Uliwezaje kufungia vyeti kabatini kisha ukajiajiri?

Kujiajiri kunatokana na kuona kitu ambacho wengine hawakioni. Ni kujikana na kuona kila changamoto ni hatua kufikia mafanikio. Ktk nchi ya Tanzania the big Challenge is taxation. Wakati ukiwaza ufanye nini TRA wao wanawazakukukamua kodi.
Hao wafanyabiashara wote wanafanyaje biashara?
 
Mkuu miaka mitatu ni mingi sana hasa unapokuwa ktk taifa kama hili letu,kumbuka kama leo tu-assume ana 3mill kwa sasa akikaa mpaka 2021 akiitia sokoni itaonekama kama 300k kulingana na kila siku kodi za vitu zinapandishwa pia fursa aliyoiona itakuwa imeshapotea.
 
Nilijiajiri, lkn kwa msoto wa magufuli biashara zimeparanganyika.

Sasa nakula tu akiba na hesabu za kirikuu changu.

Nafikiria kuanza kuomba kazi.

Biashara kipindi hiki ni pasua kichwaaa
Kwako wewe mkuu. Biashara inahitaji Ubunifu wa kipekee kabisa. Kama unafanya kile ambacho kila mtu anafanya tegemea ugumu sana.

Hiki hiki kipindi ambacho wengine wanalia.wengine wanapiga pesa
 
lakin si umefanya kazi kwanza ya kuajiriwa ndo ukapata mtaji?
 
Wakuu mje kunitia moyo. Mimi nimemaliza form six mwaka huu. Ila naona ndoto yangu ya ujasiriamali ni kubwa kuliko kupoteza miaka 3 chuo na kozi zisizona uhalisia.
UKitaka kufanikiwa vizuri maishani, tengenevyo vyanzo vitatu vinavyotokana na:-
1: KILIMO
2: Ujasiriamali
3: Taaluma.

Ukichanganya hivyote vitatu, hutokuwa maskini kamwe.
 
Employment is an opportunity that somebody offers you. Ndio maana kila jambo lazima utapangiwa na boss wako. [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kiualisia ni Miaka Mingi lkn Inajenga Experience nzuri unajifunza kuwa agressive na persistence sbbu Business is Simple but not easy nlivyoanza miez 3 ya kwanza ilikuwa horrible..nlikosa mpka hela ya luku nkikaa Mwezi nakwepa Bar..fixed cost na kodi zilinikatisha tamaa lakini nlijua lazima itakuwa hvyo Nmesoma Bcom na PG cert Nyingne ila ujuzi wa miaka 3 imenifungua sana.Ss naona mwanga mkubwa yaaan
 
UKitaka kufanikiwa vizuri maishani, tengenevyo vyanzo vitatu vinavyotokana na:-
1: KILIMO
2: Ujasiriamali
3: Taaluma.

Ukichanganya hivyote vitatu, hutokuwa maskini kamwe.
Ujasiriamali unabeba vyote hapo....ila ndani ya ujasiriamali utaamua ufanye vyote au kimoja wapo.
 
Ni utumwa sana unashindwa kukaa karibu na familia kisa kazi za watu, ni bora uwe mbali na familia kwa kitu ulichojiajiri mwenyewe kuliko kaz ya kuajiria
Familia yetu kwa asilimia 95 tumelelewa na mama kwa ukaribu sana, ilifikia hatua nikawa sina urafiki na mzee.
 
Kuwa mbali kwa muda kwa biashara yako ni sawa, lakini kuwa mbali kwa muda wote, kwa ajili ya biashara yako, bado ni sawa na utumwa wa kazi ya kuajiliwa.
.............Una maana gani mkuu!!!au sijaelewa?
Unafanya biashara yako,hela yako hakuna anaekupangia matumizi ninini kitakachokufanya uwe mtumwa?
 
Watu wengi wamepoint passion na vision mimi ngoja nitaje biashara ambazo nimekua na hands on experience halafu tuone mtaji una nafasi gani.

Ukiamua kua unajishughulisha na uuzaji muvi ziwe zilizotafsiriwa au na zisizotafsiriwa utahitaji.

Computer desktop huanzia shilingi 150K mpaka 250K.

Hard disk, kwakua hauna hela unanunua za ndani kisha unazivalisha case ili utumie kama external Terabyte moja ni shilingi 120K unahitaji Terabyte 5 mpaka 10 ili usiwazie space.

Kama unadeal na muvi zilizotafsiriwa (seasons za wakina Murphy) zinatoka kila Jumatatu, kila moja ni 1000 na kwa wastani zinatoka 40.

Fremu kutegemea na eneo ulilopo itaanzia 50K mpaka 120K.

Lakini kwakua wewe biashara unaianza kati inamaanisha seasons za nyuma hauna hivyo utawasiliana na ambao wapo kwenye gemu kitambo ili uzipate za nyuma zote. Ili kumpooza andaa kama 50K.

Kama utadeal na muvi ambazo hazijatafsiriwa pia utahitaji smartphone na vifurushi au nunua modem na kujiunga vifurushi kila siku kwa ajili ya kudownload muvi mpya.

Viti vya wateja na kiti chako jumla ni kuanzia 140K.

Kisha itabidi uwe na balansi ya kukubeba kipindi unabembeleza wateja.

Piga hesabu kwenye hii utahitaji mtaji shilingi ngapi.

Kuna bodaboda, pikipiki ambazo wateja wengi wanazitaka ni Boxer. Dukani boxer ni Milioni 2.4 za wachina ni milioni 1.5. Ukinunua kwa mtu angalau anza na mfukoni uwe na Milioni 1.5 faida ni utakuta kodi na vitu vingine vishalipiwa ila wewe unaweza kugharamia services kidogo ili usonge mbele.
Hesabu kwa siku ni 7K kama hamjapeana mkataba wa akimaliza kukufanyia kazi pikipiki inakua yake dereva, kama mmepeana mkataba huo kwa siku hesabu ni 10K.

Kilimo niliishia njiani niliishia kuwa na ardhi tu lakini ilihitajika kama milioni tano kwa kilimo cha maembe cha ekari moja.

Hoja yangu ni hii kujiajiri kunakula hela, hii siyo siri, sasa wazia kijana niliyemaliza chuo, familia maskini huo mtaji wote natoa wapi? Nakumbuka ilibidi niende kwa mmiliki wa fremu nikamwambia naomba nikulipe kwa siku kwakua sina uwezo wa kukupa hela unayotaka (ilikua kodi ni 70K na unalipa kwa mwaka) nikamwambia kila siku nitakupa 6K.

Hua nahisi kazi pekee ambayo pesa kama mtaji hauhitajiki kwa kiwango kikubwa ni udalali wa magari, hapa unahitaji connections za uhakika tu.

Anyway kila mtu na njia yake wengine njia hazijanyooka wakati wengine zimenyooka. Uwe na bahati njema.
 
Kwamba kabla ya hata kumaliza msimu tayari amepata vyote hivyo, ngumu kuamini.
Anyway mtu kuamua kufanya jambo usije muiga ukidhani nawe utapita katika njia ileile alopita, kila mtu hujua amefanya nini kufanikisha yale yanayoonekana na wengi wetu huwa tunazungumzia mafanikio tunayoyaona bila kujua nini kipo nyuma yake.
 
i mean hana mwaka ameacha kazi.shamba la kuanzia lina kama miaka kama minne
jamaa ana kuku,mbuzi bata mzinga,kondoo,ng'ombe'anafuga samaki anatoa ushauri kwa wakulima wenzie,anahamasisha watu wale matunda kwa afya. jamaa namkubali kinoma though kwao ni wakulima pure so yeye anafanya kisomi
 
but nadhan alikuwa na others sources of income hta reserve alikuwa nayo coz ni vigum sana kuamini mafanikio ya mda mfupi kis hcho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…