Niko ughaibuni nimemtumia ndugu yangu kusajili kampuni ya ujenzi.
Naye ni director . Kampuni ina wakurugenzi 3
Ila gharama alinambia ni 1,988,500.
Kwa gharama hizo ulizo ainisha maana yake amenipiga na kitu kizito?
Mkuu labda jamaa yako akawa sahihi , chukua hii
mfano, umesema ni kampuni ya ujenzi
Tuassume hizi charges kasajili bila kutumia mtu; E.g
brela 512,000
Tra kupata Tin makadirio mpaka tax clearanc lets say kalipia 200,000
Then kupata leseni ya biashara amelipia ada 500,000
Then tunakuja kwenye bodi la wakandarasi kupata leseni yao CRB
Basically hio kampuni itakuwa ni civil and building kuna ile ada ya 80,000@ nimeisahau inaitwaje, yani hapo 160,000
Afu kuna ile ada yao ya daraja la kampuni mfano kasajili class six[emoji3]ambayo ni jumla 500,000 civil and building (kama ni daraja chini ya hili maanaake hio fee itaongezeka zaidi ya 800k)
Lakini kama kampuni ni ujenzi pekee haihusishi masuala ya civil basi ada zinaweza zipungue ama zisipungue kulingana na daraja ulilosajili , ninachokijua ni hakuna civil bila building
Bado hajaweka facilitation fees kwa wadau wote wanaohusika katika kufanikisha swala zima la mihuri na ukaguzi ili upate vyeti vyote husika kwa kampuni husika tufanye umetumia 200,000 mjini hapa
Hii draft inasoma 2.72mil
Nadhani hizo gharama alikuambia ni maeshakamilisha kila kitu tayari kwa kuanza kazi,,,
Nadhani pia huyo jamaa ako kuna pahala pia amejiongeza ili mambo yaende kama mnavopanga yaende cha muhimu endelea kuaminiana