
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa kifupi yaani ulioga kwanza halafu ukapaka sabuni.
 
Unajiepusha na mengi boss, usije fumua mtu ubongo kisa kuonyesha wewe ni mwanaume, na ukikaa hapo uvumilivu utakushinda, kuondoka ndo suluhisho sahihi.
Nina jamaa zangu wa karibu wawili waliishia kwenye majanga makubwa kwa sababu ya ubabe. mmoja alimuua muhudumu wa baa baada ya kunywa bia zetu na kukataa kuondooka naye, yaani alimpiga teke moja tu tumboni ikawa jumla. Wa pili alipigwa mshale na mlinzi wa kimasai tukiwa baa tunakunywa pombe, kwa sababu tu ya ubabe pasipo lazima. Wa tatu sikuwa na ukaribu naye ila alisota sana lupango kwa kumuua hawara ya dada yake, kwa sbabu za kitoto na kushindwa kuzuia hasira. Historia ni mwalimu mzuri sana kwenye maisha, mimi sipigi mwanamkewala sipigani na mtu kamwe.
 
Aisee, Wewe una uzoefu mkuu.
 
Aisee, Wewe una uzoefu mkuu.
Mkuu, kwa umri nilioishi hapa duniani nina uzoefu kiasi chake. Yule jamaa yangu aliyepigwa mshale na mmasai, kifo chake kiliniuma sana. Tumefika mpaka hospitali ya mkoa hatukupata huduma kwa wakati, mwamba kafia mapajani kwangu tukiwa mapokezi ya hospitali na ni usiku mkubwa. Yaani nikikumbuka huwa inaniuma sana, yule mmasai hakutumia akili hata kidogo.
 
Inaumiza aisee. Najaribu kupiga picha mtu wako wa karibu anakufia mikononi huku unamtazama.
 
Ulitaka mwana afanye nini wewe mnyiramba..?
 
Kipindi nikiwa na umri wa ujana ujana zaidi, nilikua nawashangaa sana wanaume wanao wapa makofi wake zao pale wanapovuka mipaka, Ila sasa baada kuingia utu uzima nimekuja kugundua wale wazamani walikua hawatembezi vibao kisawa sawa, Dozi ilitakiwa kuwa kubwa zaidi ya nilivokua naona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…