Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Hebu taratibu kwanza mkuu. Umejuaje mtoto wa dada yako hajui kufua chupi zake?

Tujadili hili kwanza, hayo mengine yatafuatia!
 
Wewe huwa unawapigia simu kuwajulia hali? Au wao pekee ndio wanatakiwa kukupigia kukujulia hali?
 

Dah umenikimbusha mbali nikiwa mtoto mdogo sana lakini nakumbuka wakati mama anaumwa siku hiyo katembelewa na ndugu yake kaja kumjulia hali

Mama alilia kwa uchungu ninakufa naacha watoto wangu wadogo watateseka aiseee

Mama alifariki after three years mdogo wangu akaniacha after 4 years baba naye akaenda weeee nilionja magumu ya kuishi na ndugu natamani wazazi wangekuwepo hata kama tungekuwa maskini ila sio kuwa yatima

Mama pumzika sasa uwe na amani nimekua ….. niko kwangu sina mateso tena [emoji120][emoji120][emoji120][emoji24]
 
Katika kitu chenye ukatili kwa wanadamu na viumbe vingine humu duniani ni mauti. Basi tu kwa kuwa tumejikuta tumezaliwa duniani bila kupenda wala kuulizwa kama tulitaka kuja duniani. Kifo huku una watoto wadogo ni maumivu makali sana kama leo ungekutana na mtu aliyekufa huku anajua watoto wake ni wadogo ungemuuliza alijisikiaje wakati anakufa, dahh very painfull. Mauti nzuri ukiwa huna familia au watoto wakiwa watu wazima.
 
kila Comment ni wanawake tuu hivi viumbe acha TU.mimi nilipomaliza form four nikasema embu niende kwa mjomba nikapumzike wewe nilioyaona kwa mke wake nilikaa siku tatu TU nikarudi kijiji nikajisemea Mimi huu umasikini wangu niache kufata maisha ya watu.
 
Nimeishi na shangazi yangu tangu nikiwa mtoto mdogo sana na nilikuwa nafikiria kuwa yeye ni mama yangu! Sikupata taabu yoyote katika kuishi kwangu kwake, alikuwa mwema sana na alinipenda sawa na watoto wake.

Kwake tulijifunza kazi zote , tulikuwa tunafanya kwa zamu na Kila mmoja alikuwa na siku yake maalumu ya kupika, kuosha vyombo, kufagia uwanja, kudeki na kupasha maji kwaajili yake .

Kwa muda huo tulikuwa tunaona kama ni mateso na unyanyasaji uliopitiliza.

Nilitambua baadae sana kwamba ilikuwa ni sehemu ya maandalizi ya maisha ambayo leo naishi.

Watu wengi wanashindwa kuishi kwa ndugu kwasababu wanashindwa kutofautisha mazingira.

Ukienda mahali lazima ujifunze taratibu na miongozo ya nyumba usika, sio kuleta habari / tamaduni za kwenu kwenye ngome ya mtu.
 
Aisee umeniliza kwa maana tunafanana historia sana .

Mungu akutie nguvu

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 

Kuishi ma wifi alietoka kwenye ndoa iliyoshindwa ni kama unaishi na mke mwenzio tuu kashazoea maisha ya kwake ko anataka sheria zake alete hapo au anakukomesha tu kwa kusema kuwa yupo kwa kaka ake[emoji16][emoji16] au anakuonea wivu kwa maisha unyoishi na kaka ake

Ushauri wangu mwache afanye anachotaka usishindane nae hata ukifanya ivo mnakua wote wajinga hata akifanya nn wewe kaa kimya mwisho wa siku yatamshinda tuuu after all hupotezi kitu cha zaid sana unajitesa tuu bure
 
Ila wasisemwe wenye mji tu, vipi wageni wenyewe wanao kuja hapo? Unamhudumia mtoto wa mtu siku akitoka hapo utasemwa mpaka unajiuliza hivi yale niliokuwa nafanya kumbe yote mabaya,

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Fungua Uzi wako acha kupandia topics za wenzio, hiyo haihusiani. Ndo nyienyie tu mnaotesa watu
 
Ultoka salama?
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Aisee kumbe mie na mke wangu tuna roho poa sana, kwangu akifika ndugu y3yote awe wangu wa mke, kula kujigaragaza pesa tu ndio sina za kutapanya ila kula aaah utasaza mwenyewe
Ndugu yangu kumpendeza mwanadamu ni kitu kigumu sana. Unaweza kushangaa hao ndugu zako wamekomenti kwenye huu uzi eti uliwatesa

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…