Mleta mada pole kwa yaliyokukuta, lakini kwa maoni yangu tatizo si huyo unayemwita 'rafiki' yako, tatizo ni WEWE, tatizo ni matarajio yako na tafsiri yako ya 'urafiki' na pia hutaki kukubali uhalisia. Tunapowaruhusu watu waingie kwenye maisha yetu kama 'marafiki' tunapaswa urafiki uwe naturally, na wala tusiwe na MATARAJIO yoyote ya kuchuma na kunufaika kutoka kwao. Wewe umeletwa duniani kama wewe peke yako, hivyo ishi maisha yako, pambana kivyako, si jambo baya kuwa na 'rafiki', lakini isiwe nongwa kwamba 'rafiki' lazima akusaidie. Huyo sio mzazi wako na wala si mfadhili wako, ni 'rafiki' tu, yeye ana maisha yake na wewe una maisha yako kwanini iwe nongwa na iwe wajibu wake akusaidie?. Ikitokea amekusaidia, shukuru Mungu lakini tambua SI LAZIMA NA SI WAJIBU WAKE.
Nadhani watu wamepigika kimaisha wanakata tamaa hasa wanapoona mwingine anatoboa wanadhani na wao wametoboa, hapana! mwache abaki kuwa rafiki yako, ila haimaanishi akufadhili au akuondolee changamoto zako za maisha. Kila mtu anakuja duniani ana karama zake, pambana na hali yako.
Tuwe wakweli
Kuna pengo kubwa sana la uzoefu na uelewa kati ya mtu aliyetoboa kimaisha na asiyetoboa, yaani wanatazama mambo tofauti sana, wanafikiri tofauti sana, wana focus tofauti - huwezi kulijua hili hadi utoke chini hujatoboa na kisha utoboe, utaiona tofauti kubwa sana kati yako wewe uliyetoboa na 'rafiki' yako/zako asiyetoboa au wengine uliowaacha hawajatoboa.
Iko hivi, wakati wewe usiyetoboa kila wakati unalalamika, unalaumu, unawaza utakula nini leo, utapataje kodi ya nyumba, utapataje nauli, utapataje simu au pamba kali wakati bado unahangaika na maisha (Survival), unawaza nani atokee 'akuokoe' kimaisha, unamtazama 'rafiki' yako kama mkombozi wa maisha yako, yeye 'rafiki' yako kwanza si mtu kulalamika au kulaumu sana, hawazii ada, hawazii atakula bata wapi, hawazii kodi, anawaza namna gani anaweza kujenga mahusiano na kuboresha mtandao zaidi wa fursa, kupanua wigo wake wa mafanikio aidha ya kazi, biashara, ujasiriamali n,k. yeye anawaza fursa za maendeleo na maeneo gani atawekeza. Wewe unawaza ku survive wakati yeye amevuka survival stage na ametoka maisha ya mahangaiko, anayaishi maisha anavyotaka na anavyojiskia. Hata locations zenu na ku hang na washikaji zinakuwa tofauti kwasababu yeye hawazii bei au gharama za chakula au kinywaji, mavazi nk wakati wewe inabidi ujiulize maswali mengi kabla kununua chakula au kinywaji fulani.
Atamani akae na wewe 'rafiki yake' usiyetoboa, muwe na mazungumzo ya kawaida na mbadilishane mawazo, matokeo yake ni kwamba kila mkikutana hata ajenda za mazungumzo yenu ziko tofauti, wewe ni kulalamika na tozo, mara bei ya mafuta, nk, na mwisho wa siku unajua nani atalipa bili ya vyakula?, vinywaji, nani atatoa lifti au atampa nauli mwenzake? NI DHAHIRI KWAMBA SI WEWE. Atavumilia mara ya kwanza, ya pili lakini akishagundua kwamba kila mtoko wewe ni kitonga, na bado unamwambia ukisikia 'shughuli yoyote' naomba uniunganishe, atakuambia poa 'nikisikia nitakuunganisha', lakini hatakuwa na hamu ya kukaa na wewe. Anahitaji kukaa na watu ambao watam challenge, kibiashara, kifursa na maendeleo kwa ujumla. Anahitaji kukaa na watu ambao inapokuja bili ya vinywaji na chakula wanaigombania kuilipia, 'acha nilipe mimi, wewe utalipa siku nyingine', lakini kila akikaa na wewe, anachosikia si mazungumzo ya maendeleo bali malalamiko, kulaumu watu wengine, kuomba hovyo hovyo, nk, anajikuta YEYE NDIYE FURSA.
Acheni kulialia, pambaneni kutafuta maisha yenu, si tatizo kuwa na marafiki lakini wachukulie kama 'rafiki tu' na sio mfadhili wako au fursa kwako.