Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
ULIWAHI KUJIULIZA NINI KITATOKEA WANAHARAKATI NA WAPIGANIA HAKI WAKIUNGANA NA WATAWALA?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Wanaharakati na wapigania Haki wanafanana kwa mambo mengi Sana na Watawala. Tofauti iliyopo ni upande tuu.
2. Ni kama Shetani na Malaika. Wanafanana karibu Kila kitu tofauti ni upande.
3. Watawala wengi they don't care about people. Na hiyo ni Dunia nzima. Watawala haawajali kukuhusu wewe. Hiyo ndio sifa ya Kwanza ya Watawala wa Dunia. Only thing they care ni maslahi yao tuu.
4. Ukiona Mtawala anajali kukuhusu wewe ujue kuna potential kubwa anapata kwako. Huo ni ukweli.
5. Watawala kuliko ajiudhulu yeye(MTU mmoja) yupo radhi mfe maelfu kwa maelfu ya watu yeye aendelee kubaki madarakani. Hiyo ni sifa za asiimia 99% ya watawala. Hawajali na kamwe hawatajali kukuhusu.
6. Oooh! Mtibeli tumechoka na magazeti yako. Sawa. Acha nifupishe. Mambo yafuatayo yanawafanya wanaharakati na wapigania haki Vs Watawala Kufanana;
a) AKILI.
Mtawala yeyote unayemuona anaakili kuliko wengi anaowatawala.
Sio lazima awe na akili ya kurusha rocket. Nope! Akili ya kuongoza makundi mbalimbali ya watu iwe kwa hiyari yao au kimabavu.
Uwezo wa kutumia rasilimali za wengine ikiwemo akili za watu wengine kumfanya aongoze.
Watawala na wanaharakati wanafanana AKILI kwa sehemu kubwa.
Isipokuwa mmoja kaamua kukaa upande huu mwingine kaanya kukaa upande ule.
Watawala wote sio kwamba hawajui haki ni kitu gani. Wanajua vizuri Sana. Isipokuwa Haki haiwanufaishi na inagusa maslahi yao
Huziwe kuwa Mwanaharakati alafu ukawa mbumbumbu.
b) Ujasiri na uthubutu.
Wanaharakati wanaujasiri Sana Hilo hata watawala wanalijua. Huwezi ukawa mwanaharakati ukawa muoga.
Na huwezi kuwa mtawala bila kuwa Jasirii
Ujasiri wa Watawala na wanaharakati sio wakufundishwa kama wanajeshi. Nope. Wanajeshi au Askari hufundishwa ujasiri ingawaje wapo wachache ni jasiri kwa kuzaliwa ila wengi wao wamefundishwa ujasiri jeshini
Watawala wao ujasiri wamezaliwa nao. Mtawala haogopi chochote mbele ya utawala wake. Ukimuona anaogopa ujue anazuga. Mwanaharakati nao sio waoga. Yaani fikiria Mtu hana jeshi, Hana pesa, Hana lolote lakini anakimbizana na kufokeana na serikali huku asilimia 90% ya watu wakifyata mikia.
Mtawala Jambo kama halina maslahi yake hatasita kukataa. Mwanaharakati kama Jambo halina haki au interests zake atakataa katakata mbele ya macho yako.
7. Tofauti iliyopo ni upande na mmoja ana power mwingine Hana. Mmoja kaamua kujali maslahi yake kuliko Haki mwingine anapigania haki.
8. Kumbuka wapo watu wajiitao wanaharakati na wapigania haki lakini ni watawala wasio na mamlaka yaani Wasaka mamlaka.
9. Ukifuatilia kwa umakini wanaharakati wengi wanaakili na vipaji vya Kila aina. Sio watu wa kukosa hela ya Kula.
10. Mwanaharakati na mpigania haki hawezi kusumbuliwa na vitu vidogo kama basic needs.
10. Kama ikitokea Wanaharakati, wapigania haki Wakaungana na watawala au wakaamua kukaa kimya mambo yafuatayo yatajiri;
a) Jamii itaonja joto la jiwe kwa dhulma na uonevu kushamiri.
b) Kikundi cha wapambe na machawa kitakufa automatically kwani hakitakuwa na umuhimu.
Kazi ya wapambe na machawa ni kupambana na wanaharakati na wapigania haki wanaokosoa na kuonyesha ubaya wa watawala. Hivyo kama wakosoaji hawapo Kazi Yao itakuwa imekufa.
c) Maendeleo kusuasua na Tabaka la juu kuzidi kuneemeka huku maskini na wenye upeo mdogo wakizidi kuumia.
Elewa Wenye Akili hata uje utawala wa shetani mwenyewe hawawezi kuishi maisha magumu kivyovyote.
Kitendo cha kuishi maisha magumu ni kielelezo kuwa akili yako imeshindwa ku-match na mfumo.
d) machafuko na vurugu kutokea Hali ikiwa mbaya Sana.
Sio kwamba watapata ukombozi hapana. Ni kwa sababu wamebakiwa na option moja kama Wakoma. Aidha wapigane wafe au wakae kimya wafe. So kupigana ndio option.
Lakini hata wakipigana haitawasaidia kwa sababu hawana akili ya kutosha kuishi maisha mazuri.
So watawala watajivua Gamba kwa njia moja na kuvaa gamba jingine kuwazuga wakijifanya ni watu wengine kumbe ni walewale.
Watalegeza kidogo kwenye mahitaji ya msingi. Kutokana na upeo wa watu wengi kuwa Mdogo wataona wamefanikiwa na wameshinda.
11. Watawala wanajua watu wenye upeo wa chini ambao ni wengi na kama sio wengi watahakikisha wanakuwa wengi. Wawe na mtazamo wa Wanyama;
12. Kwamba mtu akipata Basics need hayo ni mafanikio. Yaani inatosha.
Ndio maana watawala watakuambia Jambo Fulani halikuletei Chakula mezani.
MTU yeyote akikuambia hivyo ujue amekuona ni akili mgando.
13. Chakula ni Jambo ambalo hata mjinga wa mwisho kabisa hawezi kukosa. Kama wanyama wasio na utashi wanakula iweje mwanadamu mwenye utashi.
14. Mwanadamu hapiganii chakula, kulala au mavazi. Hayo mambo yapo automatically lazima uyapate na mfumo wa asilli umejengwa uyapate mambo hayo.
15. Watu wanapambana kwaajili ya UTU, HAKI, UPENDO, UKWELI, AKILI n.k.
16. Je hizo basic needs na wakati unatimiza malengo yako utu wako unazingatiwa?
17. Je kuna haki katika njia na mazingira yako?
18. Watawala wanajua katika mazingira ya HAKI Sawa ikifuatwa vile inavyotakiwa wao hawawezi kujipatia Mali nyingi na nafasi yao ya kuongoza kwa muda mrefu inakuwa finyu.
19. Watawala wanasisitiza zaidi Amani kuliko haki kwa sababu Amani ndio inalinda maslahi yao kuliko HAKI.
20. Amani haijawahi kulinda maslahi ya maskini kwani wao Siku zote ni maskini tuu.
Ijumaa Kareem.
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam