Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?

Mimi naingia form one tu siku ya ya kurupoti nikaambiwa DOGO WEWE HUMALIZI SEKONDARI NAKUAPIA na sijamkosea kitu yaani anakuja kijambulisha na kufahamiana na wanafunzi kashaanza tayari maneno. Lakini LEO NIPO OFISINI. Cha kushauri tu ni kuwa waalimu kiufupi waachane na tabia hizo za kuwatamkia wanafunzi manene ambayo kwa wengine umri alio nao mwanafunzo anashindwa kustahimili uzito. Japo kuwa mimi ndio yakinifanya nikomae ili ajue kwamba hawezi kuamua hatima yangu bali ni mungu.
 
Baba yako anauza ng'ombe ili alete ng'ombe nyingine shulee🏃‍♂️🏃‍♂️💭💭💭
 
Sijawahi kutamkiwa neno lolote Baya na mwalimu KATIKA maisha yangu yote ya shule.Kwanza nilikua muoga Sana WA fimbo hivo kunikuta kwenye makosa ilikua mara chache Sana.Nakumbuka nilipokua darasa la pili mwalimu WA hesabu alikua anachapa walokosa baadhi ya maswali,hivyo kabla ya kuchapa alikua anasema "Leo nitawachapa Hadi muombe ardhi ifunguke muingie".Dah haya maneno yalikua yananifanya nilie Sana kabla ya kuchapwa.Nilikua nadhani ardhi inafunguka kweli tunadumbukia😭😭😭
 
Niliambiwa na second master hapo Tarime Sec, wewe unavyotusumbua hivi sababu baba ako anakupa pesa nyingi


Tutakufukuza shule, na kweli nilifukuzwa form four nikarudi kukamilisha ratiba ya necta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…