Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Mkeo alifanya uamuzi sahihi ila wewe na gubu lako ukashindwa kuelewa! Siku hiyo ulimpiga vibao asingeenda polisi kuna siku ungempiga na mwichi ukamuua kabisa.

Ingekuwa huyo shemeji kapatwa na tatizo lenye tija mwanamke angekuwa sahihi!! Even me kakamatwa kwa uhalifu wake nipoteze pesa zangu mimi!?

Upuuzi huo sifanyi!!!
 
Ondoa huo uchungu ulioubeba juu ya ex wife wako; ndiyo unaokusukuma kumchukia hata binti ambaye ume-share naye since binti ni part ya mama yake. Muepushe binti yako na trauma ambazo unaweza kuzizuia ukiamua na ukampa binti yako maisha mazuri sana hapa duniani especially with your "presence"
Ngoja nitafakari zaidi, umeongea kitu imegusa ndani ya moyo wangu.

Naweza kukachukua ka baby girl huko mbeleni.

Asante kwa ushauri.
 
Vyeti na nguo zako viko wapi na je hakn kikao kimekaha mjadiliwe ?
Vyeti nilitunziaga kwa baba yangu baada ya kumaliza masomo vipo huko hadi leo.

Sikuwahi kushawika kufanya vikao bali niliondoka na nguo nilizokuwa nimevaa tu, hizo zingine nilimwachia.
 
Mshauri wa aina yako ni wa kufungwa kamba ngumu ya katani mikononi na miguuni,kupandishwa kwenye carriers au boots za mabasi ya kuelekea Dodoma.Na ukifikishwa huko ni moja kwa moja upelekwe kwenye ile hotel ya nyota tano inayoitwa "Milembe Resorts and Hotels" uishi kwa raha hata miaka mitano.
Dah...humu ndani kuna majibu si mchezo ...kinachonifanya nicheke zaidi hadi machozi ni jamaa alichoandika na wewe ulichojibu...aisee watu mnamajibu.

Hii imenikumbusha kaka yangu mmoja mtu mzima sana ila majibu nihivihivi, jamaa ana busara sana sasa kosa ujichanganye utapewa jibu hilo haangalii maza, sijui mzee mtoto, kiongozi wa dini au yeyote ila we jichangange.
 
Doohh sad sad..bas inaweza ikawa hata ulichowaza kuhusu dogo yaweza kuwa sahihi kuwa sio mwanao. Vinginevyo angekutafuta kwa ajil ya mtoto walau umuone
Mkuu nilimvumilia kwa mengi huyo mpuuzi, haeleweki kabisa, lile tukio la kunilaza selo ndio liliamua hatima ya mahusiano yetu, nilaachana naye mazima
 
Uliyekuwa ukimuita mkeo awe na chuki binafsi na wewe?
-Ulifanya kosa kisheria kumpiga.
-ulimpiga baada ya kuwa na hasira.
-mngeachwa mrudi wote nyumbani lazima/kuna uwezekano ungemkoyonga tena ndiyo mkatenganishwa.
NB;Kutupwa selo ilikuwa ni njia bora ya kuwatuliza wote wawili hasira ziwatoke akilini na mtafakari upya mambo yenu.Halafu,hukutaka kukubali moyoni mwako kwamba ulikosea kupiga. Na mwishowe ukaikimbia nyumba na kumtwisha lawama mtu unayemwita "mnyiramba" badala ya kulijutia kosa lako.Hadi mke anang'ang'ania umpe hela ambazo kiuhalisia yawezekana haukuwa nazo umeonesha huna uwezo wa kujieleza,kumshawishi mtu akuamini na kusuluhisha mambo kwa amani.
mnyiramba
 
Back
Top Bottom