Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

YOU NAILED IT!
Kwako na wengine walio katika situation kama yako. Waswahili walisema ''kua uyaone''. Mimi nina experince ya maisha hivyo hili unaoelezea kwangu siyo jambo geni. Nikuambie kitu kimoja: asilimia 95 ya watu unaoita ni marafiki wako siyo marafiki wa kweli na watafanya kama unavyolalamika hapa. Trust me. Ni hivi: wanasaikolojia wanasema mtu anapokuwa na shida fulani, akakutana na mwingine mwenye shida kama yake au kuzidi, hujisikia nafuu japo shida yake iko pale pale. Haya ni maumbile na mkiwa na shida zinazofanana mtajitahidi sana kuwa pamoja. Lakini mara mmoja wenu anapofanikiwa kuondoa ile shida, haoni tena umuhimu wa kuwa karibu kwa sababu ''humliwazi'' tena, sana sana unamkera tu.
 
Hii yangu sio ya kimafanikio ila iliniuma sana.
Mwaka fulani tulimtembelea ndugu yetu, mimi nikiwa na ndugu zangu wengine.
Baada ya mambo mengi kufanyika ikatokea mimi niko nje ila wale ndugu zangu wapo ndani, bc nikaona na mimi niingie ndani ili niwe pamoja na wale ndugu zangu. Ile nmefika ndani tuu wale ndugu zangu wakatoka nje wote na kuniacha pale ndani pekee yangu, aisee niliumia mno mana ni kama vile wananitenga.
 
Kama Nina marafiki basi wako wawili tu.

Huwa napenda cycle yangu iwe ndogo.

Japo kokote napokwenda huwa natengeneza marafiki wapya tena loyal kweli.

Ila Sina mambo ya kumkumbatia au kung'ang'ania mtu.

Falsafa yangu ni kama ya mzee wa chalinze kwa mbele kushoto. Yaani "watumie fanikisha ajenda Yako Kisha wabwage" tafuta wengine.

Jamaa yule amefanikiwa sana kwenye falsafa kwa marafiki zake imemfanga awe godfather kule kusadikika.

Na Mimi muumini wa hii falsafa.

Binadamu hawaaminiki bana Anza kujijali mwenyewe

Tafuta kazi au shughuli na wewe utusue pakubwa halafu unapotea mazima hujazaliwa nae.
 
Hii yangu sio ya kimafanikio ila iliniuma sana.
Mwaka fulani tulimtembelea ndugu yetu, mimi nikiwa na ndugu zangu wengine.
Baada ya mambo mengi kufanyika ikatokea mimi niko nje ila wale ndugu zangu wapo ndani, bc nikaona na mimi niingie ndani ili niwe pamoja na wale ndugu zangu. Ile nmefika ndani tuu wale ndugu zangu wakatoka nje wote na kuniacha pale ndani pekee yangu, aisee niliumia mno mana ni kama vile wananitenga.
Dahhhh inauma sana iyo chakujifunza katika maisha ni kujua value yako.. ukishalijua ilo utoteseka kweny hii dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Nina marafiki basi wako wawili tu.

Huwa napenda cycle yangu iwe ndogo.

Japo kokote napokwenda huwa natengeneza marafiki wapya tena loyal kweli.

Ila Sina mambo ya kumkumbatia au kung'ang'ania mtu.

Falsafa yangu ni kama ya mzee wa chalinze kwa mbele kushoto. Yaani "watumie fanikisha ajenda Yako Kisha wabwage" tafuta wengine.

Jamaa yule amefanikiwa sana kwenye falsafa kwa marafiki zake imemfanga awe godfather kule kusadikika.

Na Mimi muumini wa hii falsafa.

Binadamu hawaaminiki bana Anza kujijali mwenyewe

Tafuta kazi au shughuli na wewe utusue pakubwa halafu unapotea mazima hujazaliwa nae.
Nmejifunza kitu[emoji120][emoji120][emoji120]

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
ila umelalamika ktk huu uzi kama pisi iliyoachwa na jamaa aliyotoka nae mbali kimaisha... Mwanaume unamliliaje mwanaume mwenzako? Hayo ndio maisha sasa fanya yako achana nae, what's urafik? what's kutoka nae mbali? Baba ako huyo...? All in all INTROVERT hatuko hivyo, grown up man, sikuzote mtu anapofanikiwa usitegemee ata behave kawaida kwa mtu au watu aliowazid kimaisha, hata ajitahid vipi end of the day uliyechini yake utaona kama anakukataa kiaina... Be a man, Be a gentleman
 
Kuna jamaa yangu nilimsaidia sana baada ya kupata mpunga wangu baada ya kuwekeza sehemu. Jamaa nilimtoa mpunga wa kutosha na kila baada ya muda alirudi tena nikampa bila kinyongo.

Haikuishia hapo aliniletea hadi jamaa zake ambao mimi sikuwa na ukaribu nao, yeye akawadhamini nikawaazima pesa.

