Uliza swali lolote kuhusu wanyamapori wetu na tabia zao utajibiwa

Uliza swali lolote kuhusu wanyamapori wetu na tabia zao utajibiwa

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
7,033
Reaction score
15,638
Habari waungwana.

leo nimeweka mezani kwa yoyote mwenye swali interest kuhusu wanyama wa porini.uzi huu ni muhimu kujifunza tabia zao maisha yao kama una swali linakutatiza jiskie free uliza kwa kadiri nnavyoweza nitakujibu au ataekuwa na ufahamu zaidi humu jukwaani atakujibu.ni vizuri kufahamu tabia na mienendo ya wanyama wetu ili kuubust utalii wa ndani.

Karibuni wote, sina mengi kwa kuanza tutakuwa na mengi ya kujifunza
 
Nilishawahi kukutana na chui uso kwa uso vu bin vu nikafreeze kwa woga haoooo tukatazamana tu kwa sekunde kadhaa halafu huyo kimya kimya akaenda zake. Tangu hapo navutiwa sana na mnyama huyu msiri; na ningependa kujua tabia zake za msingi. Huwa anashambulia binadamu? Anapenda kuwinda wakati gani? Maisha yake yakoje kwa ujumla?
 
Nilishawahi kukutana na chui uso kwa uso bin vu nikafreeze kwa woga haoooo tukatazamana tu kwa sekunde kadhaa halafu huyo kimya kimya akaenda zake. Tangu hapo navutiwa sana na mnyama huyu msiri; na ningependa kujua tabia zake za msingi. Huwa anashambulia binadamu? Anapenda kuwinda wakati gani? Maisha yake yakoje kwa ujumla?
Chui unaweza kulala naye juu ya mti usijue halafu ye akakuona akakuacha tu mpaka kuna kucha unafungua macho anakupita miguuni anaelekea kwenye mishe zake.

Kuna wanyama nuksi yani hata kama limeshiba likikukuta litapata tamaa kutaka kukuua likufanye akiba ya msosi wa kesho
 
chui ni mnyama mwenye aibu sana.yupo kwenye kundi la carnivore(wala nyama)jamii ya paka.chui ni mnyama solitary(wanaishi kibachela).chui maisha yake yote anapendelea kuishi juu ya miti hii ni sababu ya food competition.ana uwezo wa kupandisha juu ya mti mnyama mwenye uzito mara 3 kumzidi.kumuona chui ni bahati sana sababu wana aibu na wanapenda kujificha sana.ikitokea amepata mwanamke basi anamtia mimba kisha kila mtu anaenda na 50 zake.anatumia mkojo na kinyesi kuweka alama ya mipaka yake ina maana ukikatiza katika home range(territory) yake anakupasua.anawinda kwa kuvizia na kushtukiza(ambush & stalk).yapo mengi zaidi utazidi kujifunza mbeleni hiyo ni briefing tuu
 
asant
fisi miguu ya MBELE ni mirefu na ya nyuma mifupi hivi inamsaidiaje kwenye maisha yake ya kila siku..sababu kila mnyama anapata faida ya vile alivyoumbwa..
asante kwa swali zuri sana.
miguu ya mbele kuwa mirefu humsaidia kuinua vitu vizito hasa mizoga lakini haijawa confirmed in researche.ila kiuhalisia fisi ana kichwa na mifupa mizito sana hivyo angekuwa na miguu mifupi mbele angekuwa anapinduka.fisi anapata sufficient calcium from bones and carrions.hivyo inamfanya kuwa mnyama wa kwanza kuwa na powerful and massive jaws from all scavengers.
 
Chui unaweza kulala naye juu ya mti usijue halafu ye akakuona akakuacha tu mpaka kuna kucha unafungua macho anakupita miguuni anaelekea kwenye mishe zake.

Kuna wanyama nuksi yani hata kama limeshiba likikukuta litapata tamaa kutaka kukuua likufanye akiba ya msosi wa kesho
mnyama yoyote mkali duniani usimpe nafasi moja tuu.kama unamwangalia ukapepesa jicho pembeni kidogo tuu umekwisha.tunavyojuwa jamii ya paka wote wana aibu sana ukiweza kumwangalia usoni bila kupepesa atakuacha.ila usijaribu hicho kitu porini sababu hili ni angalizo tuu.
 
Nasikia Simba waliopo kwenye mbuga ya Manyara ndio Simba pekee duniani wenye uwezo wa kupanda na kukaa juu ya miti..

Unaweza kueleza ni kwa sababu gani?
hapana wapo simba sehemu zingine wanafanya hivyo.kwa manyara sababu zipo nyingi.manyara ni eneo lenye misitu hyo wanapanda juu ili kutafta kitoweo.pili manyara ina unyevu sana chini hvyo wanakimbia ule ubaridi na wale siafu.kingine miti ya wanayopanda simba haiko vertical iko horizontal km ilivyo ya manyara.
 
Back
Top Bottom