Mtaji wa kakampuni kadogo kadogoka kukopesha "micro credit" regulations zake
Acha nijibu kwa faida ya wengine pia ambao wanataka kujihusisha na biashara za kukopesa, nini na nini wafanye ili kupata kibali cha BOT ambao ndio wasimamizi wakuu wa biashara hii
MAELEZO YA JUMLA
1. Mwombaji anatakiwa awe amesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya makampuni
2. Jina la kibiashara la mwombaji linatakiwa liwe na maneno yafuatayo “Microfinance”, “Finance” “Financial Services” “Credit” au “Microcredit”
3. Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya maombi ya leseni ya shilingi 500,000 ambayo haitarudishwa
4. Mwombaji anatakiwa kulipa ada ya maombi isiyorudishwa kwa njia ya
uhamisho wa moja kwa moja wa TISS kutoka Benki zao kwenda Benki Kuu ya Tanzania
5. Mwombaji atahakikisha ana mtaji usiopungua shilingi milioni ishirini pale anapoanza biashara na wakati wote.
6. Sera ya Mikopo
Taarifa/Nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya Maombi ya Leseni
1 Barua ya maombi
2. Slip ya Bank inayothibitisha malipo ya ada.
3. Uthibitisho wa chanzo na upatikanaji wa mtaji unaopendekezwa na mtoa huduma ndogo za fedha.
4. Nakala zilizothibitishwa za vyeti vya taaluma na utaalam vya wajumbe waBodi na Mtendaji Mkuu.
5. Audited Financial Statement (kama ipo).
6.TIN ya kampuni
7. Sera ya Mikopo.
8. Tamko kwamba fedha itakayotumika kuwekeza haikupatikana kwa njia ya
jinai au haihusiki na shughuli yoyote ya kijinai.
10.Copy za vitambulisho vya Directors na shareholders
11.Dodoso lililojazwa kikamilifu Kwa ajili ya Wakurugenzi, Mmiliki au Mtendaji Mkuu
12.Certificate of Incorporation
13. Memorandum
14.Board Resolution.