Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Daa mkuu naona tuko umri sawa
Marehemu Donna Summer mpaka last week nilikuwa namsikiliza nikiwa naelekea Manchester
Wimbo wake wa The Woman in me
Asante sana kwa uzi huu wa nyimbo za zamani
Yaani karibu zote ndio favorite songs zangu

Kuna huu mwingine wa Donna ambao pia ulivuma sana wakati huo; nadhani unaujua. Nimesoma kuwa alifariki kwa kansa ya mapafu akiwa na umri wa miaka 63, yaani alikuwa bado kinda tu. Ni premature death iliyoondoka na talent moja kubwa sana.


View: https://www.youtube.com/watch?v=N8EkGUm9q_A
 
Kuna huu mwingine wa Donna ambao pia ulivuma sana wakati huo; nadhani unaujua. Nimesoma kuwa alifariki kwa kansa ya mapafu akiwa na umri wa miaka 63, yaani alikuwa bado kinda tu. Ni premature death iliyoondoka na talent moja kubwa sana.


View: https://www.youtube.com/watch?v=N8EkGUm9q_A

Aisee alikuwa mwimbaji mzuri sana
Kweli alikufa kwa Kansa
She works hard for the money naukumbuka sana
 
Wakuu hivi hili song linaitwaje?

Nililisikia Radio One mtaa wa magoma nika Shazam lakini haikunipa majibu

Mwenye kuujua unaitwaje na umeimbwa na nani?

Kichuguu
 

Attachments

Kuna hadithi ya kuchekesha kidogo kuwahi kutokea Tanzania kuhsu biashara ya kimataifa. Mwaka 1970 Japani iliandaa maonyesho ya biashara na viwanda pale Osaka. Mwaka huo Tanzania ndiyo tulikuwa bado tunajitafuta kwani hatukuwa na bidhaa za viwandani kuonyesa huko. Badala yake tukaepeleka bendi ya polisi iliyokuwa inaongozwa na Inspeka Mayagilo (wakati huo), Bendi ya Morogoro Jazz iliyokuwa inaongozwa na Mbaraka Mwishehe, Mzee Morissi ambaye alikuwa kipofu lakini alikuwa anajua kupiga ngoma kumi bila makosa, pamoja na kikosi cha maonyesho ya sanaa ya ngoma za kienyeji kilichokuwa chini ya idara mpya sana wakati huo ya Sanaa za Maonyesho (Visual Arts) pale chuo Kikuu. Nadhani Profesa Penina Mrama (wakati huo akijulikana kama Penina Mhando) ndio walikuwa waanzilishi wa idara hiyo. Wakapeleka wacheza mizimu na wachezea nyoka kwenye maonyesho ya biashara na viwanda.

Mbaraka aliporudi alitoa kibao kikali sana ambacho kilivuma sana anga la muziki Tanzania hadi mwaka 1972 hivi. Yaani maonyesho ya biashara na Viwanda, sisi tunapelea usanii. Nadhani tuli[aaniwa tangia hapo; burudika kuelewa kibao chetu cha Expo 70 uelewe kuwa usanii kwenye serikali ya Tanzania haukuanza leo.


View: https://www.youtube.com/watch?v=XfvNvAFcERs
 
Wakuu hivi hili song linaitwaje?

Nililisikia Radio One mtaa wa magoma nika Shazam lakini haikunipa majibu

Mwenye kuujua unaitwaje na umeimbwa na nani?

Kichuguu
Ni clip fupi yenye kelele nyingi sana sikuweza kuitambua, ila ukiweka wimbo mzima naweza kujitahidi.
 
Kundi la Boney M lilianzishwa na mjerumani mmoja akiitwa Frank Farian. Baada ya Boney M kuvunjika, Frank alianzisha kundi jingine lililoitwa Milli Vanilli. Wimbo uliowapa sifa sana Milli Vanilli ni huu hapa ambao ulihusisha waimbaji wawili ambao hawakuwa waimbaji ila waigizaji tu: Fab Morvan and Rob Pilatus. Kwenye wimbo huu, Rob Pilatus anaonekana kama mwimbaji lakini siyo kweli kwani anaigiza midomo ya uimbaji tu, yaani lip-syncing. Mimi niliusikia mara ya kwanza mwaka 1990 baada ya kununua cassete tapes zake pale Kariakoo siku moja baada ya Papa Pulo wa sita kuendesha ibada yake pale Jangwani. Jje wewe uliusikia ukiwa wapi? Ni Wimbo uliovuma sana miaka ya tisini


View: https://www.youtube.com/watch?v=ZbUENJ5FjBk
 
Pale Zaire (wakati huo - leo inaitwa DRC) kulikuwa na mwimbaji Lady Isa. Huyu mama alitoa wimbo huu wa "Kuteleza si Kuanguka" uliovuma sana mwishoni mwa miaka ya themanini. SIjui leo hii huyu mama anafanya shughuli gani lakini wimbo huu ulimpa sifa sana wakati huo. Uliwahi kuusikia na uliusikia ukiwa wapi?



View: https://www.youtube.com/watch?v=wVxMopianEc
 
Mkongwe wa Muziki kutoka Afrika ya Kusini, SIpho Mabuse, alitoa wimbo huu kuisifia Afrika wakati yeye mwenyewe alikuwa hajawahi kufika Tanzania. Alifika Zanzibar kwa mara ya kwanza kama miaka saba tu iliyopita wakati wimbo ulitoka takriban miaka 40 iliyopita


View: https://www.youtube.com/watch?v=-OGZXc_WHpU
 
Back
Top Bottom