Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

I wish nimjue huyu aliyechezea bahati..
 
Hapa kichakani umakini ni kitu muhimu sana..Hapo kwenye ID ya MALCOM LUMUMBA kutumiwa na watu wengi sikuwahi kulijua/kulifikiria hili..Uzuri ni kwamba sijawahi kuona ikitumika vibaya..
 
Hisia zangu zimeniambia ni bahati..Japo usemalo ni kweli..Mana hisia zangu zimeshawahi kuniangusha mara kadhaa..Btw ikawaje mkaishia hewani tu bila kuonana..Kikwazo kilikuwa nn??
Yupo nje ya nchi so hatukuweza kuonana kwa haraka, lkn mawasiliano yalikuwa mazuri tu.
Tulipotezeana maana kila mara tutagombana kwa mambo madogo madogo, nikaona loh hebu niachane na haya mambo ya kusadikika.
 
Yupo nje ya nchi so hatukuweza kuonana kwa haraka, lkn mawasiliano yalikuwa mazuri tu.
Tulipotezeana maana kila mara tutagombana kwa mambo madogo madogo, nikaona loh hebu niachane na haya mambo ya kusadikika.
Eti ya kusadikika..Kama mlipotezeana na kila mmoja akaona sawa basi halikuwa fungu lako hilo..
 
[emoji3][emoji3][emoji3] sio wewe. Yaani baada ya kuachana (hatukuambiana tumeachana tulipotezeana tu). Nikawa namchungulia kila dakika, nafatilia comments zake...akiflirt na wadada naumiaaaa. Dah mapenzi ya kipuuzi ona. Am glad nilitoka huko...
Nilijuaga nilikuwa peke yangu😄😄😄

Hisia za kimapenzi Goodmorning
 
Umenikumbusha mbali sana enzi hizo nilimpendaga member mmoja wa JF maarufu enzi hizo kwa jina la rubii
ukweli sikuwahi kumfahamu kwa sura ila taratibu nilijikuta nampenda mpaka kutamani kumwoa nilimsumbua sana inbox mpaka ikafika wakati nikaanzisha uzi kwa ajili yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sema alinichomolea nje sababu kubwa ni baada ya kujua mimi nauzaga majeneza hii kitu ilimfanya anikatae lakini sio mbaya baadae nilifanikiwa kumfahamu kupitia picha kwa msaada wa member mmoja wa kike ambaye alikuwa anafahamiana naye japo aliniomba ibaki kuwa siri ila ndo nilifanikiwa kuona picha halisi za mdada na kufahamu maisha yake halisi nje ya JF kifupi alikuwa ni mdada flani mstaarabu na anajielewa.
 
Sasa si afadhali muwe mshawahi onana[emoji3], hlf wewe nimekumbuka hujawahi umizwa na mapenzi
madame tuendelee kuchat tu😄😄

Hiyo tarehe 2/5/2015..siwezi isahau..mbali na kwamba ndio tarehe na mwezi wa kuzaliwa mamake Chakorii...lakini pia ndio ulioniwekea historia nzuri kwenye mahusiano 😄😄hatari sana

***** mapenzi ya kikuda kichizi..
 
Vipi tusiokuwa na mlengwa wa siasa hatukosoi wala kusifia na hata issue za mapenzi hatupo watanishawishi kwa lipi.?
 
Pamoja na misimamo yake ila hua nampenda sana cariha

Yaani kuna muda natamani nimjibu ila naacha hata akiandika kitu sikipendi

Yaani nikiona avatar na nikisoma maneno yake nikayawekea sauti namuona kama anaongea hivi
Naishia kumpenda

Nahisi alivyo akinifokea nikikosea nitafurahi
Napenda kufokewa na manzi angu nikikosea hua nahisi u romantic fulani hivi na wanawake wa aina hiyo ukimfokea anakaa kimya mara moja

Carihaaaa uko wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…