...haiwezekani/Inawezekana kuishi bila kumdanganya Mkeo/Mumeo/Mchumba wako kwa 100%?
mfano;
Inawezekana au haiwezekani? kwanini? piga kura (Optional) au tetea hoja yako.
- kudanganya unapochelewa kurudi nyumbani?
- kudanganya mapato na matumizi yako?
- kudanganya kuridhishwa kimapenzi japo unatoka kapa?
- kudanganya hakuna alilokuudhi ili yaishe?
- unexpected mobile calls, ukajidai humsikii mpigaji?
- kudanganya mambo unayojua yatamuudhi ukimwambia ukweli?
- kumdanganya mahusiano yako na marafiki asiowapenda?
- nk,...nk...?
hahahahaha!Hata kanisani huwa tunadanganya mapato... :amen:
kweli huo ni uongo mtakatifu, pia mie uongo umenisaidia bwana mana natakiwa nitoe majibu pacpo kituo, sasa kuweka mambo sawa tuweze maliza cku vizuri ni bora ni mix....50-50
Yaani kila nikiisoma hii mada, moyoni najiskia mkosaji.
binafsi huwa nadanganya sana mara nyingi lengo huwa ni kunusuru uhusiano wangu.
lakini huwa sipendi iwe hivyo.
Inaniuma sana.
hahahahaha!
halafu maaskofu mmezidi kwa wake za watu:A S tongue:
Hata wanakondoo wakikaa vibaya huwa mnawadanganya pia:sick:Hata kanisani huwa tunadanganya mapato... :amen:
huo uongo ni wa ngumi jamani, muwe mnadanganya v2 ambavyo havina madhara kwa afya, hapana uongo mkubwa huo!...kudanganywa ni kudanganywa tu.
Hakuna kudanganywa vizuri, au kidogo.
Kudanganywa kunauma. Huenda umedanganywa kwakuwa huheshimiwi, au huaminiwi, au basi tu hustahiki kuambiwa ukweli. Utapimaje kiwango cha kudanganywa mfano;
- hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo alishazaa mtoto wa nje, au...
- hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo amepandishwa cheo.
he he heee.... we endelea na weldi kapu yako...Wao ndio wamezidi na sisi... huduma za nyumba kwa nyumba...
say it again please!hata wanakondoo wa kike wakikaa vibaya huwa mnawadanganya pia:sick:
Mbu wakati mwingine kama uaminifu ni kusema kweli ambayo itakuletea shida bac bora huo uaminifu utoweke kwa dk chache kunusuru kasheshe....Ahahahaha... Nyamayao umeniacha hoi kwa kicheko, duuuh...una mix 50-50? si mchezo!
Maisha ya ndoa "UAMINIFU" muhimu, lakini huu ni uthibitisho hata UAMINIFU kwenye ndoa una mipaka yake bana... LOL
Hata wanakondoo wakikaa vibaya huwa mnawadanganya pia:sick:
lol! askofu umenivunja mbavu sana...kumbe ni wao? hahahahahahahahah mimi pia nilidhani ni nyinyi!
BAK... nani anamfuata mwenzake hapo... Mtumishi au Muumini? Sisi tunaitwa kutoa huduma (but remember we are all human beings... majaribu yakizidi tunamchapa shetani)
...kudanganywa ni kudanganywa tu.
Hakuna kudanganywa vizuri, au kidogo.
Kudanganywa kunauma. Huenda umedanganywa kwakuwa huheshimiwi, au huaminiwi, au basi tu hustahiki kuambiwa ukweli. Utapimaje kiwango cha kudanganywa mfano;
- hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo alishazaa mtoto wa nje, au...
- hukuambiwa ukweli kwamba mkeo/mumeo amepandishwa cheo.
Hapo kwenye blue, kama ukisema uongo basi uhakikishe mwenzio hawezi kujua. Hiyo iko nje ya vipimo vyangu vya mambo ambayo yamebarikiwa na Bwana; naye anaweza kukupa shavu! Kama ulishazaa kabla ya ndoa ni vizuri na muhimu sana kumweleza mume/mke wako. Kwani ikijulikana baadaye itaiweka ndoa mashakani (inaweza kusababisha mtu kupata yellow au red card). Ila kama umezaa ndani ya mahusiano basi hakuna cha uongo hapo, inabidi ufiche hiyo kitu kama unavyoficha figo zako ndani ya mwili. Kwangu hilo ni kosa la red card ya moja kwa moja! Na hilo la kutosema pale unapopanda cheo naona ni upuuzi tu. Hakuna uongo hapo bali unakuwa mpuuzi kutomwambia mwenzio. Kwani ukifukuzwa kazi hutasema pia?
...Ohoo, hujawahi sikia wewe?, kuna mijitu ina wivu bana, Mkewe akipandishwa cheo anakuwa mkali na kuhoji ilikuwaje bosi amempendelea yeye hakuwapandisha wengine cheo. Wengine hawataki kabisa kusikia wake zao eti wanakwenda semina za kikazi na mabosi wao... hakieleweki!
...Ohoo, hujawahi sikia wewe?, kuna mijitu ina wivu bana, Mkewe akipandishwa cheo anakuwa mkali na kuhoji ilikuwaje bosi amempendelea yeye hakuwapandisha wengine cheo. Wengine hawataki kabisa kusikia wake zao eti wanakwenda semina za kikazi na mabosi wao... hakieleweki!
houseboy anajishindia coz uwezo wao wa kufikiri utakuwa unafananandiyo maana kuna mianaume mingine hung'ang'ania kuoa darasa la saba ili mke akae nyumbani tu.
Kama jitu linatabia kama hizo basi hata likidanganywa makubwa zaidi sitasikitika. Ni kweli kwa baadhi ya wanaume inauma sana mke anapopata nafasi ya kwenda semina au safari nyingine ya kikazi...
Ni kweli kabisa kuna mianaume ina wivu wa kupitiliza. Mkewe siku zote hastahili kupata promotion akipata promotion basi katembea na bosi ofisini ndiyo maana kapewa cheo na ikijulikana kapewa cheo basi kasheshe ya hali ya juu inazuka nyumbani...kusafiri kikazi ndiyo usiseme tena....