Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Kuna mtu nilimpendaga humu jf. Jamani alinitesa sana..namuwaza 24/7. Aliniteka vibaya mno na nilikuwa tayari kwa lolote...ila akawa na moods za ajabu ajabu tukaachana ila nilimpenda for real.
Nasoma comments zake zote na avatar yake matata sana ni picha yake halisi.
.
.
Tuliachana bila kuonana. Utakaposoma hii comment jua kwamba ni kweli nilikupenda na mipango yote niliyowaza juu yako ilikuwa ya kweli.
Nimeshamove on, na Jana ndo nimefuta namba yako wakati napitia contacts kwenye phone book.
I wish nimjue huyu aliyechezea bahati..
 
Tuwe makini tu Mkuu Kaboom, binafsi hii ID hii imetumiwa na watu wengi kwa nyakati tofauti-tofauti ( MALCOM LUMUMBA) ni zaidi ya mtu mmoja hivyo siyo rahisi kukishawishi kikundi cha watu. Lakini ningekuwa mimi peke yangu huenda ningekuwa nishashawishika na ofa zinazotolewa. Tanzania is not a safe country anymore, but most people do not realise this: We live in a de-facto Mafia State full of malignant and evil people.
Hapa kichakani umakini ni kitu muhimu sana..Hapo kwenye ID ya MALCOM LUMUMBA kutumiwa na watu wengi sikuwahi kulijua/kulifikiria hili..Uzuri ni kwamba sijawahi kuona ikitumika vibaya..
 
Hisia zangu zimeniambia ni bahati..Japo usemalo ni kweli..Mana hisia zangu zimeshawahi kuniangusha mara kadhaa..Btw ikawaje mkaishia hewani tu bila kuonana..Kikwazo kilikuwa nn??
Yupo nje ya nchi so hatukuweza kuonana kwa haraka, lkn mawasiliano yalikuwa mazuri tu.
Tulipotezeana maana kila mara tutagombana kwa mambo madogo madogo, nikaona loh hebu niachane na haya mambo ya kusadikika.
 
Yupo nje ya nchi so hatukuweza kuonana kwa haraka, lkn mawasiliano yalikuwa mazuri tu.
Tulipotezeana maana kila mara tutagombana kwa mambo madogo madogo, nikaona loh hebu niachane na haya mambo ya kusadikika.
Eti ya kusadikika..Kama mlipotezeana na kila mmoja akaona sawa basi halikuwa fungu lako hilo..
 
[emoji3][emoji3][emoji3] sio wewe. Yaani baada ya kuachana (hatukuambiana tumeachana tulipotezeana tu). Nikawa namchungulia kila dakika, nafatilia comments zake...akiflirt na wadada naumiaaaa. Dah mapenzi ya kipuuzi ona. Am glad nilitoka huko...
Nilijuaga nilikuwa peke yangu😄😄😄

Hisia za kimapenzi Goodmorning
 
Habari za wakati huu wakuu

Wakuu hadi naandika hapa binafsi huwa natokewa na hali hii for instance, kupitia mitandao ya kijamii mfano, hapa jf kupitia mada au comment za mtu unaweza jikuta unampenda mtu usiemfahamu.

Mara kadhaa hali hii huwatokea watu na ushahidi anao kila aliewahi kutokewa na hali hii. Note: sio lazima umpende kimapenzi japo inatokea kuna wengine anapenda tu japo aone comments zako au kila anapoingia online lazima apitie profile kwako au timeline yako.

Mbaya zaidi sasa, watu wanaogopana sana humu ndani kiasi kwamba hata ukivutiwa nae au amevutiwa na wewe unapata/anapata shida anaanzanje/unaanzaje kumuaminisha kuwa wewe ni mtu mwema kwake na huna nia ovu.

Mkijitahidi sana mtachat PM akiona niaje niaje anakupiga block kimasihara. Offcoz nafahamu wapo wengi wenye mgongano wa aina hii ya kuvutiwa na baadhi ya watu hususani humu ndani watatoa ushuhuda hapa.

Ninae mpenda akisoma hii thread atajijuwa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Umenikumbusha mbali sana enzi hizo nilimpendaga member mmoja wa JF maarufu enzi hizo kwa jina la rubii
ukweli sikuwahi kumfahamu kwa sura ila taratibu nilijikuta nampenda mpaka kutamani kumwoa nilimsumbua sana inbox mpaka ikafika wakati nikaanzisha uzi kwa ajili yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sema alinichomolea nje sababu kubwa ni baada ya kujua mimi nauzaga majeneza hii kitu ilimfanya anikatae lakini sio mbaya baadae nilifanikiwa kumfahamu kupitia picha kwa msaada wa member mmoja wa kike ambaye alikuwa anafahamiana naye japo aliniomba ibaki kuwa siri ila ndo nilifanikiwa kuona picha halisi za mdada na kufahamu maisha yake halisi nje ya JF kifupi alikuwa ni mdada flani mstaarabu na anajielewa.
 
Sasa si afadhali muwe mshawahi onana[emoji3], hlf wewe nimekumbuka hujawahi umizwa na mapenzi
madame tuendelee kuchat tu😄😄

Hiyo tarehe 2/5/2015..siwezi isahau..mbali na kwamba ndio tarehe na mwezi wa kuzaliwa mamake Chakorii...lakini pia ndio ulioniwekea historia nzuri kwenye mahusiano 😄😄hatari sana

***** mapenzi ya kikuda kichizi..
 
Tatizo siyo kutumiwa ujumbe au kusumbuliwa PM, tatizo ni uharamia unaofanywa na watu waovu huku mitandaoni. Tunawindana kama wanyama, hasahasa pale unapokuwa mkosoaji mkubwa mwenye mawazo ya tofauti ua ushawishi dhidi ya chama tawala. Matapeli nao hawako nyuma, wameumiza watu wengi sana humu ndani. Usipokuwa makini utaumizwa vibaya,.........
Vipi tusiokuwa na mlengwa wa siasa hatukosoi wala kusifia na hata issue za mapenzi hatupo watanishawishi kwa lipi.?
 
Pamoja na misimamo yake ila hua nampenda sana cariha

Yaani kuna muda natamani nimjibu ila naacha hata akiandika kitu sikipendi

Yaani nikiona avatar na nikisoma maneno yake nikayawekea sauti namuona kama anaongea hivi
Naishia kumpenda

Nahisi alivyo akinifokea nikikosea nitafurahi
Napenda kufokewa na manzi angu nikikosea hua nahisi u romantic fulani hivi na wanawake wa aina hiyo ukimfokea anakaa kimya mara moja

Carihaaaa uko wapi
 
Back
Top Bottom