Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Sijawahi fanya sherehe yoyote tangu nizaliwe..
Watanifanyia ya mazishi.
Mimi pia nilikuwa na huo mtazamo, I was so rigid.

Nilikuja kuubadirisha baada ya kuona mgogoro umekuwa Mkubwa Kwa mwenzangu kutaka hayo mambo ya harusi.

Mwisho wa Siku wanasema funika kombe mwanaharamu apite

Sasa nimebaki kusubiri sherehe ya mazishi yangu japo sitaweza kuishuhudia 🙌
 
ki kanuni za pesa ulicheka mzee mwenzangu sema ndio imeshatokea
Kwa kweli Mzee mwenzangu, kutumia 10M kugharamia harusi nilichemka

Hicho kiasi ningekuwa nimeingiza kwenye Mradi wa ufugaji wa Samaki saivi ningekuwa mbali kiuchumi 🙌
 
Kununiwa kawaida babu...who cares?
Afadhali umeturahisishia Wazee wenu kazi, akija Kijana wa Kuoa.

Tunapokea mahari yako kisha tunawafungisha Ndoa ya kimya kimya mkaendelee na maisha huko Mjini
 
Nilipokuwa katika harakati za kuoa, nilikuwa napambana kumalizia ujenzi wa yatakoyokuwa makazi ya mimi na mwenzangu. Sikutaka michango ila muda ulipokaribia familia ikaingilia kati na kusema lazima nichangiwe na watu wahudhurie kama vile tu mimi nanavyochangia wengine. Niligoma kidogo ila baadae nikakubali tu mambo yaishe kwa amani.

Nikajichagua kuwa mtunza hazina. Michango ikiingia tu naelekea 'hardware'. Nikakamilisha makazi. Kiasi cha michango kilichobakia ndicho nikakipangia sherehe. Siku ya siku watu wakahudhuria na kufurahia sana.
 
Hiyo hela mi Bora ninunue honda click tu
 
Suala la Kuoa ama kuolewa bado litaendelea kuwa ni hitaji muhimu miongoni mwa Jamii ya watu wengi Ulimwenguni.

Kwa Tanzania, tunazo Ndoa za aina mbalimbali ambazo zinatambulika kisheria ambazo ni Ndoa za Kidini, Kimila na Kiserikali.

Mara baada ya kufunga Ndoa, maharusi wengi Kwa kushirikiana na jamii zao, hupenda kufanya sherehe. Sherehe hizo huambatana na michango Kwa walio wengi kupitisha Kadi kwaajili ya kuomba kuchangiwa kufanikisha sherehe za harusi zao.

Japo baadhi hufanya sherehe za harusi zao pasipo kuomba michango Kwa ndugu/jamaa na marafiki. Wao hugharamia Kila kitu wao wenyewe na hao ndugu/jamaa na marafiki hupewa Kadi za mwaliko kuweza kuhudhuria sherehe tu.

Kwa utafiti usio rasmi, sherehe za harusi hupendwa zaidi na Wanawake kuliko Wanaume. Wanaume wako tayari kufunga Ndoa za kimya kimya lakini sio Wanawake.

Je, ulitumia fedha kiasi gani kufanikisha harusi yako ama umepanga kutumia fedha kiasi gani kwaajili ya harusi yako na mwenzi wako?

Binafsi, nilitumia kiasi cha shilingi milioni 10 kuweza kufanikisha harusi yangu na Bibi yenu miaka kadhaa iliyopita 🤗🙏

Sikuhitaji kuchangiwa fedha kufanikisha sherehe ile, bali niliweza kujipanga mwenyewe Kwa muda wa miaka 5.

Nilifungua akaunti maalumu Benki (Fixed deposit account) ambayo nilikuwa nina ruhusiwa kuweka fedha pasipo kutoa Kwa muda wa miaka 5 hivi, japo nilikuwa napata interest kidogo za Benki.

Baada ya miaka 4 hivi, nilikwenda kuchungulia fedha nikakuta nina milioni 9.35 so nikaanza maandalizi kujiandaa na harusi Mwaka unaofatia.

Mind you, tayari nilikuwa nina Cheti cha Ndoa ya Serikali na mwenzangu lakini yeye Kiu yake ni lazima tukafunge ile ya Kanisani 🙌

Kuna wakati nilikuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza mazao ya nafaka. Nilikuwa naenda Mashambani, nawakopesha fedha Wakulima then wakati wa mavuno nilikuwa naenda kukusanya mazao hasa zao la Mpunga.

Kwahiyo kwenye ile harusi, sikuwa na hofu ya Chakula maana tayari nilikuwa nina stock ya magunia ya kutosha ya Mpunga.

