Ulishawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti mliyeshibana sana?

Ulishawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti mliyeshibana sana?

Hizi mambo ziliwezekana enzi za kombolela tu...

Baada ya kuanza kunjunjana basi ubongo ukaongezewa kitengo maalumu cha kuyakimbia mahusiano mnayoyataja hapa...

Chakorii eti inawezekana kweli tukawa tu marafiki halafu tusichome ramani ya vita? 😊😊
 
Ulichosema hivyo hivyo kilinitokea mimi tofauti yangu na wewe ni

Yule mdada alikuwa bikra hadi form 6 na alisema hatakuja kushiriki tendo mpaka ndoa tukawa tunabishana sana namwambia utakamatika tu

Sasa alikuja kumpata mwanaume ambaye sio tu alimtoa bikra bali alimpa mimba sasa bikra alivyotolewa aliniambia tu nimekomaliwa nimeZidiwa ujanja nimetolewa bikra.

Alivyopata mimba alishindwa kuvumilia akawa ananikwepa kwepa Kiukweli roho iliniuma sana kujua ameshindwa kuwa huru kwa jambo hilo nadhani ni sababu ya kushika dini sana.

Ni marafiki hadi leo mimi nimeoa yeye bado hajaolewa ila ile chemistry imepungua kdg sababu siku niliyogundua ana mimba ilikuwa ina miezi 8 nilimwambia ukweli tu umeni disappoint sana sikutarajia kama wewe kupata mimba ungefanya siri kwangu nilidhani mimi ndo ningekua mapema sana instead nimekuja kuambiwa na watu tu.

Mtoto kamuita jina langu na kwenye matatizo tunapeana tough.Hiyu ndo mtu pekee ambaye kuanzia iq na kila kitu tunaendana hamna kitu nitaongea asinielewe na hamna kitu ataongea nisielewe.

Sijawahi kupata rafiki wa hivyo mpaka leo hata mke wangu hajafikia level z kunielewa kupita huyu mtu

Note:Hatujawahi kuwa na hisia za kimapenzi na huyu mtu
 
I have this Madame aiseee mpka leo hii ni marafiki wakubwa sana

Tulifahamiana kupitia my best friend kipind tuko chuo then tukajikuta mim na huyu Madame tumekuja kuwa marafiki kuliko huyu rafiki angu ambae alikua anafahamiana nae kabla.

Mpka dakika hii amebakia my very good friend na namshirikiksha mambo mengi sana na yeye ananishirikisha yake.
 
Hahaha. Nakuja mkuu [emoji126][emoji126]
Grena, umenikumbusha nilikuwa na rafiki yangu flani alikiwa anapenda kunidekea sana, nami nilijua kumdekeza basi naye alikamatia hapo hapo...nina mmiss balaa
 
Nimeshibana sana na mke wa mtu. Anajua kabisa niko single, ananipigia simu all time akijisikia.

Nimemtania kwamba nitamkula, kajibu 𝐭𝐮𝐭𝐚𝐣𝐚𝐝𝐢𝐥𝐢 𝐡𝐢𝐥𝐨, 𝐚𝐤𝐚𝐜𝐡𝐞𝐤𝐚 kisha akakata simu😅😅
 
Daaa huu uzi umenigusa mmnoooo,
Nilikuwa na rafiki pia, alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu,
Alikuwa na mwanamke ambaye sahizi ni mke wake, nilimpenda yule dada kwaajili ni demu wa rafiki yangu, alipooa nadhani ilikuwa ni ndoa yangu ya kwanza kuchangia hela nyingi.

Alipoolewa tu yule dada jamani, alinigeuzia kibao kikubwa na kusema nambebea mumewe, akawa anampelekesha rafiki yangu vibaya ilikuwa inaniuma sana, lakini niliamua kukaa pembeni nisilete ugomvi wa ndoa ya watu.
Rafiki yangu alikuwa ni kajamaa flani kenye nyota, si kazini wala mtaani lakini gafla aliandamwa na mabalaa mara ajali mara madeni, alipoteza nuru na kila kitu.

Nikimwona roho inaniuma sana kwasababu kapoteza vingi kwa kupelekeshwa na mke..

Rafiki yangu, nakumiss sana natamani nikusaidie hayakuwa matarajio yako lakini pambana tu labda Mungu atakuona na atakusaidia mana umeoa jini...mke hata ndugu hataki!!!
 
Back
Top Bottom