Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Nina kisa kama chako ila kwangu tuliponaliza Chuo getho(vingunguti) tukaendelea kuishi pamoja magetoni)

Kumbuka sio Chuo kikuu bali ni vyuo vya Kati. Msaada home ukakata,tukatafuta ajira. Mwenzangu akawahi kupata. Akasapoti Kodi katika kipindi chote.

Siku Moja nilikuta amehama amechukua godoro na kitanda nilikuta mabox(sikumbuki kama palikuwa na chandarua) lkn Ngosha mie nililala chini, nakumbuka nilipoingia na dem wangu alisikitika Sana. Kosa ambalo nahisi alihama na hakuwa anapenda hiyo kitu ni Mimi kula tunda mule ndani. Is okay sikutaka kuendelea kula mule tena.

Akahamia nisipopajua lkn baadae nikajua ni (ilala).

Nina marafiki wachache pia na nahisi hata yeye sio rafiki ni Ile kuishi pamoja, as time went on nikapata kazi 'alhamdullillah,' nikatafuta room mbili na choo(lkn huku najua Dem ni MTU wa tamaa japo niliplan tuishi tufunge ndoa Nikaishia pale. Yule Dem Wangu naye akanimwaga silently Kwa sabb nahisi naye aliona Basha mie Sina mbele Wala kazi(sikumwambia nimepata kazi) ilikuwa hivi kila nilivyopita naye sehemu na tukikaribia kufika shell Moja ya mafuta Dem.."ananambia hapa Pana MTU sipendi atuone" mie napita kule yeye huko. Tunakutana mbeleee huko. Nikahoji.....

Mimi.." kwani ni nani..."
Dem..'.....(hasemi anazungazuga)...

Sisi introverts Huwa tunafikiria na kutatua issues ndani Kwa ndani...

Nikajinyamazia kinyaa.... Baadae nikagunfua kumbe pale Kuna jamaa ana 'wazifa'.

Mungu si athuman nikapaa majuu... Basi bana si simu hizo kutoka Kwa wasaliti.
Ule msemo kuwa kiswahili ni kibantu ndio huu ..uyu jamaa ni mbantu kabisa siyo kwa kiswahili iki[emoji28][emoji28][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna msela ambaye alifukuzwa shule ya msingi akiwa darasa la 4, me nikamchukua nikampeleka kwenye shule ambayo nilikuwa nasomea mimi kwakuwa nilikuwa monitor wa darasa na majina nilikuwa naita mimi basi nikamuandikisaha akasoma kama miezi 3 hivi ndo walimu wanakuja shituka heee, huyu mbona kwenye vitabu vyetu hatumfahamu basi kubanwa nikatajwa alimanusura nifukuzwe shule ila tu mkuu wa shule alikuwa ananikuli sana toka ni toke nikachwapwa fimbo za kuzugia nikaendelea na masomo,

Msela tulipo maliza sekondari akapewa piki piki mpya na dingi yake kama mnavyojuwa miaka hiyo boda boda zilikuwa zinalipa akaanza kunionyeshea vidharau na kusema haweziongea na mimi wakati tulikuwa mabest balaa,
Tangu siku hiyo me sina rafiki maalum,

Kisa cha pili,
Jfm, nilipata rafiki mdada furani hivi anaitwa JANETH, nilikuwa namkubali sana tukawa tunawasiliana whatsapp na sms za kawaida, inshort nilifurahiya kampani yake ila alivyo niblock bila sababu iliniuma sana,
Janeth popote ulipo juwa nakukubali mpaka leo, maana ulikuwa na ushauri wa maendeleo.
najuwa utasoma uzi huu pia utaona comment yangu.
Muwe mnaelewa, acheni shobo na watt wa kike kwa kisingizio cha URAFIKI WA KUSHAURIANA. ACHA U-K. UMA!
 
Mimi aliniambia sasa hivi siko level yake. Hata kama tulikuwa marafiki huko nyuma siyo sababu ya kuwa close naye. ( Ni baada ya kupata kazi serikalini kitengo kizuri)

Nikapiga moyo konde nikaedelea na maisha yangu.

