Ulishawahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au na mtu mwenye ndoa?

Ulishawahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au na mtu mwenye ndoa?

Umewahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au na mtu mwenye ndoa?

  • NDIO

    Votes: 48 60.0%
  • HAPANA

    Votes: 33 41.3%

  • Total voters
    80
...haiwezekani/Inawezekana kuishi bila kumdanganya Mkeo/Mumeo/Mchumba wako kwa 100%?

mfano;
  • kudanganya unapochelewa kurudi nyumbani?
  • kudanganya mapato na matumizi yako?
  • kudanganya kuridhishwa kimapenzi japo unatoka kapa?
  • kudanganya hakuna alilokuudhi ili yaishe?
  • unexpected mobile calls, ukajidai humsikii mpigaji?
  • kudanganya mambo unayojua yatamuudhi ukimwambia ukweli?
  • kumdanganya mahusiano yako na marafiki asiowapenda?
  • nk,...nk...?
Inawezekana au haiwezekani? kwanini? piga kura (Optional) au tetea hoja yako.

Hata kanisani huwa tunadanganya mapato... :amen:
 
...kudanganywa ni kudanganywa tu.
Hakuna kudanganywa vizuri, au kidogo.
Kudanganywa kunauma. Huenda umedanganywa kwakuwa huheshimiwi, au huaminiwi, au basi tu hustahiki kuambiwa ukweli. Utapimaje kiwango cha kudanganywa mfano;
  • hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo alishazaa mtoto wa nje, au...
  • hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo amepandishwa cheo.
 
kweli huo ni uongo mtakatifu, pia mie uongo umenisaidia bwana mana natakiwa nitoe majibu pacpo kituo, sasa kuweka mambo sawa tuweze maliza cku vizuri ni bora ni mix....50-50

...Ahahahaha... Nyamayao umeniacha hoi kwa kicheko, duuuh...una mix 50-50? si mchezo!
Maisha ya ndoa "UAMINIFU" muhimu, lakini huu ni uthibitisho hata UAMINIFU kwenye ndoa una mipaka yake bana... LOL

Yaani kila nikiisoma hii mada, moyoni najiskia mkosaji.
binafsi huwa nadanganya sana mara nyingi lengo huwa ni kunusuru uhusiano wangu.
lakini huwa sipendi iwe hivyo.
Inaniuma sana.

...kwakweli, heri yako unayeungulia moyoni kuliko yule anayejionea kuongopa ni sehemu ya maisha, LOL!
 
hahahahaha!
halafu maaskofu mmezidi kwa wake za watu:A S tongue:

he he heee.... we endelea na weldi kapu yako...Wao ndio wamezidi na sisi... huduma za nyumba kwa nyumba...
 
Kwa kusema ukweli ni BAHATI na NADRA sana kuwepo mtu japo awe moja ambaye hajawahi kufanya udanganyifu japo iwe ni mara moja tu kwenye ndoa. Ni vizuri na inatosha tu watu wakijua kwamba udanganyifu kwenye ndoa ni dhambi kwa mwenzi wako na kubwa zaidi mbele za MWENYEZI MUNGU
 
...kudanganywa ni kudanganywa tu.
Hakuna kudanganywa vizuri, au kidogo.

Kudanganywa kunauma. Huenda umedanganywa kwakuwa huheshimiwi, au huaminiwi, au basi tu hustahiki kuambiwa ukweli. Utapimaje kiwango cha kudanganywa mfano;
  • hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo alishazaa mtoto wa nje, au...
  • hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo amepandishwa cheo.
huo uongo ni wa ngumi jamani, muwe mnadanganya v2 ambavyo havina madhara kwa afya, hapana uongo mkubwa huo!
 
he he heee.... we endelea na weldi kapu yako...Wao ndio wamezidi na sisi... huduma za nyumba kwa nyumba...

lol! askofu umenivunja mbavu sana...kumbe ni wao? hahahahahahahahah mimi pia nilidhani ni nyinyi!
 
...Ahahahaha... Nyamayao umeniacha hoi kwa kicheko, duuuh...una mix 50-50? si mchezo!
Maisha ya ndoa "UAMINIFU" muhimu, lakini huu ni uthibitisho hata UAMINIFU kwenye ndoa una mipaka yake bana... LOL
Mbu wakati mwingine kama uaminifu ni kusema kweli ambayo itakuletea shida bac bora huo uaminifu utoweke kwa dk chache kunusuru kasheshe.
 
lol! askofu umenivunja mbavu sana...kumbe ni wao? hahahahahahahahah mimi pia nilidhani ni nyinyi!

BAK... nani anamfuata mwenzake hapo... Mtumishi au Muumini? Sisi tunaitwa kutoa huduma (but remember we are all human beings... majaribu yakizidi tunamchapa shetani)
 
BAK... nani anamfuata mwenzake hapo... Mtumishi au Muumini? Sisi tunaitwa kutoa huduma (but remember we are all human beings... majaribu yakizidi tunamchapa shetani)

hahahahahahahah eh! Majaribu yakizidi mnachapa shetani siyo!? LOL! Haya Askofu kila la hei katika kumchapa shetani..... sijui huwa mnatumia fimbo ipi?
 
