Uliwahi kuchapwa fimbo nyingi kiasi gani ulivyokuwa shule?

Uliwahi kuchapwa fimbo nyingi kiasi gani ulivyokuwa shule?

Mi fimbo nilichapwa 40.
Nilitoroka shule nikaona msala kesho yake nikaenda na sickbook teacher akachukua halafu akacheka akalichana akaniambia nilale chini ni viboko tu halafu ukimaliza unainuka kigangster maana kulialia mbele ya mademu ilikuwa ni ishara ya udhaifu.
2012 hiyo Pomerini Secondary Wilaya ya kilolo Mkoa wa Iringa.
Yule teacher alikuwa mnoko ila somo lake nlkua napasua Sana yaani.
Respect sana walitujenga
 
Pamoja na kusoma nyakati za viboko haswa sijawahi kuchapwa zaidi ya fimbo nne kwa mkupuo.

A level ilikuwa nimalize bila kuonja mbarati hata mara moja sema kuna mpuuzi mmoja aliiba feni ofisini kwa walimu akaileta bwenini, tukanyukwa wote.
 
Watoto wa siku hizi wanadeka sana.

Enzi hizo unaweza ukala fimbo za kutosha shuleni na wala hakuna noma. Mimi shule fimbo ilikuwa ni torati.

Hebu toa ushuhuda ni kiasi gani cha fimbo uliwahi kula kww mkupuo wakati unasoma sekondari?
nilipigwa 10 na maza mzazi kabisa mwalimu na alipomaliza nikamwambia ongeza mi sijaridhika akatupa fimbo kaondoka.
 
Nilimvizia monita wa darasa nje nikampiga ngwala...
Kesho yake nilikula viboko bila idadi mwili mzima....
 
Kuchapwa fimbo shuleni ni Moja ya dalili za umaskini, siamini shule kama braeburn, feza, st Constantine, ist, ism na shule zinazofanana na hizo watoto wanachapwa. Hizo shule watoto hwwachapwi na bado watoto wengi kwenye hizo shule wanafaulu.

Shule za umaskinini mtoto anachapwa fimbo nyingi na bado anakua kilaza, Yani umaskini mbaya sana kiuhalisia ni kama mtoto anaadhibiwa shuleni sababu ya umaskini wa mzazi, na si kwasababu ya kosa lake
 
Vitatu mbele ya shule mda wa parade namchukia yule mwalimu mpaka leo
 
Kuchapwa fimbo shuleni ni Moja ya dalili za umaskini, siamini shule kama braeburn, feza, st Constantine, ist, ism na shule zinazofanana na hizo watoto wanachapwa. Hizo shule watoto hwwachapwi na bado watoto wengi kwenye hizo shule wanafaulu.

Shule za umaskinini mtoto anachapwa fimbo nyingi na bado anakua kilaza, Yani umaskini mbaya sana kiuhalisia ni kama mtoto anaadhibiwa shuleni sababu ya umaskini wa mzazi, na si kwasababu ya kosa lake
Fimbo haijawahi kuwa means nzuri yakufundishia wala kuadhibu
 
Nakumbuka 2008 tumetoroka bweni tunaingia mtaani kula maisha kurudi tobo letu limefungwa ruka ukuta tunadakwa temebezewa kichapo sana fimbo kama 100 hivi kumekucha hatuwezi kutembea tukaona hatuwezi kufa kizembe shuleni kuna mizinga ya nyuki tukawachokoza watu walitoka manundu alafu sisi hatupo tulikausha kimya dah wana sijui wako wapi sasa hivi hope wanapambania kombe fresh ✌🏼
 
Back
Top Bottom