(Mungu si mwanadamu na mimi akanionyesha njia na kunipunguzia magumu ya maisha. Kiasi fulani maisha yakabadilika)

Kuna siku akapata shida nyumbani kwao bila hiyana nikaisolve kwa moyo mmoja ili nimfichie aibu yake.Nilijitoa kweli kweli mpaka alibaki amepigwa na butwaa, hakutegemea kabisa.

Nilivyomaliza kuisolve nikaweka mipaka. Amejaribu kuwasiliana na mimi lakini sina muda naye na hasa baada ya kugundua kumbe hakuwa rafiki mwema kwangu, aliniharibia maisha kwa kiwango kikubwa.

Nilishampiga bloku ya nguvu. Kuweni makini na hawa marafiki.Rafiki wa kweli ni yule anayepata kazi na pesa still habadiliki yuko vile vile siku zote, ila hawa malimbukeni wa maisha ni pasua kichwa.
 
Kwenye maisha naona usijipange sana kwamba watu watakuwa unavyowadhani.....jipange kwa yote ili wakibadilika usipate nafasi ya kulaumu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Iko hivi, mimi na wewe ni marafiki wa kufa na kuzikana, shida yako shida yangu.

Wote hatuna nauli ya kutufikisha Posta kutokea maeneo tunayoishi, kwasababu tupo kwenye harakati na wapambanaji tunaamua kutembea kwa miguu kuanzia maeneo tunayoishi hadi Posta.

Tunapanga mipango mingi ya kimaendeleo iwapo tukibahatika kujikwamua kwenye hali hii ya ukata tuliyokuwa nayo.

Ghafla mwenzangu neema ya aina yoyote ile inakuangukia, na unajua fika mimi na wewe hali zetu zilivyo na tumetoka mbali. Mara baada ya neema kukuangukia unanitenga. Hata nikikuulizia chanali wewe hutaki kutoa chanali na inafikia wakati unanipotezea mazima
 
Kuwa humble ni tofauti na kuwa na marafiki viazi. Elewa hoja. Kama you can't even comprehend this basi wewe ni prime example ya marafiki wa kuwabwaga ASAP.

Maisha hayanichapi abadan. Kupanga ni kuchagua. Hamna bahati maishani yote ni mipango, nidhamu na hardwork.

New level. New devil.
Motivational speaker unaongea sana......

Binafsi nishapoteza watu wengi wa muhimu so hakuna kiumbe duniani ambaye namhofia akienda mbali na mimi nitakusa raha.

Ishu hapa ni maskini kama ww ukipata mfereji kidgo unajifanya unawaacha uliosota nao na wengine wamekusaidia kipindi huna mbele wala nyuma..Hafu badae mambo yako yawe onpoint useme ooh sijui hawana cha kushare sijui wana vizinga hapo ni kwamba ww ndo umekuwa msaliti na limbukeni ila wapo watu huo ulimbuken kama wako hawana wanapata mifereji na wanakumbuka walikotoka.
 
Iko hivi, mimi na wewe ni marafiki wa kufa na kuzikana, shida yako shida yangu.

Wote hatuna nauli ya kutufikisha Posta kutokea maeneo tunayoishi, kwasababu tupo kwenye harakati na wapambanaji tunaamua kutembea kwa miguu kuanzia maeneo tunayoishi hadi Posta.

Tunapanga mipango mingi ya kimaendeleo iwapo tukibahatika kujikwamua kwenye hali hii ya ukata tuliyokuwa nayo.

Ghafla mwenzangu neema ya aina yoyote ile inakuangukia, na unajua fika mimi na wewe hali zetu zilivyo na tumetoka mbali. Mara baada ya neema kukuangukia unanitenga. Hata nikikuulizia chanali wewe hutaki kutoa chanali na inafikia wakati unanipotezea mazima
Bufa usipoelewa na hapa basi uende milembe.
 
Kuna msela ambaye alifukuzwa shule ya msingi akiwa darasa la 4, me nikamchukua nikampeleka kwenye shule ambayo nilikuwa nasomea mimi kwakuwa nilikuwa monitor wa darasa na majina nilikuwa naita mimi basi nikamuandikisaha akasoma kama miezi 3 hivi ndo walimu wanakuja shituka heee, huyu mbona kwenye vitabu vyetu hatumfahamu basi kubanwa nikatajwa alimanusura nifukuzwe shule ila tu mkuu wa shule alikuwa ananikuli sana toka ni toke nikachwapwa fimbo za kuzugia nikaendelea na masomo,

Msela tulipo maliza sekondari akapewa piki piki mpya na dingi yake kama mnavyojuwa miaka hiyo boda boda zilikuwa zinalipa akaanza kunionyeshea vidharau na kusema haweziongea na mimi wakati tulikuwa mabest balaa,
Tangu siku hiyo me sina rafiki maalum,

Kisa cha pili,
Jfm, nilipata rafiki mdada furani hivi anaitwa JANETH, nilikuwa namkubali sana tukawa tunawasiliana whatsapp na sms za kawaida, inshort nilifurahiya kampani yake ila alivyo niblock bila sababu iliniuma sana,
Janeth popote ulipo juwa nakukubali mpaka leo, maana ulikuwa na ushauri wa maendeleo.
najuwa utasoma uzi huu pia utaona comment yangu.
Kama hukumtongoza huyo Janeth basi elewa alitarajia kitu kama hicho kutoka kwako, alipokikosa tu na kupata mwingine aliyewahi akakuvua vyeo vyote
 
me sikuwahi kumtongoza ila tu nilipenda mawazo yake ya maendeleo, na nikili kuwa alinitoa sehemu moja kwenda level nyingine, nilimchukulia kama rafiki tu na nilimpenda kama mshikaji
 
Motivational speaker unaongea sana......

Binafsi nishapoteza watu wengi wa muhimu so hakuna kiumbe duniani ambaye namhofia akienda mbali na mimi nitakusa raha.

Ishu hapa ni maskini kama ww ukipata mfereji kidgo unajifanya unawaacha uliosota nao na wengine wamekusaidia kipindi huna mbele wala nyuma..Hafu badae mambo yako yawe onpoint useme ooh sijui hawana cha kushare sijui wana vizinga hapo ni kwamba ww ndo umekuwa msaliti na limbukeni ila wapo watu huo ulimbuken kama wako hawana wanapata mifereji na wanakumbuka walikotoka.

To each their own.
 
Alikuwa na hisia kwako, ukachelewa kujua hilo
Daaah, me sikulitambua hilo na hata angefunguka tu,
Nilimuona kama rafiki mwema kwangu na alinishauri mambo kibao ya maana hata wakati niliokata tamaa alinifanya niinuke tena
 
Iko hivi, mimi na wewe ni marafiki wa kufa na kuzikana, shida yako shida yangu.

Wote hatuna nauli ya kutufikisha Posta kutokea maeneo tunayoishi, kwasababu tupo kwenye harakati na wapambanaji tunaamua kutembea kwa miguu kuanzia maeneo tunayoishi hadi Posta.

Tunapanga mipango mingi ya kimaendeleo iwapo tukibahatika kujikwamua kwenye hali hii ya ukata tuliyokuwa nayo.

Ghafla mwenzangu neema ya aina yoyote ile inakuangukia, na unajua fika mimi na wewe hali zetu zilivyo na tumetoka mbali. Mara baada ya neema kukuangukia unanitenga. Hata nikikuulizia chanali wewe hutaki kutoa chanali na inafikia wakati unanipotezea mazima
Mkuu umeongea kitu Cha msingi sana, watu mmesota wote, itokee mmoja aotee eti ghafla tu iwe hakuna kitu mtaongea, how come..
 
Mi nilimchukua mshkaj flan ambae tulimaliza wote shule,akaleta shida kwao wakamfukuza,akaja home nikaa nae sana kakaangu mkubwa akamtafutia kibarua,yaani kwa ufupi mwamba tulimgeuza kama ndugu kabisa,Mungu si Athumani katika mishe zake akatoka sijui alichofanya hadi akafanikiwa anajua yeye,kimya kimya akajenga mbezi hii ya kimara,mara kajenga chanika kimyakimya,ghafla akasema anaenda kumsalimia mamaake! Ndio kimoja hakurudi,hilo halikuwa tatizo ila shida ilikuwa moja tu alisepa na mke wa bro(aliemtafutia kibarua)
 
Back
Top Bottom