Zero Conscious
JF-Expert Member
- Apr 23, 2022
- 254
- 519
Wakuu habari za wakati huu! Nina Imani mu wazima wa afya na mnaendelea kupambana na maisha ya Kila siku. Mungu atusaidie sana.
Kama ambavyo title inajieleza, Mimi ni mtu ambae sina marafiki wengi, si kwakuwa ninajiskia sana, hapana ila ni aina ya watu ambao ninaweza kusema ni introvert. Nina marafiki wachache tu ambao nina amani sana kuwa nao.
Sasa kuna mmoja ambae ndio mtu wa karibu zaidi, jambo lake ni langu na langu ni lake, tumesaidizana kwenye nyakati ngumu na hatukuwahi kutengana kote tulikopita kama marafiki. Hatuna maisha mazuri kwakuwa bado ni vijana na tunapambana kutafuta angalau siku moja tuwe kwenye nafasi nzuri pia kimaisha.
Sasa changamoto imekuja kuonekana baada ya huyu mwenzangu kuwa amebahatika kupata chaka sehemu, yaani imekuwa si yeye ninaemfahamu tena. Kwa ukaribu wangu na yeye sidhani hata kama ni kubanana inaweza kuwa kwa mwenendo huu anaouonyesha.
Imekuwa ni mara chache sana siku hizi kuonana tena involuntarily ingawa najua yupo, na baadhi ya watu anakutana nao anapokuwa nje ya majukumu yake ila si mimi tena. Unaweza kumtumia ujumbe usijibiwe kabisa na tangu aanze kazi nakumbuka alinitumia ujumbe siku mbili tu za kwanza tangu alipoanza kazi.
Kiufupi sijapendezwa na mwenendo huo, muda mwingine asiponijibu ujumbe au simu yangu najisikia unyonge sana. Najiona kama nimepoteza nafasi kama rafiki kwake kutokana na aidha anahisi ntamlilia shida au sina msaada tena kwake. Silaumu yeye kupata kazi sababu mwisho wa siku haya ni maisha, tunatakiwa kukua kuelekea hatua nyingine. Mwenzangu katangulia ilhali wakati wangu wa milango kufunguka Bado..
It pains, kwa nyakati tulizifanikiwa kukutana tangu apate kazi anaonyesha kabisa he doesn't care about me and not interested with me anymore,, even jokes we used to make Hana response nazo kabisa. Mnaweza kuwa kwenye maongezi ghafla tu utaiskia anasema nataka niende kwa akina flani, like he's escaping me. Nimeamua kuacha kumtafuta pia sababu nishakuwa inferior kwa jinsi asivyojali tena kuhusu Mimi.
Ndipo nimepata kujifunza kuwa vitu vidogo sana huua urafiki.Si kwamba nahitaji pesa Toka kwake, it's all about value of friendship (THAMANI YA URAFIKI), Sawa naweza kukwama nikahitaji msaada kwake kama kawaida lakini si kudepend moja kwa moja kwenye kile alichonacho. Mara nyingi tu nimemshika mkono kipindi mambo yangu yanakwenda sawa, nimenusuru mahusiano yake zaidi ya mara moja, nimemvusha kifedha kipindi Mwanamke wake kalazimisha kuja ilhali hakuwa na pesa, nilimkabidhi sehemu ninayokaa Ili aenjoy na Mwanamke wake as a best friend of me. Treatment nayoipata sasa ndio inayoninyima furaha, sitegemei kama atajali tena lolote kati yangu naye. Nadhani kakutana na watu wapya, wa category yake ndio maana imekuwa hivi.
Anyway, Mi bado muangaikaji ambae siijui kesho yangu inakucha vipi ila naamini Mungu atanionyesha mlango pia. Tusiwapuuze watu tunaokuwa nao kwenye kipindi kigumu pindi tunapofunguliwa njia za mafanikio. Japo kuna ubize lakini si mbaya tukajuliana Hali tu..
Asanteni wakuu🙏, dondosha pia kisa chako