Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Kwa uhakika nakushauri ujaze fomu ya maombi
Udahili umeanza, Chuo Kikuu Huria Tanzania na vyuo vingine hapa nchini.

Tuna chuo kimoja hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kinachotoa elimu wazi na Masafa(Open and distance learning)

Serikali ilianzisha chuo hiki kwa sheria ya bunge namba 17 ya mwaka 1992. Hii ilikua kuwapa fursa wafanyakazi na watu wenye majukumu yanayowafanya washindwe kwenda conventional university, hivyo kujikuta mahitaji yao ya kujiendeleza kielimu yakishindwa kufikiwa.

Kwa mwaka huu wa masomo udahili utakua ni bure.
Ingia tovuti ya chuo www.out.ac.tz na ufanye online application. Unahitaji kuwa na soft copy ya vyeti na picha(passport size moja).

Kwa tuliosoma na kufanikiwa tujitahidi wenzetu pia ambao wanauhitaji, kuwatangazia waweze kuitumia fursa hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Masomo Huria sio masomo wazi na masafa
 
GPA inayotakiwa kwa mujibu wa wasimamizi wa Vyuo vikuu (TCU)kwa mtu anaepaswa kudahiliwa Kutoka Diploma kujiunga na shahada ya kwanza (Bachelor degree) anapaswa kuwa na GPA ya kuanzia 3.0 zamani ilikua 2.7 lakini kuanzia mwaka wa masomo uliopita imewekwa GPA ya 3.0.

Alternative unaweza kufanya diploma nyingine upate GPA stahiki, au unaweza kufanya mtihani wa kidato cha sita na kupata sifa stahiki au unaweza kufanya mtihani wa RPL unaotolewa na TCU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Foundation Course pia
 
Je kama mtu amedailiwa Julai anaweza kuomba masoma yake yaanze Oktoba (iwe kama amedailiwa Oktoba)? Na taratibu ni zipi za kufanya hivyo?
 
Mkuu me naomba unifahamishe kuhusu mambo kadha wa kadha

1:Kwa mtu mwenye cheti cha Ualimu Grade A anaweza kujiunga OUT na akasoma kozi ya Business Administration ngazi ya Diploma?

2:Na je kama inawezekana ada zao zipoje?

Msaada please nitashukuru sana
 
mie nataka soma cert ya sheria sifa na vigezo ni vipi pia ada ni kiasi gani?
 
Kwenye application Kuna sehemu wanasema O level school ambayo ulisoma.Lakini nafasi ya kuandika haipo na ukitaka kuendelea inasema andika Kwanza jina la shule uliyosoma.Sasa Hiyo shule unaandika wapi
 
Kuna rafiki yangu kila akiomba course ya foundation ana kosa na vigezo anavyo ana D S S advance?
 
Back
Top Bottom