Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Mkuu naomba kufahamu,ili ufaulu foundation course unatakiwa upata ngapi ktk yale masomo 6.

Pia hii ipoje mkuu maana nimeona wengi waliosoma foundation wanalalamika kwamba wakiomba vyuo vingine tofauti na OUT wanakosa kudahiliwa.Naomba utuambie vyuo gani ambavyo vinadahili direct wahitimu wa foundation course.
#Regards
 
FOUNDATION PROGRAM

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinawapongeza wahitimu wote wa Kidato cha Sita ambao matokeo yao yametoka leo.

Sambamba na pongezi tunawakaribisha wote wenye sifa za Kujiunga na _Foundation_ _Program_ waje wajiunge mapema kwani nafasi ni chache sana. Sifa za Kujiunga ni:

(a) Mhitimu wa Kidato cha Sita mwenye ufaulu wa kuanzia Pointi 3.5 mpaka 1.5 kwenye masomo mawili ya Tahasusi.

(b) Mhitimu wa Diploma mwenye GPA ya 2.9 mpaka 2.0

(c) Mhitimu wa NTA Level 5

Tuma maombi yako kupitia tovuti ya chuo au fika kwenye tawi letu la karibu. HAKUNA MALIPO YA KUTUMA MAOMBI
 
Wanaotegemea kufanya supplementary ya foundation course kwenye mitihani inayoanza tarehe 8 September matokeo yao yatawahi kiasi kwamba wataweza kufanya application vyuo vingine?????
Matokeo yatawahi hawawezi kuchelewa
 
Mkuu naomba kufahamu,ili ufaulu foundation course unatakiwa upata ngapi ktk yale masomo 6.

Pia hii ipoje mkuu maana nimeona wengi waliosoma foundation wanalalamika kwamba wakiomba vyuo vingine tofauti na OUT wanakosa kudahiliwa.Naomba utuambie vyuo gani ambavyo vinadahili direct wahitimu wa foundation course.
#Regards
Foundation unapaswa kupata GPA ya tatu, wastani wa B.
Mwaka jana OFP ndio ilikua inaanza hivyo vyuo vilichelewa kuiingiza Kama sifa ya kudahiliwa.
TCU iliagiza vyuo vyote vilivyochini yake viiweke Kama moja ya sifa ya kudahiliwa.
Hii sio programme ya OUT ni programme ambayo ipo under TCU.
 
Mkuu naomba kufahamu,ili ufaulu foundation course unatakiwa upata ngapi ktk yale masomo 6.

Pia hii ipoje mkuu maana nimeona wengi waliosoma foundation wanalalamika kwamba wakiomba vyuo vingine tofauti na OUT wanakosa kudahiliwa.Naomba utuambie vyuo gani ambavyo vinadahili direct wahitimu wa foundation course.
#Regards

Inatakiwa Upate GPA ya 3.0 Wanapokea Vyuo vyote asikudanganye mtu Mimi nilisoma Open
 
Nimefaulu masomo mengine ila nimefail maths ninataka kusoma IT ,nitaweza?
 
Mkuu samahani hio Foundation course unasoma masomo kama uliokua unasoma advance au inakuaje naomba unielewehe apa mkuu
Unasoma
Development studies
ICT
Communication skills
Na mengine Matatu unachagua kutokana na programme unayotaka kusoma Bachelor Kati ya History, kiswahili, English, Geography, Physics, Math, Chemistry, Biology, Economics, Business studies, business mathematics and statistics.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unaweza kufafanua kuhusu executive programme na hiyo distance learning?
Kuna kuwa na
Executive ambayo mnaingia darasani baadhi ya programme na maeneo wanazo hizo progaramme
Evening ambayo wanaingia jioni class
Blended mode hii ni mchanganyiko wa face to face session na distance

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom