Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Udahili umeanza, Chuo Kikuu Huria Tanzania na vyuo vingine hapa nchini.

Tuna chuo kimoja hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kinachotoa elimu wazi na Masafa(Open and distance learning)

Serikali ilianzisha chuo hiki kwa sheria ya bunge namba 17 ya mwaka 1992. Hii ilikua kuwapa fursa wafanyakazi na watu wenye majukumu yanayowafanya washindwe kwenda conventional university, hivyo kujikuta mahitaji yao ya kujiendeleza kielimu yakishindwa kufikiwa.

Kwa mwaka huu wa masomo udahili utakua ni bure.
Ingia tovuti ya chuo www.out.ac.tz na ufanye online application. Unahitaji kuwa na soft copy ya vyeti na picha(passport size moja).

Kwa tuliosoma na kufanikiwa tujitahidi wenzetu pia ambao wanauhitaji, kuwatangazia waweze kuitumia fursa hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu ambaye ni medical doctor by proffesion anaweza akajoin ur university kuchukua MBA?
 
Kwani serikali imeruhusu foundation siku hizo maana Dogo wangu anaitamani degree kinoma noma
Ndio inatolewa na chuo Kikuu Huria pekee
Kwa mwanafunzi aliemaliza form 6 akawa na ufaulu wa walau E na S(cut off point ya 1.5)
Then akiwa amemaliza Diploma walau awe na GPA ya 2.0 and above
 
Wanaotegemea kufanya supplementary ya foundation course kwenye mitihani inayoanza tarehe 8 September matokeo yao yatawahi kiasi kwamba wataweza kufanya application vyuo vingine?????
 
Back
Top Bottom