Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Ni benki gan hiyo ambayo ulifungulia hiyo fixed account
 
Kwa ile video ya equatorial guinea 🇬🇶 bado mna mpango wa kutoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya sherehe ya harusi mi nafkiri mahari inatosha
Hiyo ni ajali Kazini

Unaweza kupewa Mke bure usitoe hata shilingi 10, lakini ukaja kuchapiwa.

Wanasema kuchapiwa hakuepukiki.

Muhimu ikifika zamu yako, kula kama vile kesho huletewi Tena😜
 
Hiyo ni ajali Kazini

Unaweza kupewa Mke bure usitoe hata shilingi 10, lakini ukaja kuchapiwa.

Wanasema kuchapiwa hakuepukiki.

Muhimu ikifika zamu yako, kula kama vile kesho huletewi Tena😜
Bora nipewe bure haitaniuma kma nikiwa nimetumia mapesa mengi
 
Inaonekana suala la Kuoa hujalipa kipaumbele, nashauri ujipe muda wa kutosha uweze kutafakari.

Nina uhakika ukifika above 40 unaweza kuanza kuona umuhimu wa Kuoa na kuwa na familia yako
Nakubaliana na mahari ila kufanya sherehe hilo kwangu halipo
 
Nilijiwekea lengo la kutosumbua watu kwenye michango, na nilifanikiwa
Ila cha kushangaza unasumbuliwa, harusi ni mambo ya kijamii si mbaya kushiriki na wenzako maana na wao watashiriki yako, mwisho wa siku hutachangia wenzako maana hukuomba support zao.
 
Dah sidhani kama nitafanya sherehe, sina hobby na hizo harakati japo mama ndio anaforce, mimi ni msabato nimemwambia wife, nikishatoa mahali mimi nakubeba tutaenda kufunga ndoa kwa mchungaji baadae, asipotaka basi.
Shida ni kwamba wazo la sherehe huanza kuwa organised na wengine kabisa mwishoni unaingizwq mzima mzima kwa ahadi kuwa unafanyiwa harusi ndogo tu.
 
Ila cha kushangaza unasumbuliwa, harusi ni mambo ya kijamii si mbaya kushiriki na wenzako maana na wao watashiriki yako, mwisho wa siku hutachangia wenzako maana hukuomba support zao.
Hii tabia imekuwa kubwa mno miongoni mwetu.

Yaani michango ya harusi inakuwa kama ni lazima, na usipotoa watu wanakununia

Kama hautakuwa makini hadi Mwaka unaisha, unaweza kujikuta unachangia zaidi ya harusi 20 ama zaidi, wakati huo harusi yako uliifanya pasipo kuomba hata shilingi 10 ya mtu🙌
 
Shida ni kwamba wazo la sherehe huanza kuwa organised na wengine kabisa mwishoni unaingizwq mzima mzima kwa ahadi kuwa unafanyiwa harusi ndogo tu.
Hatari sana 🙌
 
Ila cha kushangaza unasumbuliwa, harusi ni mambo ya kijamii si mbaya kushiriki na wenzako maana na wao watashiriki yako, mwisho wa siku hutachangia wenzako maana hukuomba support zao.
Mimi nachangia tu nikiona kuna ulazima/umuhimu wa kuchangia, sio zote lazima uchangie.

Lakini, mtazamo wangu ni kuwa kama unajiweza hamna haja ya kusumbua watu kwa kuwaomba michango, fanya jambo kiasi watakaoamua kukusupport wafanye hivyo bila kusukumwa na wale ambao hawataki napo isiwe case.

Imagine harusi inaandaliwa ndani ya miezi 6 kisa mtu unakomaa kuomba watu michango ilihali una uwezo, its chaos!
 
Miezi 6 ya kuwakomalia ndugu na jamaa wakuchangie harusi, wakati huo huo unataka harusi ya shilingi milioni 20 halafu muhusika ana shilingi milioni 1 kama kianzio

Milioni 19 zote zinategemea wadau 🙌
 
Kuna kijana wa jirani yangu yeye binafsi hakutaka makuu kutokana na hali aliyonayo,nia yake afunge ndoa kanisani kisha jioni awatoe wanafamilia wa karibu kwa chakula cha jioni
Ndugu sasa Oh hiyo kitu haiwezekani lazima tufanye sherehe,Dogo akamwambia sawa kama ndiyo hivyo andaeni hiyo sherehe
Mie ni mmoja wa wanakamati ninavyoandika hapa tumeshafanya vikao viwili ...... sioni dalili ya kufanikiwa kwani hao waliokuwa wanataka sherehe siwaoni vikaoni na ukiwapigia simu za ahadi ya michango....hizo ahadi zao sasa😞
 
Ndiyo maana kwenye utangulizi wa hii mada hapo juu, nimeelezea kwamba mara zote wanaoshinikiza sherehe za harusi ni ndugu either wa kikeni ama kiumeni bila kujali uwezo uliopo.

Usipo tafakari vyema, unaweza kujikuta unalazimika kuingia Kwenye madeni ili kuwafurahisha ndugu na jamaa kufanya sherehe kubwa, lakini baada ya hiyo sherehe ukajikuta unaishi kwenye ukata na madeni yasiyoisha wewe na Mkeo hadi mkajikuta mnakonda kwasababu hizo 🙌
 
Watu kama hao ningewanyoosha. Ikifika siku ya siku baada ya church, picha, afu tunaenda kwa shishifood au buhetifood ndo nimemaliza. Kila mtu na mipango yake, nini kuchoshana. Watu tuliolewa kimya kimya na maisha yanasonga, mi nialikwe kwenye kamati naenda na plan ya harusi ndogo, na yeyote atakaetaka sherehe aahidi kuanzia laki tano esp kama bwana harusi choka mbaya.
 
Hizo gharama za kuwapeleka maharusi na waalikwa ShishiFood nani atagharamia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…