Ulishawahi kusingiziwa ujauzito wakati wewe si muhusika? Je, ulifanyaje kukabiliana na hali hiyo?

1. Kitanda hakizai haramu
2. Kuchapiwa ni siri ya ndani
3. Kuchapiwa hakuepukiki
4. DNA
5. Kwa sasa usikwepe majukumu [emoji2221][emoji2221][emoji2221][emoji2221]
Hii inatokana na utamaduni wa makabila fulanifulani haswa wafugaji na wa pwani. Wafugaji wanasema kama jike lako likipandwa machungani huyo ndama ni wa mwenye jike au dume? Na hawa wa ngomani wanaojua fika kinachoendelea huko unategemea wawe na kesi za kujadili mimba?
Watoto wa machungani na ngomani ni wengi mno!
 
Kuna tetesi nliskia et kua ukienda pima DNA lazma tu matokeo yatakuja kua "ww ndio baba" lengo lao likiwa ni kupunguza watoto yatima sjui haki za mama na mtoto blah blah.. Kuna ukweli hapa?
Hili jambo niliwahi kusikia toka kwa rafiki yangu kituo cha afya hivyo hivyo.
Sasa uhitaji wa DNA haupo!
 
Dah,hii kitu ilinitokea miaka ya 2003 nilipata kuwa na mdada dizaini mdangaji fulani mana nilikua simuelewi elewi,katika harakati za mahusiano nikaja kumkuta "red handed"anabambiwa uchochoroni nilikua na washkaji kwa bahati nzuri mimi ndio niliyemuona Mana si unajua mtu chake mana ilikua saa nne usiku.
Nikawashtua jamaa tukarudi mpaka pale wakamsalimia kisha tukaendelea na safari yet na ndio ukawa mwisho wa mahusiano yetu,haikupita mwezi yule binti akaondoka kwenye ile nyumba ambayo alikua akiishi.
Baadae sana ndio nikaja pata stori yake kuwa kipindi anaondoka alikua mjamzito hivyo maisha yalikua magumu akaamua kwenda kwa dada yake kwani alijaribu kwa wanaume kama watatu kuwabebesha ule mzigo wote wakakataa ila bahati ikawa upande alipofika kwa dada ake kuna lijamaa akazimia mzigo akapewa ile mimba mana yule dada alikua na tumbo zuri kweli nafikiri wazoefu wananielewa hapo mana halionekani.
Jamaa akamsogeza akalea mimba na mtoto,nikaja kuonana nae kwa bahati mbaya kweli mwaka 2007 mwishoni mtoto mkubwa hapo, alikua na mawifi zake,dah nafikiri mawifi waliona aibu.....
 
Vipi mtoto umefanana nae????[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Daah...kweli tunatofautiana na ndo uzuri wa Jf.

Binafsi ni fan mkubwa sana wa hawa madogo wanaozaliwa kiutatautata hivi, mara cjui dingi kakana mimba siyo yake mara dingi cjui kapotea mazima mara cjui maza kataka kumtia dogo maliwatoni.

Madogo dizaini hizi wanakuwa bold sana hlf wana spirit ya kuwa independent mapema sana, wengi wao sio lelemama ukilinganisha na hawa tunaosema ni wetu OG. Ukimtupa popote yey anastawi. Ni kama mungu anawasimamia sana.

Kwangu mmama akijimix akanipa dogo kwa dizaini hizi bas imekula kwake nitamtwaa huyo dogo tu na kuhakikisha tunasainishana kabisa kuondoa utata wowote huko mbeleni.

Mtoto akishazaliwa anahitaji malezi tu na miongozo unapata jembe lako safi la bdae. Sie wote ni waja hujui nani atakusaidia hapo bdae.
 
dah kwa mwanaume kusingiziwa mtoto ni kawaida sana nilishapatwa na huo mkasa,jambo la kwanza baada ya kuhisi mtoto anaweza asiwe wangu nilituliza akili na kujiuliza nifanye nini kujua ukweli pasipo kumshilikisha huyo mwanamke.na hapo ndo nilipofankiwa maana nilifanya action moja matata sana yaani mwanamke niliendelea kuishi nae bila kuonesha utofauti huku nikikusanya data mpaka nilipofikisha asilimia 90 ya ushahidi ndo nikaweka kikao,lkn hicho kikao nilikipa kichwa cha habari "KIKAO CHA AWALI CHA NDOA".nikaomba aje na ndug yake mmoja kama muwakilishi na mimi nikaita ndugu zangu watatu ambao nilishawapanga kila kitu,nikamwaga data zangu nilizokusanya mwezi mzima tena kwa kumtumia yeye bila yeye mwenyewe kujua.tulimbana mpk akakubali na picha likaishia hapo japo haikua rahisi hata huko kukubali kwenyewe ndugu yangu mmoja alitumia plan B kwenye kikao baada ya plan A kuchelewesha matokeo,ila kuanzia cku hiyo ndo nilijua kwamba ningezingatia masomo ningekua mpelelezi maana nilifanikiwa kwa vitu vikuu vitatu ,(BUSARA,UVUMILIVU na AKILI)
 
Nmekuelewa vyema sana Mkuu... Ahsantee!
 
Unaibiwaa[emoji444][emoji444]kawimbo ya rayvany
 
According to yeye anasema ujauzito una week saba but me nlisha-suspect tangu kitambo and nkamwambie bas tukapime kama ana ujauzito akawa "Hataki"... Just imagine mtu hataki kujua hali yake ya Afya?!?? Especially swala la ujauzito?
Subiri mtoto azaliwe kma ni wako kuna vitu mtafanania,eidha vidole,masikio,macho,mdomo etc hakuna haja ya dna ni wewe mwenyewe
 
Tafuta ndugu unaemwamini zungumza nae mashaka yako juu ya huyo mwanamke, fanya jitihada za kupata ushahidi Kama kupima Kenya kimya kimya,

Kwa mujibu wa mada yako hii ni wazi hiyo mimba sio yako
 
Pole sana ndugu..je umeoa? Una watoto? Huyo mwanamke ni mfanyakazi au hajishughulishi? Tuliza sana kichwa katika kipindi hiki..subiri akizaliwa mtoto utapata. Majibu ya mashaka yako
 
Tafuta ndugu unaemwamini zungumza nae mashaka yako juu ya huyo mwanamke, fanya jitihada za kupata ushahidi Kama kupima Kenya kimya kimya,

Kwa mujibu wa mada yako hii ni wazi hiyo mimba sio yako
Ahsantee sana mkuu!
 
Pole sana ndugu..je umeoa? Una watoto? Huyo mwanamke ni mfanyakazi au hajishughulishi? Tuliza sana kichwa katika kipindi hiki..subiri akizaliwa mtoto utapata. Majibu ya mashaka yako
Hapana sijaoa na sina watoto , yeye anafanya shughuli ndogo ndogo tu.
 
Asee, kwa jibu lake ilo, mie ningepiga chini haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…