Uliwezaje ku move on kwa mtu uliyempenda sana?

Uliwezaje ku move on kwa mtu uliyempenda sana?

Umenistua kuona Kuna watu bado wanapenda Kwa kiwango hicho ktk Dunia ya leo
 
Uliwezaje ku move on kutoka kwa mpenzi uliyempenda sana?
Kuachana na mpenzi uliyempenda sana ni changamoto kubwa, na inahitaji muda na subira.

Watu wengi hupitia hatua kadhaa ili kuweza kukubaliana na hali hiyo na kuendelea mbele.

Kwanza kabisa, ni muhimu kuruhusu hisia zako zote, iwe huzuni, hasira, au hata kukata tamaa. Kukubaliana na hali hiyo kunaweza kukusaidia kuanza kupona polepole.

Kujihusisha na shughuli unazozipenda au ambazo zinaweza kukusaidia kusahau kidogo. Unaweza kujaribu mambo mapya, kama vile kujifunza ujuzi mpya, kufanya mazoezi, au kusafiri.

Kumpata mtu wa kumwambia unachopitia kunaweza kusaidia sana. Wanaweza kukupa mtazamo mpya au kukufariji unapohisi huzuni.

Pia, hali ya kuwa na malengo yako binafsi na kuyafanyia kazi kunaweza kukupa nguvu mpya. Inaweza kuwa ni wakati mzuri wa kujijenga na kujitunza zaidi.

Na huu ni wakati wa kujikumbusha thamani yako na kujijengea imani upya.

Haina haja ya kuharakisha mchakato huu. Unapochukua muda wako vizuri, utaweza kujenga maisha yako kwa hali ya upya kwa kuielekea furaha yako.

Inaweza kuwa ngumu mwanzoni, lakini baada ya muda, utaanza kuona mabadiliko.

Ova
 
mimi naitumia kutongozea ,nikiwa namtongoza mwanamke namuomba anipe kampani ya kupunguza mawazo namdanganya nimeachwa ,najifanya kama nimeumia moyoni sana

yeye nae anaona awe karibu kunipunguzia mawazo kama binadamu mwenye moyo safi,anakuja kushtuka tayar tumeshakuwa wapenzi.

nb:introvet
 
Thanks for everyone who participated either semi or fully kwenye kunipa ushauri,na kunitengeza kua mpya.

Finally nime recover na ninaweza kufanya mambo yangu vizuri tu bila shida yoyote.

Nilichojifunza katika mahusiano usimpe partner wako 100% maana watu wana change.

Thanks to the almighty God.🙏
 
**""nakuona wewe ni mzuri sana na speed yako sitoweza endana nayo, ngoja nijitafute then nikijipata takutafuta,,,"""
 
Napitia kwenye hii hali.

Naumia sana ila sina jinsi.

Sikuwahi kuwaza kama mapenzi yanaweza kunifanya hivi.

Nahisi kufa kufa tu.
Inabidi ufe kihisia ili uzaliwe upya
.hapo Sasa hakuna kitu itakutesa
 
Kupendwa raha..kupenda mateso, imagine anayekupenda anateseka kiasi gani😂😂😂
 
Nilishindwa kbs kumuacha akaamua kubeba mimba ya mshkaji, hapo sikutazama nyuma tena nikachapa lapa.
 
Napitia kwenye hii hali.

Naumia sana ila sina jinsi.

Sikuwahi kuwaza kama mapenzi yanaweza kunifanya hivi.

Nahisi kufa kufa tu.
Kaza moyo Mzee nikwel kinakuwa kipindi kigumu lakin nikuhakikishie Huwa Kuna kusahau na kuanza upya . Pole sana
 
Back
Top Bottom