Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Kifupi mswahili Ni mbwa.
Msaidie Ila usije ukategemea msaada kutoka kwake. Hata salaam sahau.
Ndugu yako ni mke/mume wako na watoto wako tu. Sahau kitu inaitwa dada au Kaka.
Take it from me and thank me later.
Mkuu kuna bwana ni rafiki yangu toka primary akapata Kazi taasisi flani Maisha safi kwa maana ya nyumba na gari ila aliwahi Nipa 15,000 elfu tu kipindi chote cha urafiki

Nikapigana kujitolea kwenye ile taasisi wakakubali, nimekaa pale jamaa hana msaada kwangu nikachaguliwa kwenda kusimamia tawi lingine

Jamaa akatolewa kazini, msaada ukawa ni mimi (mwaka mzima namsaidia) akapata Kazi daah nikakwama sehemu jamaa nikaomba anikopeshe laki 2 nikija mjini nalipa Hadi leo jamaa hapokei simu yangu kisa laki 2 na nafahamu anayo Iyo hela ila ajataka Nipa.

Kifupi jamaa ni mtu wa kujijali yeye tu ila akipata shida anapenda omba msaada na ukimkazia maneno ni mengi mnooo
 
Mleta mada acha kuhangaika na mtu,suala la urafiki ni la hisia na makubaliano yaliyo nje ya sheria ndio maana kuvunja urafiki ni simple kuliko kutoa talaka.
Pambana na hali yako kama unapenda marafiki utapata wengi sana endapo ukiwa na pesa kama huna ww huna rafiki zaidi ya maadui.
 
Aisee mimi ni vice versa,miaka karibu nane toka nikutane na mshikaji alikua kamaliza chuo maisha yanamchapa mimi wala sikumfanyia wema wowote wa maana sana ila tulitokea kua washkaji sana maisha yangu ni kuunga tu mwana alikuja kula mashavu sehemu ya maana hajawahi kuniletea dharau au kunikataa hata siku moja huwa ananisaidia mnoo kipesa na kimawazo,kuna siku kaja kwenye goli langu kuna dada mmoja huwa ni mteja wangu japo ana dharau wakakutana kumbe jamaa ni boss wa dada na dada alimnyenyekea kinoma ila alishangaa ninavoongea nae kisela tena hadi kumtukana sometimes japo kiutani.
HUWA ROHO INANIUMA SANA NI LINI NITAKUJA KULIPA FADHILA ZA MSHIKAJI TENA YEYE ANAFANYA YOTE HAYO KUKIWA HAKUNA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA MIMI KUJA KUMZIDI KIMAISHA.


Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mi nilivyo jeuri uwiii sijaligi tena napenda.
Mana nilikujaga kugundua nnaowaita marafiki ni maadui zangu namba 1 nikaona kumbe urafiki hauna maana...
Maisha yanilize kwa ugumu bado tena na hao So- called friends niumie wakiniacha... puuuh!! Waende kwa amani
 
Vijana mkipata mfereji kidgo mnajionaga mpo smart sana.

Nakupunguza tu hatuna tena common ground ndo uhalisia wa maisha. Wewe unataka tuongelee Simba/Yanga day siku nzima, me nawaza kutanua biashara zangu. Ndege hufananao huruka pamoja.

Sisemi mpira au bata ni mbaya, mwenyewe ni mla bata namba moja hapa ila kila jambo na kiasi.
 
Ni kawaida kabisa mm kunawqtu tulikuwa ofisi moja baada ya kupunguzwa kazini tulikuwa na group letu tunafarijiana ila baada ya kuwa mmoja baada ya mwinhine anapata nafasi nkaanza kuona hata ukaribu unapungua hata simu hakuna no chat kwa group mtu anakupita kiwizi wizi usimuone jamani .maisha haya
 
Acha undezi tafuta pesa hakuna aliekutenga
 
Back
Top Bottom