Ngoja nikujibu jibu la maelezo marefu kidogo kwa faida yako na wote kwa siku zijazo.
Mnapokadiriwa kodi na TRA labda mwanzoni mwa mwaka, na unaona miezi inaenda ile biashara imekua ndivyo sivyo au imekufa kabisa jitahidi kabla mwaka haujaisha katoe taarifa TRA ili wabadilishe makadirio yako ya kodi, utawaambia umeenda kufanya ammendment ya makadirio ya kodi (TRA hawapendi hiki kitu ila ni inawezekana)
Kama una ushahidi wa kusupport unayoyaongea inakua vizuri zaidi, kama kodi labda ilikua 250k unaweza ukajikuta umepunguziwa hadi 100k
Ukikaa ukisubiri mpaka mwaka uishe kabisa hiyo kodi ni lazima utailipa, hata utoe sababu gani
Kama wewe ni mfanyabiashara ambae hutunzi kumbukumbu za hesabu wala huandai mahesabu ya mwaka (Tax under Presumpitve) HAKUNA PENALTY.. ingekua ni mfanyabiashara ambae unatunza kumbukumbu na kupeleka hesabu penalty ni sh 75,000 kwa kila mwezi unaochelewa na kwa kampuni penalty ni sh 225,000 kwa mwezi
Kama biashara umefunga tangu kipindi hiko andika barua kabla ya mwezi March tarehe 31 mwaka huu, usisubiri mwisho wa mwaka