Mimi naomba kuuliza kidogo ,
1).Je kama kampuni mulianzisha watu wawili yaani 50% kila mmoja ,lakini mukaona ili tuendelee vizuri tunahitaji kuuza hisa kwa investors ili wafeed hii , so, mgawanyo wa Hisa unakuwaje ? yaani nani anatoa thamani ya hisa munazotaka kumpa investor ? if shareholders mumekubaliana kutoa 5% kila mmoja =10%
2).Sheria ya brela inatutaka waanzilishi wa kampuni wawe 2 , but Mimi katika kuanzisha nikamtafuta just friend mfano nikampa 30% but wakati kampuni inaendelea tu vizuri yeye akasema anataka kuondoka na apewe haki yake , so, vipi hii inakaaje , yaani hakuna sheria naweza weka kwa mtu yoyoye ambae nitampa share ??/( note : Mimi ndie nimetoa mtaji , yeye nimempa just tutimize takwa la kuwa wawili waanzilishi ??)
3).Je CEO anaweza akawa fire out licha ya kuwa yeye ndie mmiliki mkubwa wa hisa/,miongoni mwa wamiliki wa hisa ??
1. Hayo ni makubaliano ya kampuni na huyo Investor, kwasaabu kwenye Private Company sheria inaruhusu mauziano ya shares baina ya mtu mmoja na mtu mwengine.. kama Investor atataka kuja kununua shares ambazo ziko issued kwenu basi nyie wenyewe ndio mtaangalia mnaweza kumuuzia asilimia ngapi ambayo ina thamani ya kiasi gani.
Ndio maana kwenye mauziano ya share inaandaliwa kwanza Board Resolution, kuonyesha kuwa kampuni au shareholder wa kampuni ameamua kuuza asilimia kadhaa ya shares zake kwenda kwa mtu flani na huyo mtu atalipa kiasi fulani.
Baada ya hayo maamuzi kupitishwa na Bodi ya wakurugenzi then itaandaliwa na mikataba ya mauziano ya shares.
Kufupisha habari naweza kusema hili jambo ni makubaliano binafsi kati ya Investor na kampuni, hata mkitaka kumuuzia shares zote ni sawa tu. Sheria inakuongoza kufuata tu legal process ili zoezi lifanyike kihalali na serikali ipate kodi yake, ila haikuambii utoe asilimia ngapi au nani auze shares na nani asiuze, hayo ni maamuzi yenu
2. Unapotaka kuweka mtu ili kutimiziwa matakwa ya kisheria, huwa tunashauri kwanza kabisa umpe aailimia chache, maana kisheria unaweza kumpa mtu share hata 1% tu, hizo 30 ulizotoa wewe ni nyingi sana
Tukija upande mwengine, huyu mtu ana haki ya kudai haki zake maana kisheria yeye ana umiliki wa 30% za kampuni, hakuna sehemu kimamlaka utasema nilimuweka tu ili kutimiza masharti. unapomueka mtu kwenye kampuni basi anahesabika kama mkurugenzi/mmiliki na anakua katika part ya umiliki, operations, faida na kila kitu kinachohusu kampuni.
Ndio maana wanasema kama hauko tayari kufanya kazi na mtu yoyote basi jisajili tu as Sole Proprietorship, maana kwenye kampuni lazima mkae chini walau watu wawili na mkubaliane, kama mtakua na makubaliano mengine binafsi hiyo sasa ni nyinyi ila Brela na TRA wao watatambua kuwa huyo ni mmoja wa wahusika katika kampuni.
Ikitokea situation kama hiyo sasa muhimu busara tu zitumike kutatua jambo.
3. Mabadiliko yoyote katika kampuni huwa yanaamuliwa na Bodi, na katika Bodi kuna mwenyekiti ambae ndio huyo CEO.
Ili mabadiliko yoyote yafanyike na kupitishwa katika kampuni inabidi maamuzi yake yasainiwe na Chairman na Company Secretay.
So kwa hizi kampuni zetu za watu wawili watatu CEO kutoka ni mpaka aidhinishe kujitoa mwenyewe,
NB: Upo pia utaratibu wa Chairman kutolewa na kampuni endapo kutakua na sababu ya kufanya hivyo kama vile ugonjwa mkubwa wa kumfanya ashindwe kufanya majukumu yake, kifo, kurukwa na akili, kutokua na uwezo wa kuongoza n.k hii inqtegemea tu na katiba ya kampuni inasemaje kwenye situation kama hizo