Ulisoma english medium au shule ya serikali? Na nini unakumbuka kuhusu shule yenu?

Ulisoma english medium au shule ya serikali? Na nini unakumbuka kuhusu shule yenu?

Wakati mwingine nyie vijana bila kufokewa kidogo hamkitulizi 🤣 🤣 🤣
Hili kovu sitaki liondoke buana, ni kumbukumbu na kila anayeliona analipenda.
ww kweli ni mshangazi wa nguvu basi😂🤩.

sasa najua nikitulizana tyu naweza pewa ruksa ya kuliona kovu, na naweza kulipenda🤸‍♂️🤸‍♀️🤸‍♂️

Ah, ila naelewa nina wajomba zangu humu hawatafurahishwa na ww kunionyesha kovu ndugu🤣🤣🤣🤣🤣🤣😅😜

....sawa mshangazi nitatulia tyu.
 
Nilisoma shule za serikali kuanzia primary, sekondari mpaka chuo.
Nikijitathmini sasa hivi, nina uelewa wa mambo mengi kuliko wengi wa rika langu bila kujali walisoma shule za EM au serikali; zote ni juhudi binafsi.

Pamoja na hayo, mwanangu anasoma shule ya binafsi na hiki kijacho, nimeoanga kisome Cambridge Schools. Nina uhakika shule za binafsi zinarahisisha mambo ilhali kwa shule za serikali, ukitoka, jua wewe kichwa kwelikweli.
Asante kwa kushare.
Nimeona kwa watoto wangu, shule za binafsi zinarahisisha transition ya primary to secondary.
 
Nilisoma shule za serikali kuanzia primary, sekondari mpaka chuo
nyinyi ndo mlikuwa mnatuchafua maliwatoni. kule mlikuwa mnatumia vyoo vya kulenga. huku mmekuta vyoo vya mchawi mweupe, hessian.

mtu anaingia maliwato anapanda na viatu vyake ile sehemu ya kukalia anashusha mzigo anasepa😜
 
Shule ya msingi nimesoma ya serikali! ... Nakumbuka kwenda na maji shule, kubeba matofali ya kuchoma kwa ajili ya ujenzi.

Umbali wa mahali tunapotoa matofali mpaka shule inapojengwa ni zaidi ya km 2

Nakumbuka moments za kulima na kuvuna shambani!

Secondary niliisoma Private ... Form one to two shule ya kisabato! ... Kila darasa lilikuwa na Pastor wa Darasa ila ni darasa letu tu ndo lilikuwa na Pastor's wawili wa kuchaguliwa na walimu na Mimi wa kuchaguliwa na wanafunzi.

Form two .. Nikahama shule, baada ya Baba kufariki! Nilishindwa kusoma Ile shule maana ilikuwa na vitu vingi vinavyo nifanya nimkumbuke sana Baba!

Ndo nikarudia Tanga, Eckenforde Cambridge ... Hapo Sasa Pombe na Mimi, enzi za viroba vya konyagi ya makatasii ... Kidogo 500 au 600 na Kikubwa 12000 ... Na kula na pariki Ile Barabara ya 4 pale tawakal na Mkwakwani

Walimu wakasema msihangaike na huyo mlevi kwanza hawezi Kufaulu form 4

Ajabu baada ya Matokeo kutoka katika wanafunzi 12 sijui 8 walifaulu kwenda advance na Mimi nimooo 🤣
 
Shule ya msingi nilikuwa na demu wangu anaitwa v ... Baba ake Sasa hivi RPC mkoa fulani!

Alikuwa mweupeee afu Mpoleee ... Niliwahi kuitwa ofisi na mwalimu ambaye ni Rafiki yake na mama ... Akasema nimesikia unamchumbaa ... Nikachezea viboko!

Na yeye akachapwa! From 2004 wakahama tukapotezana ila ajabu nilikuwa namkumbuka miaka yote

Nikiwa chuo kikuu SAUT ... Mwaka wa 3! Nikiwa kwenye mitihani ya Sup za Linguistics

Asubuhi napokea simu! Ni Yeye aiseeeeee! Tuliongea saa zaidi ya Moja! Akaniuliza uko wapi?

Nikamjibu Mwanza akasema nakujaaaaaaaa!

😂😂😂
 
Nimesoma shule za serikali, nakumbuka shule ya msingi kuna mwamba alikuwa memkwa amekomaa sana tulikuwa tunamuita juma vigimbi, huyo mwamba hakuja na mbolea na aligoma kumwagilia maua akachapana na mwalimu wa hisabati, ticha alikula mitama yakutosha tu wanafunzi wa darasa la saba tukashangilia sana... tukatembezewa stick darasa zima.

sijui kama watoto wa sasa wanajua maana ya memkwa 😁
Ila Juma Vigimbi, alikua kashindikana 🤣🤣🤣
Sisi wazee tunaijua MEMKWA na wengine tumesoma na baba zetu wadogo shule 😅
 
Back
Top Bottom