Ulitamani kuwa nani?

Ulitamani kuwa nani?

Nilitamani kuwa Mwanaheria, lakini peer pressure ilinisukuma vibaya, pia kukosa ushauri mzuri na kujiamini kulipoteza. Nilifaulu vizuri sana form six, nikaambiwa sheria ngumu sana, utadisco, nikaomba sheria UDSM nikapata ila nikasema wameniambia sheria ngumu, nikaacha kwenda kusoma sheria nikaishia kusoma UDOM course nyingine kabisaaa BA DS. Ila I believe whatever happen, it happens for a reason, With what i studied imenipa fursa na opportunity nyingi sana nilifanikiwa na kusoma MA, Namshukuru Mungu i am not where i wanted to be, but I am in a place where I not used to be.
BA DS ni nini??? Wengine ni std 7 hatuelewi.
 
Bado naona ndoto yangu ipo natamani kuwa Mataalam wa takwimu.. ili nije kutenda haki kwenye iyo area maan naona wrong figure kila eneo
 
Nimegundua Kati ya watu kumi mmoja ndo hufanikiwa kukamilisha ndoto yake wengine huangukia kwenye kazi ambazo hawakupanga

But whatever ishallah maadamu mkono kinywani
Si kazi, wengine mpaka kwenye mikoa na maeneo wanayoyafanyia kazi sio waliokuwa wanayategemea.
 
"Nilitamani niwe hakimu ni wahukumu watu wabaya hasa waliohusika kwenye kifo cha baba yangu lakini nimeishia kuwa daktari nayaokoa maisha ya watu hata wawe ni majambazi" (mwisho wa kunukuu)

Je wewe ulitamani kua nani? Ndoto yako imetimia au haikutimia?
Ni changamoto zipi ulikutana nazo?

Nawasilisha
Bro mimi sijui kama ilikuwa ndio ndoto yangu au talent, Nikiwa mdogo nilikuwa mhangaikaji kweli kweli kwenye biashara. Nilianza biashara ya kuuza sigara(1984) kwa mtaji wa ZIRO mpaka ukafika sh 1500/=(wakati huo mfuko wa sukari wa kilo 50 ulikuwa unauzwa sh 1000/=). Nilianza kwa kuuza sigara, nikauza magazeti na mifuko ya kutengeneza mwenyewe kwenye bucha za nyama, niliwahi kuza ndizi za kupika kwenye Keep-left, niliwahi kuuza unga wa YANGA, niliwahi kuuza SUKARI kwa kilo. Hiyo ilikuwa ni kati ya 1984 na 1988.
Sasa hivi sijijui mimi ni nani, na sina hela. AIBU
 
Nilitamani sana kuwa MLIPUZI na MCHORONGAJI.
Drealling and Blasting...migodini.........Kila ninanposikia mlipuko napata mzuka kama mwehu.😡😡
simple_img_2.jpg

Huyu ndio mchorongaji
images
na hapa ni ulipuzi(blasting)
 
Nilitamani kuwa mwandishi wa habari , lakini nlishia kuwa mwalimu
 
Back
Top Bottom