SectionTwenty
JF-Expert Member
- Aug 3, 2013
- 675
- 611
- Thread starter
- #261
Naomba hints nataka kuanzisha kampuni inayofanya kazi kama mtandao wa kupatana.com
Utaratibu wa kusajili kampuni ya aina yoyote ile huwa unafanana, ila utofauti huwa unakuja kwenye upatikanaji wa leseni na vibali vya biashara
Ili kusajili kampuni mpya kwanza kabisa inabidi waanzilishi wa kampuni muwe wawili na kuendelea, na pia kama wote ni watanzania ni lazima muwe na namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na namba za TIN zenu binafsi, ila kama kuna raia wa kigeni inabidi awe na passport ya kusafiria.