...kudanganywa ni kudanganywa tu.
Hakuna kudanganywa vizuri, au kidogo.
Kudanganywa kunauma. Huenda umedanganywa kwakuwa huheshimiwi, au huaminiwi, au basi tu hustahiki kuambiwa ukweli. Utapimaje kiwango cha kudanganywa mfano;

  • hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo alishazaa mtoto wa nje, au...
  • hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo amepandishwa cheo.

Hapo kwenye blue, kama ukisema uongo basi uhakikishe mwenzio hawezi kujua. Hiyo iko nje ya vipimo vyangu vya mambo ambayo yamebarikiwa na Bwana; naye anaweza kukupa shavu! Kama ulishazaa kabla ya ndoa ni vizuri na muhimu sana kumweleza mume/mke wako. Kwani ikijulikana baadaye itaiweka ndoa mashakani (inaweza kusababisha mtu kupata yellow au red card). Ila kama umezaa ndani ya mahusiano basi hakuna cha uongo hapo, inabidi ufiche hiyo kitu kama unavyoficha figo zako ndani ya mwili. Kwangu hilo ni kosa la red card ya moja kwa moja! Na hilo la kutosema pale unapopanda cheo naona ni upuuzi tu. Hakuna uongo hapo bali unakuwa mpuuzi kutomwambia mwenzio. Kwani ukifukuzwa kazi hutasema pia?
 
...Ohoo, hujawahi sikia wewe?, kuna mijitu ina wivu bana, Mkewe akipandishwa cheo anakuwa mkali na kuhoji ilikuwaje bosi amempendelea yeye hakuwapandisha wengine cheo. Wengine hawataki kabisa kusikia wake zao eti wanakwenda semina za kikazi na mabosi wao... hakieleweki!
 
Kama jitu linatabia kama hizo basi hata likidanganywa makubwa zaidi sitasikitika. Ni kweli kwa baadhi ya wanaume inauma sana mke anapopata nafasi ya kwenda semina au safari nyingine ya kikazi. Lakini kama unamwani (walau kwa kiasi kikubwa i.e kwa 75-99.99% kama mimi) basi utamruhusu tu aende ila kweli roho huwa inauma kidogo. Lakini kama mtu hafurahii mafanikio ya mke wake basi hapo kuna tatizo. Ama yeye pia ni mwizi kwa hiyo anaogopa kuibiwa au anamjua kwamba hana uwezo wa kufikia viwango hivyo anavyopewa na ofisi au boss wake! Kwa ufupi hapo kuna tatizo kubwa zaidi.
 
...Ohoo, hujawahi sikia wewe?, kuna mijitu ina wivu bana, Mkewe akipandishwa cheo anakuwa mkali na kuhoji ilikuwaje bosi amempendelea yeye hakuwapandisha wengine cheo. Wengine hawataki kabisa kusikia wake zao eti wanakwenda semina za kikazi na mabosi wao... hakieleweki!

Ni kweli kabisa kuna mianaume ina wivu wa kupitiliza. Mkewe siku zote hastahili kupata promotion akipata promotion basi katembea na bosi ofisini ndiyo maana kapewa cheo na ikijulikana kapewa cheo basi kasheshe ya hali ya juu inazuka nyumbani...kusafiri kikazi ndiyo usiseme tena....ndiyo maana kuna mianaume mingine hung'ang'ania kuoa darasa la saba ili mke akae nyumbani tu. Hajui kuoa msomi watoto na familia yote inafaidika kwa kuwa na mke msomi na mama msomi. Akishaoa darasa la saba anaona aibu kutoka naye maana atamuibisha mbele ya marafiki zake!!!! Mtu una Phd au Masters kwanini usitafute mke angalau kamaliza A' level? Mhhhh! Mianaume mingine ndivyo ilivyo!

Kama jitu linatabia kama hizo basi hata likidanganywa makubwa zaidi sitasikitika. Ni kweli kwa baadhi ya wanaume inauma sana mke anapopata nafasi ya kwenda semina au safari nyingine ya kikazi...

Ni kweli kabisa kuna mianaume ina wivu wa kupitiliza. Mkewe siku zote hastahili kupata promotion akipata promotion basi katembea na bosi ofisini ndiyo maana kapewa cheo na ikijulikana kapewa cheo basi kasheshe ya hali ya juu inazuka nyumbani...kusafiri kikazi ndiyo usiseme tena....

...hahaha... yaani mlivyounga mkono inaonekana tatizo hili sugu limejikita vilivyo katika jamii. Sasa wivu wa nini mke akipandishwa cheo au akienda kulala semina?... No wonder kinadada (wachache) hutumia visababu vikiwemo "eti", semina ni kwa kina mama tu! ha ha ha...

Mpaka sasa mnaosema INAWEZEKANA mmeuchuna kutetea hoja, ...
Eti nyie kinadada, mnapodanganya mnaumwa kichwa almuradi mume asile chakula cha usiku si urongo ule?!
 
Back
Top Bottom