Ulisoma english medium au shule ya serikali? Na nini unakumbuka kuhusu shule yenu?

Ulisoma english medium au shule ya serikali? Na nini unakumbuka kuhusu shule yenu?

Nimesoma kayumba 3 S/Msingi, nikahamia EM kuanzia darasa la 5-7.
Kayumba imenifundisha uwajibikaji kufagia eneo langu,kuwahi shuleni,kuishi kijamii bila ubaguzi.
Sema kuombana kulikuwa kunaboa, umenunua zako barafu/mihogo mikono kama 20 ishafika "Noma naomba hata kadogoo, naomba aya sitakupa barafu yangu"
unagawia wenzako unakula kadogo, mixer kulamba barafu yote ili usiombwe, but kayumba was fun.

EM ilikuwa poa sana kwanza tuko wachache, miundombinu imara, library ina maencyclopedia kama 200. EM vitoto vinaringa kinoma kuna pisi nilikubali naitafuta mpaka sahivi inaitwa Winifrida Sylvester kama upo humu jitokeze.

Kuanzia sekondari ya awali mpaka sekondari ya juu nimepiga kayumba, wana na wadada wako peace.

NB: Me ni mtoro konki toxic mtoro, nishawahi kufatwa na Discipline,Academic, na Biology teachers home wakisema niende skuli baada ya kukaa utoro 2months.
Sasa umekua!
 
Saa mshangazi nn tena😉, unanifuria nn😂😂😂😂, nisha kupa tahadhari juu, 'usinvimbie' nawe unafura tu bac naomba nichangie operesheni "Ondoa Kovu"
Wakati mwingine nyie vijana bila kufokewa kidogo hamkitulizi 🤣 🤣 🤣
Hili kovu sitaki liondoke buana, ni kumbukumbu na kila anayeliona analipenda.
 
Nilisoma shule za serikali kuanzia primary, sekondari mpaka chuo.
Nikijitathmini sasa hivi, nina uelewa wa mambo mengi kuliko wengi wa rika langu bila kujali walisoma shule za EM au serikali; zote ni juhudi binafsi.

Pamoja na hayo, mwanangu anasoma shule ya binafsi na hiki kijacho, nimeoanga kisome Cambridge Schools. Nina uhakika shule za binafsi zinarahisisha mambo ilhali kwa shule za serikali, ukitoka, jua wewe kichwa kwelikweli.
 
Kwa uelewa ulionao sasa, unafikiri ungesoma shule tofauti ingekusaidia kwenye maisha, ajira au biashara?
Je, watoto wako watasoma shule kama uliyosoma wewe au utawapeleka kwingine?

Binafsi nimesoma shule ya msingi ya serikali, mkoani Tabora. Nakumbuka nilikua na eneo langu la bustani la kumwagilia na kusafisha kila asubuhi, walimu walikua wakarimu sana na nilifurahia shule.
Vifaa vya darasani vilikua duni, bado nina kovu kubwa pajani la kukatwa na viti vya chuma vilivyokua vimechakaa.

Sekondari nimesoma shule ya private, tulikua tunachagua vyakula na kutengeneza meal plans kila term.
Watoto wangu wamesoma EM, kwa sababu baba yao alitaka wasome huko.

CC:
Nomadix
makutupora
realMamy
Mallerina
Umenikumbusha mbali sana 😅 nimesoma Shule ya serikali na nilipoingia form one hakuna nilichokua naelewa 😀
 
Kwa uelewa ulionao sasa, unafikiri ungesoma shule tofauti ingekusaidia kwenye maisha, ajira au biashara?
Je, watoto wako watasoma shule kama uliyosoma wewe au utawapeleka kwingine?

Binafsi nimesoma shule ya msingi ya serikali, mkoani Tabora. Nakumbuka nilikua na eneo langu la bustani la kumwagilia na kusafisha kila asubuhi, walimu walikua wakarimu sana na nilifurahia shule.
Vifaa vya darasani vilikua duni, bado nina kovu kubwa pajani la kukatwa na viti vya chuma vilivyokua vimechakaa.

Sekondari nimesoma shule ya private, tulikua tunachagua vyakula na kutengeneza meal plans kila term.
Watoto wangu wamesoma EM, kwa sababu baba yao alitaka wasome huko.

CC:
Nomadix
makutupora
realMamy
Mallerina
Both😂😂
Nilianzq kawaida badae nikahama
 
Nimesoma shule za serikali, nakumbuka shule ya msingi kuna mwamba alikuwa memkwa amekomaa sana tulikuwa tunamuita juma vigimbi, huyo mwamba hakuja na mbolea na aligoma kumwagilia maua akachapana na mwalimu wa hisabati, ticha alikula mitama yakutosha tu wanafunzi wa darasa la saba tukashangilia sana... tukatembezewa stick darasa zima.

sijui kama watoto wa sasa wanajua maana ya memkwa 😁
 
Back
Top Bottom