Jamaa nilimpa uhuru urudishe muda wowote hata kwa nusunusu ila wale jamaa zake nilikomaa awaambie waniturudishie kwa wakati.

Kama ujuavyo mambo ya pesa, kuna wakati nilipatwa na shida mpunga ukakata kabisa wakati huo jamaa alikuwa amevuta mkopo bank.

Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimekwama ada ya mtoto wangu alikuwa std ii ameambiwa asipande school bus bila pay slip na walikuwa karibu kupiga paper.

Nikampigia mshkaji kumuomba laki4 tu kwa ahadi ya kurudisha mwisho wa mwezi, jamaa alinijibu hivi:
"Aiseee hii hela siwezi kuitoa kabisa, nimeamua yote niipeleke kwenye ujenzi"

Niliishiwa nguvu, hatakama ni ya ujenzi utaweza kuitumia yote kwa siku moja? Lakini nilijikaza kiume na kujiona fala kwamba hela yangu ndo ilikuwa ya vikoba ila yake ya ujenzi 🤣
 
Kwa kawaida rafiki yako mlieshibana kitambo ikatokea ametoboa kimaisha alafu akagundua ya kwamba wewe maisha yako ni ya kuunga unga atakufungia vioo tuu iko hivyo ndo maisha ya Duniani hata connection hatakupa atakuacha ukafilie mbali akisikia umekata Moto ndo ataibuka na mbwembwe tele!
 
Nimesema alikuwa na wapenz wawili wa kwanza siyo mwongeaji na wa pili muongeaji....kutokana na uongeaji na pesa pia wa pili akamzidi kete wa kwanza Ivo akafanikiwa kumtoa bikra Jay,siku ya siku ikafika wa kwanza kakaza anataka game akapewa na akakuta alichoambiwa anacho Jay hakipo tena....Ivo Mshikaji akakasirika ikawa kama amesusa Fulani....Jay hakupata pressure sana coz wa pili ndo anaemweka mjini.....mwisho wa siku akapata mimba akiwa mwaka wa 3....mimba akaniambia ni ya mpenz wa kwanza(asiye na Hela na siyo mwongeaji) na hata Ivo huyu mwenyehela alipoambiwa Nina mimba akakimbia(japo mimba ni kweli haikuwa yake maana yule aliyekuta bikra imetolewa mbali na kususa mzigo but Kuna time nyege zikimjaa alikuwa anakula mzigo kimtindo afu ndo tuhuma za ujauzito zikamwangukia)...
Mshikaji asiyenazo alikuwa Hana shida akakubali....ila changamoto ikawa namna ya kumtunza Binti na mimba yake(mwanzoni alikuwa hadaiwi matumizi kwa kuwa alikuwa haombwi,Jay si alikuwa anapewa na yule mwingine)....so majukumu yakamwelemea yule kaka,Ivo Jay Kwa kuwa alizoea kutunzwa vyema akatafuta mchepuko mwingine hapohapo chuo,huo mchepuko ukawa unahudumia ila ndo ukawa hautaki Jay awe na mpenz mwingine....
Sasa utamfukuzaje huyo uliyemkuta ...ndo jamaa akaamua kuitumia mbinu ambayo alimficha Jay....Kila wakikutana kusex,jamaa alikuwa anapenda wajirekodi na Jay pasipo kufikiri akawa anakubali....mwisho wa siku yule jamaa akamtumia pictures na video yule Shem(mwenye Ile mimba) .....Shem akamtumia watu wa Karibu na Jay Ili akimkataa Jay kuwe na uthibitisho.....Nadhan hicho ndicho kilichomkimbiza Jay maishani mwangu....Kwa Ile aibu hakutaka kuniona Tena.Japo nilisikia alidisco,akafanya Tena mitihani akafaulu na sasa ni mwalimu songea 😥🙏
Sisi hayo yalitukuta mengi mengi sana, na tuliyasolve kibingw. Maana best kwao mashallah. Nakumbuka tulipomaliza form 6 aliniambia unajua naenda USA kusoma na ADA itatoka huko bongo sasa naenda kuosha vyombo mpk uje kule maana mimi na wewe tukiwa pamoja tutafanya makubwa.Duuuh nakumbuka wkt baada ya wk km mbili dingi akaanza kuumwa.
 
Sisi hayo yalitukuta mengi mengi sana, na tuliyasolve kibingw. Maana best kwao mashallah. Nakumbuka tulipomaliza form 6 aliniambia unajua naenda USA kusoma na ADA itatoka huko bongo sasa naenda kuosha vyombo mpk uje kule maana mimi na wewe tukiwa pamoja tutafanya makubwa.Duuuh nakumbuka wkt baada ya wk km mbili dingi akaanza kuumwa.
Endelea wangu,naendelea kusoma
 
Kifupi mswahili Ni mbwa.
Msaidie Ila usije ukategemea msaada kutoka kwake. Hata salaam sahau.
Ndugu yako ni mke/mume wako na watoto wako tu. Sahau kitu inaitwa dada au Kaka.
Take it from me and thank me later.
Duu hata na wewe Bado unajidanganya.
 