Wanasema harusi ni kula na Kunywa. Kwahiyo nilijiandaa kwenye eneo hili.

Kwenye upande wa Chakula niliandaa wali mweupe,Pilau, chips, mtori, nyama za kukaanga, kachumbali

Vinywaji niliandaa Soda na Maji tu.

Niliandaa Kadi za Mwaliko za watu 300 lakini walifika watu 358 japo hili nilijua lazima lingetokea maana harusi yenyewe niliifanyia Kijijini kwahiyo wengi ni wale watu mnajuana. Kwahiyo niliweka chakula na Vinywaji Kwa zaidi (excess budgeting)

Pamoja na Wageni waalikwa, usiku ule nilikuwa na Mchungaji pamoja na Mwinjilisti ambao walishiriki kuanzia mwanzo wa harusi hadi tunamaliza tukio majira ya saa 9 usiku.

Gharama za mavazi za Wapambe niligharamia mwenyewe kuanzia mavazi ya Kanisani hadi Ukumbini 🙌

Niliamua kukodisha Ma-MC wawili ili kunogesha sherehe 🤗

Pete nilinunua zenye ppt ya dhahabu, kuogopa zisije kupauka.

Mchanganuo wa Bajeti yangu kufanikisha sherehe ile, nimeambatisha kwaajili ya wengine kujifunza.

Kumbukeni, hata kama umeoa bado unaweza kuja kuozesha watoto wako miaka ijayo. Baadhi yetu mnaweza kuwa Wanakamati kwenye harusi za wengine pia

Kwahiyo Harusi zitaendelea kufanyika hata baada ya kufa kwetu maana tutakuwa tumeacha Kizazi chetu kinaendelea Kuoa na kuolewa.
Mademu wa sasa hata buku inatoshaa
 
Nilipokuwa katika harakati za kuoa, nilikuwa napambana kumalizia ujenzi wa yatakoyokuwa makazi ya mimi na mwenzangu. Sikutaka michango ila muda ulipokaribia familia ikaingilia kati na kusema lazima nichangiwe na watu wahudhurie kama vile tu mimi nanavyochangia wengine. Niligoma kidogo ila baadae nikakubali tu mambo yaishe kwa amani.

Nikajichagua kuwa mtunza hazina. Michango ikiingia tu naelekea 'hardware'. Nikakamilisha makazi. Kiasi cha michango kilichobakia ndicho nikakipangia sherehe. Siku ya siku watu wakahudhuria na kufurahia sana.
Kwahiyo hela ya michango ya harusi wewe ukajengea??

Una bahati ulibakiwa na Salio la kukamilisha harusi yako, otherwise ungeandikwa kwenye magazeti Kwa herufi kubwa "Bwana harusi atoweka na michango ya harusi Siku 3 kabla ya harusi" 😅
 
Kwahiyo umeamua kusisitiza ulichoongea Kwa Kipare?

Ngoja nimwite Mjukuu wangu Atoto aje anisaidie kutafsiri hicho Kipare

By the way, Bajeti ni muhimu. Vinginevyo baada ya harusi Mume anaweza kuanza kutembea huku akiongea pekeyake kutokana na stress za madeni
Babu nilivyo na stress na yule mpare hata hicho kipare unadhani naweza kujifunza!! Kwanza ili nikakitumie wapi🤣🤣
 
Mimi pia nilikuwa na huo mtazamo, I was so rigid.

Nilikuja kuubadirisha baada ya kuona mgogoro umekuwa Mkubwa Kwa mwenzangu kutaka hayo mambo ya harusi.

Mwisho wa Siku wanasema funika kombe mwanaharamu apite

Sasa nimebaki kusubiri sherehe ya mazishi yangu japo sitaweza kuishuhudia 🙌
Aiseee wanawake wana nguvu hao.
 
Kwahiyo hela ya michango ya harusi wewe ukajengea??

Una bahati ulibakiwa na Salio la kukamilisha harusi yako, otherwise ungeandikwa kwenye magazeti Kwa herufi kubwa "Bwana harusi atoweka na michango ya harusi Siku 3 kabla ya harusi" 😅
Yes mkuu. Niliona nifanye mambo ya maana kwanza na michango ilikuwa inaingia tu. Kiukweli naweza kusema nilipiga mahesabu vizuri ama nilichanga karata zangu vizuri. Kwa bahati nzuri, hata baada ya yote na baada ya harusi, bado kuna ka 'balance' nilibaki nako mfukoni kakanisogeza sogeza kwa miezi kadhaa.

Hata wadogo zangu wanaonifuata nikawaambia wakijikuta katika harakati za ndoa, wahakikishe pesa za michango wanakaa nazo wenyewe na wafanye mambo ya maana kwanza 😀😀
 
Back
Top Bottom