Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Halafu nimekumbuka ulisema uliona avatar yake inayumbayumba mahali humu nikakuuliza ameshacomment humu au bado? Hivi ulishanijibu?
Nilisema nimeiona avatar yake ikiyumba yumba lakini si kwenye huu uzi.

Huku bado hajaingia ila nilimuona sehemu fulani fulani hivi nikahisi harufu ya makopa kopa yanaanza kuota😄😄hatari sana.

Akiingia humu nitafurahi sana 🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️
 
Binafsi nimewasiliana na wanachama wengi humu ndani (ME + KE), lakini mbali na kuleteana masikhara na kudanganyana kule PM sijawahi kabisa kutaka kufahamiana na mtu humu ndani. Naamini kuna waliokuwa na nia njema na wako Genuine, lakini waovu, wauaji, watekaji, mamluki na matapeli wako wengi sana mitandaoni. Hivyo wale watu wema wanisamehe tu.........

Nashauri vijana, hata kama umependa na kuvutiwa na mwandiko wa mtu, fahamu kwamba huku kwenye mitandao kila mtu huonekana ni malaika japo uhalisia hauko hivyo. Nawafahamu watu ambao wameshaumizwa na kuvurugwa kisa haya mawasiliano ya humu JF, Twitter na Instagram. Binafsi nimewahi kutumiwa links za mitego na E-Mails nyingi huko PM.

Wengine wanaanzia mbali kwa kujenga urafiki mimi nawachora tu nasema Hiiiiiiiiiiiiiiiii. Huko PM nimepewa ofa kubwa za kufa mtu, wengine wanasema wananipenda sana (wanajaribu kunijaza Sweet-Nothing) , wengine wananiletea vitisho,wengine wanataka ushauri, wengine wananiletea umbeya na majungu, wengine wanakuja kunimwagia misifa. Sasa kama ukiwa na kichwa kibovu itakula kwako. There's No Free Lunch in the World: You Eat the Devil's Food, You Pay the Devil's Bill....

Ila kama umempenda mtu wewe jilipue at your own risk, lakini kaa ukikumbuka kwamba waliomo humu ndiyo haohao wa mtaani kwako. Tanzania ya leo imejaa watu waovu wengi mno, tumefika pabaya sana, kuwa makini (Be vigilant and don't have unrealistic expectations).....

Una nakosea ndugu Mgonga Like ???
Umenena vyema, nimependa hapo you eat devil's food, you pay devil's bill😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom