Uliwezaje kumsamehe mke/mme wako baada ya kugundua kakusaliti?

Uliwezaje kumsamehe mke/mme wako baada ya kugundua kakusaliti?

Kati ya tiba nzuri sana ya moyo ni kusamehe au kupotezea...

Ukiishi na makosa ya mtu moyoni, kifuatacho ni kypata magonjwa yasiyo na majina wakati mkosaji akiishi kwa furaha tele...

Sana sana ukiona maji mazito, piga chini uishi kwa amani...wachuchu wapo wengi tu
 
Sijui kwa nini watu wanaona kusamehe dhambi ya usaliti ni kawaida tena kwa watu walio kwenye ndoa.

Unapoingia kwenye ndoa ni umeamua kuwa na huyo mtu wako ndio maana mnakula viapo iwe kidini au kimila.

Dhambi ya usaliti haina msamaha. Mimi siku nachukua mke niliwaambia wazazi wa pande zote. Mmoja wetu akionekana msaliti itakua mwisho wa ndoa na hakuta kua na vikao. Wote tukakubaliana
[emoji119][emoji119]
 
Ni wiki mbili sasa tangu bidada agundue mme wake anauhusiano wa kimapenz na rafiki yake wa miaka mingi...

Mdada alikua na rafiki yake tangu 2009 ambapo walikutana chuo wakawa marafiki wakaribu sana mpaka wakaitwa mapacha kwan hata nguo walikua wanavaa za kufanana....

Kila mmoja aliweza kwenda kwao na mwenzie kufikia hatua mpaka wazazi wakawa wanafahamiana ...
Badae wote walipata familia ...2019 bidada huyu alimkaribisha mwenzie nyumban kwake mkoa mwingine alipokua ameolewa akaenda kumsalimia kama familia wakamchinjia mbuzi.... Kama miez miwili hv bidada akashangaa ukaribu wa mawasiliano aliokua nao na rafiki yake ukapungua bila sababu ya msingi...

Kama wiki mbili zilizopita ndio akakuta chating kwenye cm ya mume wake za mapenz baina yake na mume wake. Mume anaomba msamaha tu yaishe alipitiwa ...rafiki mtu ndio hapokei cm kabisaa...
Mdada anshindwa kabisa kumsamehe mwanaume anajikuta roho inamuuma tu kila akifikiria ukaribu aliokua nao na rafiki yake wa miaka 13 umevunjika kijinga sana ....

Uliwezaje kumsamehe mwenzie wako ulipogundua kakusaliti?
Duuh
 
Back
Top Bottom