Mr sule
JF-Expert Member
- Oct 14, 2021
- 606
- 1,110
Iko hivi,
Mwaka unapoanza unajikadiria kodi yako kutokana na faida unayotegemea kupata kwa mwaka huo (kama ulivyoambiwa)
Mfano saaa umekadiria mwaka huu utapata faida ya milion 10.. kodi yako 30% itakua ni sh milion 3.
Ikatokea mwaka umeisha (itabidi kwanza uandae mahesabu ya kampuni (Audited Financial statement) na hayo mahesabu yakonyesha mfano umepata faida ya milion 20.
Kwa hivyo Kodi yako ilipaswa kuwa milion 6, na wewe ulilipia Mil 3 mwanzoni basi utapaswa kuongezea milioni 3 nyengine ili hesabu ziende sawa.
Ila Ikitokea mwaka umeisha na mahesabu yako yakaonyesha kuwa umepata hasara, basi ile kodi uliyokadiria mwanzon ya milion 3 inakua kama credit utayokua unawadai tra na itakusaidia kupunguza kodi za mbeleni.
Nimeipata boss, shukrani sana