Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Yeah ni muhimu ufanye hivyo, na endapo ulishafanya makadirio ya kodi kwa mwaka huu basi andika barua ya kufunga biashara then chukua na barua ya serikali ya mtaa ya uthibitisho kwamba biashara imefungwa na kodi zilizobakia (za mwaka huu) hautozilipa.. na kama una leseni ya biashara pia andika barua ya kufunga leseni yako
Najifunza mengi sana unatoa free information kwa moyo wako wote God bless you man
 
Naomba kuongeza kuuliza kwamaba, kampuni inaweza kufanyabshughuli ambayi hakuandikwa kwenye memoradum. na kuna kosa gani kisheria kufanya hvyo.

yaani najiongezea huduma bila kuweka kwenye sheria ya kampuni
 
Gharama ya kusajili limited company huwa inategemea na share capital yake, nakuainishia kila kundi la share capital na gharama yake hapa chini

Mtaji Gharama za usajili
1. 20k-1M - 167,200
2. 1M-5M- 247,200
3. 5M-20M- 332,200
4. 20M-50M- 362,200
5. 50M mpaka mwisho 512,200
Hizi bei zako zinatia mashtaka au umeweka markup yako hapo?
 
Niko ughaibuni nimemtumia ndugu yangu kusajili kampuni ya ujenzi.
Naye ni director . Kampuni ina wakurugenzi 3
Ila gharama alinambia ni 1,988,500.

Kwa gharama hizo ulizo ainisha maana yake amenipiga na kitu kizito?
Tena sana maana huyu naye kaongeza.
Kwa kampuni yenye mtaji zaidi ya 50m gharama zake ni 440,000
 
Unaandika barua kwenda TRA kuwajulisha kuwa umefunga biashara, na utaandika barua kwenda halmashauri uliyochukua leseni ya biashara ili kuwajulisha waifunge leseni yako
Unapotaka kufungua biashara, wapi napaswa kuanza kwenda.
Je, Halmashauri au TRA?
 
Hizi bei zako zinatia mashtaka au umeweka markup yako hapo?

Ni vizuri kitu kama hukielew usitie neno, inasaidia sana kuficha uwezo wako wa kutafsiri mambo..

Hizo bei ni za Brela, sijaweka hata facilitation/consultation fee.. Hizo fee hapo zinajumuisha Registration Fee, Filling Fee na stampduty na zinalipwa kwa control no (Brela)

Kwa lugha rahisi tunasema kama mtu atakomaa mwenyewe kusajili kampuni bila kumtumia mtunmwengine basi kulingana na mtaji wake ajiandae kulipia hizo gharama
 
Tena sana maana huyu naye kaongeza.
Kwa kampuni yenye mtaji zaidi ya 50m gharama zake ni 440,000

Kwa mtaji wa milion 50 unalipia Brela kama ifutavyo

Registration fee ni 440,000
Filling Fee ni 66,000
Stampduty ni 6200
Jumla ni 512,200

Hiyo 512,200 unailipa kwa pamoja kipindi unasajili, so hamna ambacho niliongeza hapo
 
Naomba kuongeza kuuliza kwamaba, kampuni inaweza kufanyabshughuli ambayi hakuandikwa kwenye memoradum. na kuna kosa gani kisheria kufanya hvyo.

yaani najiongezea huduma bila kuweka kwenye sheria ya kampuni

Kisheria haiko sawa, kampuni inapaswa kudanya shughuli tu ambazo zimeorodheshwa katika memorandum ya kampuni.

Kama shughuli unataka kuifanya na haikuwepo katika objectives za kwenye memorandum ya kampuni basi unapswa kufanya ammendment ya objectives, na utaandaa board resilution ya kuonyesha kwamba mmeamua kuongeza shughuli flani katika kampuni.

So kujiongezea pasipo kufuata utaratibu wa kisheria ni kosa.
 
Naomba kujuzwa kuhusu kampuni ya magari ya kukodisha

Utaratibu wa kusajili kampuni ya aina yoyote huwa ni mmoja, utafoatui unakuja kwenye upatikanaji wa vibali na leseni ya biashara.