Mleta mada pole kwa yaliyokukuta, lakini kwa maoni yangu tatizo si huyo unayemwita 'rafiki' yako, tatizo ni WEWE, tatizo ni matarajio yako na tafsiri yako ya 'urafiki' na pia hutaki kukubali uhalisia. Tunapowaruhusu watu waingie kwenye maisha yetu kama 'marafiki' tunapaswa urafiki uwe naturally, na wala tusiwe na MATARAJIO yoyote ya kuchuma na kunufaika kutoka kwao. Wewe umeletwa duniani kama wewe peke yako, hivyo ishi maisha yako, pambana kivyako, si jambo baya kuwa na 'rafiki', lakini isiwe nongwa kwamba 'rafiki' lazima akusaidie. Huyo sio mzazi wako na wala si mfadhili wako, ni 'rafiki' tu, yeye ana maisha yake na wewe una maisha yako kwanini iwe nongwa na iwe wajibu wake akusaidie?. Ikitokea amekusaidia, shukuru Mungu lakini tambua SI LAZIMA NA SI WAJIBU WAKE.

Nadhani watu wamepigika kimaisha wanakata tamaa hasa wanapoona mwingine anatoboa wanadhani na wao wametoboa, hapana! mwache abaki kuwa rafiki yako, ila haimaanishi akufadhili au akuondolee changamoto zako za maisha. Kila mtu anakuja duniani ana karama zake, pambana na hali yako.

Tuwe wakweli
Kuna pengo kubwa sana la uzoefu na uelewa kati ya mtu aliyetoboa kimaisha na asiyetoboa, yaani wanatazama mambo tofauti sana, wanafikiri tofauti sana, wana focus tofauti - huwezi kulijua hili hadi utoke chini hujatoboa na kisha utoboe, utaiona tofauti kubwa sana kati yako wewe uliyetoboa na 'rafiki' yako/zako asiyetoboa au wengine uliowaacha hawajatoboa.

Iko hivi, wakati wewe usiyetoboa kila wakati unalalamika, unalaumu, unawaza utakula nini leo, utapataje kodi ya nyumba, utapataje nauli, utapataje simu au pamba kali wakati bado unahangaika na maisha (Survival), unawaza nani atokee 'akuokoe' kimaisha, unamtazama 'rafiki' yako kama mkombozi wa maisha yako, yeye 'rafiki' yako kwanza si mtu kulalamika au kulaumu sana, hawazii ada, hawazii atakula bata wapi, hawazii kodi, anawaza namna gani anaweza kujenga mahusiano na kuboresha mtandao zaidi wa fursa, kupanua wigo wake wa mafanikio aidha ya kazi, biashara, ujasiriamali n,k. yeye anawaza fursa za maendeleo na maeneo gani atawekeza. Wewe unawaza ku survive wakati yeye amevuka survival stage na ametoka maisha ya mahangaiko, anayaishi maisha anavyotaka na anavyojiskia. Hata locations zenu na ku hang na washikaji zinakuwa tofauti kwasababu yeye hawazii bei au gharama za chakula au kinywaji, mavazi nk wakati wewe inabidi ujiulize maswali mengi kabla kununua chakula au kinywaji fulani.

Atamani akae na wewe 'rafiki yake' usiyetoboa, muwe na mazungumzo ya kawaida na mbadilishane mawazo, matokeo yake ni kwamba kila mkikutana hata ajenda za mazungumzo yenu ziko tofauti, wewe ni kulalamika na tozo, mara bei ya mafuta, nk, na mwisho wa siku unajua nani atalipa bili ya vyakula?, vinywaji, nani atatoa lifti au atampa nauli mwenzake? NI DHAHIRI KWAMBA SI WEWE. Atavumilia mara ya kwanza, ya pili lakini akishagundua kwamba kila mtoko wewe ni kitonga, na bado unamwambia ukisikia 'shughuli yoyote' naomba uniunganishe, atakuambia poa 'nikisikia nitakuunganisha', lakini hatakuwa na hamu ya kukaa na wewe. Anahitaji kukaa na watu ambao watam challenge, kibiashara, kifursa na maendeleo kwa ujumla. Anahitaji kukaa na watu ambao inapokuja bili ya vinywaji na chakula wanaigombania kuilipia, 'acha nilipe mimi, wewe utalipa siku nyingine', lakini kila akikaa na wewe, anachosikia si mazungumzo ya maendeleo bali malalamiko, kulaumu watu wengine, kuomba hovyo hovyo, nk, anajikuta YEYE NDIYE FURSA.

Acheni kulialia, pambaneni kutafuta maisha yenu, si tatizo kuwa na marafiki lakini wachukulie kama 'rafiki tu' na sio mfadhili wako au fursa kwako.
 
Back
Top Bottom