Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

VRN Ina umuhimu gani?
Naomba nimsaidie maana naona kaleta mada chokozi lakini hana majibu, VRN navyofahamu mimi ni vat registration number kwa lugha mama ni namba ya usajili wa vat.Faida yake ni kama umesajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani yaani vat risiti zote za mauzo yako au manunuzi inatakiwa namba ya muuzaji na mnunuzi kama wote ni vat register ionekane kwenye risiti sababu ukiuza sana kuliko kununua unapeleka tra hiyo vat na kinyume chake ukinunua sana na ukawa haujauza sana basi ile tofauti ya manunuzi na uuzaji unarejeshewa na tra.Ili uweze rejeshewa risiti lazima iwe na hiyo vrn ya aliyekuuzia na ya kwako kwenye risiti ya manunuzi.
 
Nahitaji kujua process za Kusajili ecommerce company. Mfano kama Amazon/Alibaba ambazo ni mtu wa kati hazjna maduka.
Utaratibu wa kufungua kampuni ni ulele ila wakati wa kufungua ndiyo utaeleza aina ya biashara yako kwenye memorandum of association. utajisajili brella baadaye TRA
 
Kama una swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa usajili wake, kufanya mabadiliko, kodi za TRA na chochote kile kinachohusu kampuni kwa BRELA na TRA uliza hapa nitakujibu.

Karibu
Mkali wao wadau tunaomba majibu basi maana umesema tuulize sasa ni aje?
 
Gharama ya kusajili limited coy ni shilingi ngapi?

Gharama ya kusajili limited company huwa inategemea na share capital yake, nakuainishia kila kundi la share capital na gharama yake hapa chini


Mtaji Gharama za usajili
1. 20k-1M - 167,200
2. 1M-5M- 247,200
3. 5M-20M- 332,200
4. 20M-50M- 362,200
5. 50M mpaka mwisho 512,200
 
Nahitaji kujua process za Kusajili ecommerce company. Mfano kama Amazon/Alibaba ambazo ni mtu wa kati hazjna maduka.

Utaratibu wa kusajili kampuni ya aina yote ile huwa unafanana, utofauti huwa unakuja kwenye kupata vibali na leseni za biashara.

Ili kusajili kampuni mpya kwanza kabisa inabidi waanzilishi wa kampuni muwe wawili na kuendelea, na pia kama wote ni watanzania ni lazima muwe na namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na namba za TIN zenu binafsi, ila kama kuna raia wa kigeni inabidi awe na passport ya kusafiria.

Baada ya hapo taratibu nyengine zitafuatia kama vile kuandaa Memorandum and Articles of associtaion ya kampuni, kujaza documents nyingine za usajili (Form 14b na Ethics and Intergrity form) pamoja na kufanya usajili wenyewe kwa njia ya mtandao wa ORS (Online Registration System)
 
VRN Ina umuhimu gani?

VRN (Vat Registration Number) ni namba ya usajili anayopewa mfanyabiashara au kampuni ambayo imetimiza vigezo vya kupata VRN.

Kigezo kikuu cha kupata VRN ni turnover yako ifike milioni 100 kwa mwaka au milioni 50 kwa miezi 6, lakini pia kuna biashara ambazo zipo makundi maalum ya kupata VRN pasipo kuangalia turnover yake (mfano ujenzi, consultation n.k)

Umuhimu wa VRN kwanza kabisa ni rahisi kufanya kazi na kampuni kubwa, mara nyingi (sio mara zote) kampuni kubwa hupenda kufanya biashara na watu waliosajiliwa na VAT.. sababu wao huwa wamesajiliwa na Vat so na wao wanatafuta wenzao waliosajiliwa ili wafanye biashara, na hii huwa inawasaidia wao kupunguza kodi za VAT pale wanaponunua kwa mtu ambae amesajiwa kama wao

Lakini pia asilimia 90% kama sio 95% ili upate Tender ya serikali ni lazima uwe na VRN. So kwa namna moja au nyengine VRN ina umuhimu pale tu unapojua nini unatakiwa kufanyia au kama biashara yako imeshazidi turnover ya Milion 100 kwa mwaka.. Otherwise hutohitaji kuwa na VRN
 
Kusajili kampuni kea ORS Kuna vikwazo gani, kampuni yangu tangu 2016 nahangaikia ORS sipati usajili japo ilikuwa na usajili was awali kabla ya ORS shida Nini,nifanyeje? Maana Kama Ni gharama nimetuma za kutosha Niko hoi
 
Nawezaje kuendesha kampuni bila kulipa kodi.

Utaratibu wa kupeleka hesabu ya mapato kila mwaka inafanyika(mpangilio).

Unaweza kuwakata wafanyakazi kodi ya serekali kwenye mishahara, na Ninapoajiri natoa ripoti wapi?
 
Kusajili kampuni kea ORS Kuna vikwazo gani, kampuni yangu tangu 2016 nahangaikia ORS sipati usajili japo ilikuwa na usajili was awali kabla ya ORS shida Nini,nifanyeje? Maana Kama Ni gharama nimetuma za kutosha Niko hoi

Aiseee ORS yenyewe imeanzishwa february 2018, ila kama unakwama kwa kipindi chote hiko basi unahiraji msaada wa kufanikisha hilo jambo.. Maana miaka yote hiyo kuhangaikia jambo la usajili inashangaza kwa kweli… NiPM au nitafute whatsapp no 0714499248 kwa msaada zaidi
 
Back
Top Bottom