Ulitamani kuwa nani?

BA DS ni nini??? Wengine ni std 7 hatuelewi.
 
Bado naona ndoto yangu ipo natamani kuwa Mataalam wa takwimu.. ili nije kutenda haki kwenye iyo area maan naona wrong figure kila eneo
 
Nimegundua Kati ya watu kumi mmoja ndo hufanikiwa kukamilisha ndoto yake wengine huangukia kwenye kazi ambazo hawakupanga

But whatever ishallah maadamu mkono kinywani
Si kazi, wengine mpaka kwenye mikoa na maeneo wanayoyafanyia kazi sio waliokuwa wanayategemea.
 
Bro mimi sijui kama ilikuwa ndio ndoto yangu au talent, Nikiwa mdogo nilikuwa mhangaikaji kweli kweli kwenye biashara. Nilianza biashara ya kuuza sigara(1984) kwa mtaji wa ZIRO mpaka ukafika sh 1500/=(wakati huo mfuko wa sukari wa kilo 50 ulikuwa unauzwa sh 1000/=). Nilianza kwa kuuza sigara, nikauza magazeti na mifuko ya kutengeneza mwenyewe kwenye bucha za nyama, niliwahi kuza ndizi za kupika kwenye Keep-left, niliwahi kuuza unga wa YANGA, niliwahi kuuza SUKARI kwa kilo. Hiyo ilikuwa ni kati ya 1984 na 1988.
Sasa hivi sijijui mimi ni nani, na sina hela. AIBU
 
Nilitamani sana kuwa MLIPUZI na MCHORONGAJI.
Drealling and Blasting...migodini.........Kila ninanposikia mlipuko napata mzuka kama mwehu.😡😡

Huyu ndio mchorongaji
na hapa ni ulipuzi(blasting)
 
Nilitamani kuwa mwandishi wa habari , lakini nlishia kuwa mwalimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…