1. YES, Inakuwa Limited Company.. Nachomaanisha kiundani ni kwamba sheria za makampuni wameweka hisa za mtaji (share capital) ambayo hii ni kama thamani ya kampuni kwa lugha rahisi, Ianzie kati ya 20k-1M
Ukifungua kampuni ya share capital yoyote kati ya hiyo Brela watataka ulipie sh 167,200 tu kama Registration Fee yako.
Ingawa kadri utavyokua unapandisha mtaji wa kampuni basi na gharama za usajili nazo zitazidi kuongezeka.. mfano mtu mwenye kampuni kati ya milion 5-20 yeye Registration fee yake huwa ni 332,200
2. Kufungua kampuni ambayo utaonesha una mtaji mdogo changamoto kubwa inaeza kukupata kwenye uombaji wa tender, maana sehemu nyengine wanaweza wakaangalia thamani ya kampuni yako wakaona ni ndogo sana hivyo hutoweza kumudu tender yao kwa jinsi wanavyotaka.
Na vile vile kuna baadhi ya leseni za biashara kama ukiweka mtaji mdogo mamlaka haiwezi kukupa leseni (japo ni biashara chache maana nyingi unaweza kupewa leseni pasipo kuzingatia mtaji wako wa kampuni)