Ukisoma vizuri nishaelezea utaratibu wa kusajili kampuni, ila tukija kwenye inshu yako ya magari ya kukodisha inapaswa ufuate utaratibu huu (kwa ufupi)

1. Usajili wa kampuni Brela
2. Usajili wa TIN ya kampuni TRA
3. Usajili wa LATRA
4. Leseni ya Biashara Brela
 
Tuna kikundi chetu cha watu wanne na mtaji wa milioni 6 tunafanya biashara ya kukopeshana kazini kwetu, tunataka kusajili microfinance, hatua zipi tunatakiwa kuzifuata ili isajiliwe na kulipa kodi ya Serikali?
SectionTwenty

Hatua za kufuata ni 4 mkuu

1. Usajili wa kampuni BRELA
2. Usajili wa TIN ya kampuni na upatikanaji wa Tax Clearance (TRA)
3. Kibali cha kufanya biashara ya Microcredit kutoka BOT
4. Leseni ya biashara (BRELA)

Ukitaka msaada zaidi na kama una maswali ya ziada whatsapp na kawaida namba 0714499248
 
Niko ughaibuni nimemtumia ndugu yangu kusajili kampuni ya ujenzi.
Naye ni director . Kampuni ina wakurugenzi 3
Ila gharama alinambia ni 1,988,500.

Kwa gharama hizo ulizo ainisha maana yake amenipiga na kitu kizito?

Kila consultatnt/lawyer au mtu yeyote anaehusika na usajili wa kampuni huwa ana gharama zake za kufacilitate ukiondoa zile gharama za Brela.

Ila huyo aliewapa hiyo gharama aisee gharama zake ni za juu sana, hata Section Twenty hatujafikia level hizo [emoji23][emoji23] sisi bei zetu ni zwa wananchi wa kawaida.

Next time mkuu ukiwa unamuagiza mtu afuatolie jambo akikuletea gharama/ bei ukiweza omba breakdown, akupe tu mchanganuo kwamba imekuaje kuaje hadi gharama imekuwa hivyo
 
Naomba nimsaidie maana naona kaleta mada chokozi lakini hana majibu, VRN navyofahamu mimi ni vat registration number kwa lugha mama ni namba ya usajili wa vat.Faida yake ni kama umesajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani yaani vat risiti zote za mauzo yako au manunuzi inatakiwa namba ya muuzaji na mnunuzi kama wote ni vat register ionekane kwenye risiti sababu ukiuza sana kuliko kununua unapeleka tra hiyo vat na kinyume chake ukinunua sana na ukawa haujauza sana basi ile tofauti ya manunuzi na uuzaji unarejeshewa na tra.Ili uweze rejeshewa risiti lazima iwe na hiyo vrn ya aliyekuuzia na ya kwako kwenye risiti ya manunuzi.
Na je kama mnunuzi wako ni kutoka nje ya nchi na alikulipa cash?
 
Hatua za kufuata ni 4 mkuu

1. Usajili wa kampuni BRELA
2. Usajili wa TIN ya kampuni na upatikanaji wa Tax Clearance (TRA)
3. Kibali cha kufanya biashara ya Microcredit kutoka BOT
4. Leseni ya biashara (BRELA)

Ukitaka msaada zaidi na kama una maswali ya ziada whatsapp na kawaida namba 0714499248
Mkuu Brela ni usajili na si watoaji wa leseni. Nadhani namba 1 ni sahihi ila namba 4 ni mamlaka inayohusika na hiyo biashara au halmashauri ya eneo alilopo
 
Mkuu Brela ni usajili na si watoaji wa leseni. Nadhani namba 1 ni sahihi ila namba 4 ni mamlaka inayohusika na hiyo biashara au halmashauri ya eneo alilopo
Pia brela wanatoa leseni za biashara mkuu.. ila inategemea na aina ya biashara sio biashara zote leseni zake zinapatikana manispaa.
 
Back
Top Bottom