Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Mungu huruhusu tukutane na watu kwa wakati maalum na pia kwa sababu maalum.ulipaswa ujue huyo unayemwita rafiki ulikutana naye ili iweje? Ukute hukupaswa hata kumwita rafiki
 
Lazima akuogope maana ww ni malaika wa kifo
 
Mimi yupo mmoja huyo alikuwa ananijaribu siku nampigia anatuma message Eti piga [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kisa kapata kazi nimemchunia mpaka leo kajirudisha hapa mm tayari sio rafiki angu tena saiv yy ndo anapiga simu kila siku
 
Vp alikuja kuwa girl friend wako?
 
Kuna msela ambaye alifukuzwa shule ya msingi akiwa darasa la 4, me nikamchukua nikampeleka kwenye shule ambayo nilikuwa nasomea mimi kwakuwa nilikuwa monitor wa darasa na majina nilikuwa naita mimi basi nikamuandikisaha akasoma kama miezi 3 hivi ndo walimu wanakuja shituka heee, huyu mbona kwenye vitabu vyetu hatumfahamu basi kubanwa nikatajwa alimanusura nifukuzwe shule ila tu mkuu wa shule alikuwa ananikuli sana toka ni toke nikachwapwa fimbo za kuzugia nikaendelea na masomo,

Msela tulipo maliza sekondari akapewa piki piki mpya na dingi yake kama mnavyojuwa miaka hiyo boda boda zilikuwa zinalipa akaanza kunionyeshea vidharau na kusema haweziongea na mimi wakati tulikuwa mabest balaa,
Tangu siku hiyo me sina rafiki maalum,

Kisa cha pili,
Jfm, nilipata rafiki mdada furani hivi anaitwa JANETH, nilikuwa namkubali sana tukawa tunawasiliana whatsapp na sms za kawaida, inshort nilifurahiya kampani yake ila alivyo niblock bila sababu iliniuma sana,
Janeth popote ulipo juwa nakukubali mpaka leo, maana ulikuwa na ushauri wa maendeleo.
najuwa utasoma uzi huu pia utaona comment yangu.
 
Kupata washikaji ukiwa na pesa ni rahisi...
Ukipata na hauna kitu jua umefanikiwa kichizi mi sikufichi...
 
Janeth nae!

Pole sana, au ulitupia vocal na yeye hakupendezewa?
 
Hii inatokea sana mzee mana nyingi wakishakua wako sehemu wanabadilisha marafiki wanataka wale wa level moja, ila wakikwama wanakumbuka walipotoka. Kikubwa pambania kesho yako mzee
Maneno kuntu haya.

Mimi kuna mmoja baada ya miaka miwili kupita tangu aliponikataa, tulikutana sehemu kibahati mbaya.

Akaanza kujishaua kwasababu ameona mabadiliko upande wangu, na akaomba udhamini kwenye miradi yake nimuongezee nguvu, ingawa hakuniambia moja kwa moja amejifanya kuniomba nimsaidie wadhamini kwasababu biashara zake zimeyumba.

Sikutaka kumkatisha tamaa, nilimuitikia kinafiki, lakini moyoni nikawa najiambia watu wepesi kusahau tena wanasahau haraka sana.

Huyu ni mmoja wapo, ila wapo wengi wa sampuli hii.

Nashukuru nimepata funzo kutoka kwao, kama utaamua kusaidia, saidia lakini usijitoe kivile ukitegemea kwamba fadhila italipwa, sahau
 
Yote maisha tu tutakutana kwenye ATM halafu mikausho mikali
Na ndio mpango mzima.....mm kuna jamaa/rafiki yangu alikua kakwama sana tena sanaaa nika msupport kabiashara flan ambako yy ali kaplan basi ikawa story nyiingi za malalamiko kua hali "tete"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ biashara ngumuu kuumbe nayy anajurusha kinyemela, nika mwachia tu ili ajikim maisha ya endelee lkn ile biashara ikafa.......lkn tegemeo kubwa kubwa nita ibust biashara niikipata ishu ya Sensa nikamwambia hongera sana km ume pata sa'bu alikua na uhakika nayo kuipata, sasahv hata salam hakuna hata what's app hata kureply ukimaliza jambo flan la mtaani tu, wkt ilikua ni km ada kweke nikiwa online tu lzm ukute ujumbe wake wa kunijulia hali au ukifika jioni saa 12 azima apige simu hata kwasimu yyt ili ajue nipo ktk kinywaji au lah atie timu nahii ilikua kdg km kero sometimes namyeyusha kua sijarudi mtaani....... Lkn namimi nilikua nimesha mstukia nikamfanya km daraja tu la company tag ubavuni😊 maisha ya endelee........ Marafiki niwakua nao makini sana wakati huu wengi wanapenda kia chawa na mteremko lkn ujanja niku block vimisaada na kuto watembezea vibia, dawa yao ni K-Vant kubwa tu no Bia alafu wazime WADUNDWE alafu unawakataa mapema mnooπŸƒπŸƒπŸƒ πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…