Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Sijawahi fanya sherehe yoyote tangu nizaliwe..
Watanifanyia ya mazishi.
Mimi pia nilikuwa na huo mtazamo, I was so rigid.

Nilikuja kuubadirisha baada ya kuona mgogoro umekuwa Mkubwa Kwa mwenzangu kutaka hayo mambo ya harusi.

Mwisho wa Siku wanasema funika kombe mwanaharamu apite

Sasa nimebaki kusubiri sherehe ya mazishi yangu japo sitaweza kuishuhudia πŸ™Œ
 
ki kanuni za pesa ulicheka mzee mwenzangu sema ndio imeshatokea
Kwa kweli Mzee mwenzangu, kutumia 10M kugharamia harusi nilichemka

Hicho kiasi ningekuwa nimeingiza kwenye Mradi wa ufugaji wa Samaki saivi ningekuwa mbali kiuchumi πŸ™Œ
 
Kununiwa kawaida babu...who cares?
Afadhali umeturahisishia Wazee wenu kazi, akija Kijana wa Kuoa.

Tunapokea mahari yako kisha tunawafungisha Ndoa ya kimya kimya mkaendelee na maisha huko Mjini
 
Afadhali umeturahisishia Wazee wenu kazi, akija Kijana wa Kuoa.

Tunapokea mahari yako kisha tunawafungisha Ndoa ya kimya kimya mkaendelee na maisha huko Mjini
Baaas, imeisha hiyo πŸ₯΄
 
Nilipokuwa katika harakati za kuoa, nilikuwa napambana kumalizia ujenzi wa yatakoyokuwa makazi ya mimi na mwenzangu. Sikutaka michango ila muda ulipokaribia familia ikaingilia kati na kusema lazima nichangiwe na watu wahudhurie kama vile tu mimi nanavyochangia wengine. Niligoma kidogo ila baadae nikakubali tu mambo yaishe kwa amani.

Nikajichagua kuwa mtunza hazina. Michango ikiingia tu naelekea 'hardware'. Nikakamilisha makazi. Kiasi cha michango kilichobakia ndicho nikakipangia sherehe. Siku ya siku watu wakahudhuria na kufurahia sana.
 
Hiyo hela mi Bora ninunue honda click tu
 
Mademu wa sasa hata buku inatoshaa
 
Kwahiyo hela ya michango ya harusi wewe ukajengea??

Una bahati ulibakiwa na Salio la kukamilisha harusi yako, otherwise ungeandikwa kwenye magazeti Kwa herufi kubwa "Bwana harusi atoweka na michango ya harusi Siku 3 kabla ya harusi" πŸ˜…
 
Babu nilivyo na stress na yule mpare hata hicho kipare unadhani naweza kujifunza!! Kwanza ili nikakitumie wapi🀣🀣
 
Aiseee wanawake wana nguvu hao.
 
Kwahiyo hela ya michango ya harusi wewe ukajengea??

Una bahati ulibakiwa na Salio la kukamilisha harusi yako, otherwise ungeandikwa kwenye magazeti Kwa herufi kubwa "Bwana harusi atoweka na michango ya harusi Siku 3 kabla ya harusi" πŸ˜…
Yes mkuu. Niliona nifanye mambo ya maana kwanza na michango ilikuwa inaingia tu. Kiukweli naweza kusema nilipiga mahesabu vizuri ama nilichanga karata zangu vizuri. Kwa bahati nzuri, hata baada ya yote na baada ya harusi, bado kuna ka 'balance' nilibaki nako mfukoni kakanisogeza sogeza kwa miezi kadhaa.

Hata wadogo zangu wanaonifuata nikawaambia wakijikuta katika harakati za ndoa, wahakikishe pesa za michango wanakaa nazo wenyewe na wafanye mambo ya maana kwanza πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…