Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Uliza swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa kodi na usajili

Kuna jamaa yangu mwaka jana wakati anafanya return july 2021 aliomba aongezewe muda akaonhezewa 30dys.

Kabla ya 30dys kuisha kama siku 5 hivi mtandao wa tra ukaanza kusumbua kila ajiupload unagoma akatoa taarifa ofisi za tra mkoa husika kwa barua na viambatanisho vikapokelewa.

Baada ya 30.07.2021 mtandao ulikaa sawa na kila akienda kufuatilia majibu anaambiwa wametuma makao makuu hawahajibiwa wanasubiri majibu.

Alisubiri hakupewa majibu,cha kushangaza jana kaenda kufanya makadilio akaambiwa alipe adhabu ya kuchelewa kusubmit hiyo return 450,000 ndiyo mambo mengine ya endelee na afisa yuleyule aliyemhudumia mtandao ulipogoma .

Je hatua zipi afuate kupinga hiyo adhabu kwani hakuwahi kupewa notisi ya adhabu hiyo na pia makadirio yake yalikuwa zero na meaka huu ni zero tena kwani amesimamaisha shighuli zake kwa sasa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Kwa faida yako na wengine kwa siku zijazo, ufanyapo au ufanyiwapo ritani yoyote ya kodi ya TRA basi HAKIKISHA UNAPATA ASSESMENT YAKO. Iwe ni return ya kufile online au umefanyiwa na Tax Officer make sure unaiangalia Assesment yako ili kujua kodi iliyotoka na kama kuna Penalty au Interest.

Endapo utabaini kuna kitu chochote kile hakipo sawa na maongezi ya kutumia busara za kibinadamu yameshindikana kukisahihisha basi unaruhusiwa kufile OBJECTION ya hiyo kodi kwenda TRA ili wapitie suala lako kihalali. Note kwamba Objection inaruhusiwa kufanyika ndani ya SIKU 30 tangu tarehe ya kutoka hiyo Assesment.

Ikipita muda huo ndugu yangu kwa kweli hata ukilalamika wakija kwenye base ya sheria ya kupinga kodi utapigwa KO mapema sana.

So hata sasa hivi ukiamua kupinga ni useless tu mkuu, hawatojisumbua maana uko nje ya muda wa kupinga kisheria. Pole!
 
Principle amount ikishaingia kwenye system na imeingizwa kihalali pasipo kutokea makosa yoyote basi hiyo inapaswa kulipwa.

Penalty na Interest unaweza kuomba msamaha Kwa Regional Manager kwa kujaza fomu ya APPLICATION FOR REMISSION OF INTEREST/PENALTY (lakini hii ni ngumu kidogo kukubaliwa though unaweza kujaribu)

Maana changamoto deni likishaingia kwenye system ndio lishaingia na njia rahisi ya kuliondoa ni kulipa.

Ukiona kama njia hiyo hapo juu imeshindikana basi kaa nao chini mkubaliane payment plan na uanze kulipia kidogo kidogo (hii unakubaliwa bila shida) huku mambo yako mengine kma vile kupewa Tax Clearance yakiendelea.
Asante kwa ushauri nitawafata na offer

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wa JPM tuliagizwa tupeleke tin namba zetu , nini madhumuni ya zoezi lile.
Lingesaidia vipi kudhibiti wafanyakazi hewa kwenye kampuni binafsi?
Kodi ya paye ambayo inalalamikiiwa na waajiri kuwa wanalipa kodi wakati mwajiri ni wakala tu ingeisaidia vipi?
Kwa nini kusiwe na juhudi kubwa za kuhakikisha kila kampuni mhasibu wake anajua kodi kama hajui basi mtaalambwa kodi aajiriwe.?

Nitajibu kwa namba

1. Madhumuni ilikua ni kila mfanyakazi alipe kodi yeye mwenyewe kupitia TIN yake, walitaka kila muajiriwa wa nchi hii awe anahusika direct na ulipaji wa kodi yake ya PAYE

2. Hii wanajua serikali wenyewe na plan waliyojiwekea kuhusu kudhibiti wafanyakazi hewa

3. Kodi ya PAYE inakatwa kwenye mshahara wa mfanyakazi, mwajiri ni wakala kama ulivyosema, sioni sababu kubwa ya yeye kulalamika wakati anakata kwenye mishahara ya wafanyakazi, wanaopaswa kulalamika ni waajiriwa..

4. Hili sasa ni jukumu la TRA na serikali kwa ujumla, sie wengine ni washauri tu ila maamuzi kama hayo yanafanywa na wao
 
Alipata assessment yake yenye NIL akafanya OBJECTION ndani ya muda ndiyo akaambiwa asubiri majibu wametuma makao makuu alifuatilia bila mafanikio hadi juzi alipofanya assessment ndipo anaambiwa majibu hayajarudi kutoka makao makuu hivyo alipe 450,000 ya kichelewa kufile return ya mwaka jana,hapo ndiyo mgogoro ulipo!!

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Aaaah hapo akomae tu kwa kweli.. japo ni kweli Objection zinachukua hata miezi 6 na hata zaidi, ila kesi ikawa haijatolewa maamuzi hiyo kodi huwa inawekwa pending then mambo mengine yanaendelea kama kawaida..

inawezekana anaongea na mtu ambae hayupo kitengo cha Objection ndio maana inakua ngumu, aende akaongee na Head of Techinical Unit Department ajue muafaka wa suala lake
 
Aaaah hapo akomae tu kwa kweli.. japo ni kweli Objection zinachukua hata miezi 6 na hata zaidi, ila kesi ikawa haijatolewa maamuzi hiyo kodi huwa inawekwa pending then mambo mengine yanaendelea kama kawaida..

inawezekana anaongea na mtu ambae hayupo kitengo cha Objection ndio maana inakua ngumu, aende akaongee na Head of Techinical Unit Department ajue muafaka wa suala lake
Mkuu unaweza kunisaidia namna ya kuangalia jina la kampuni ninalotaka kulisajiri kuwa kampuni kama limesajiliwa tayari na Brela....???
 
Mkuu unaweza kunisaidia namna ya kuangalia jina la kampuni ninalotaka kulisajiri kuwa kampuni kama limesajiliwa tayari na Brela....???

Ingia kwenye ORS then nenda kwenye sehemu ya Name Clearance halafu search jina unalotaka, majibu yatakuja hapo
 
Kuna Annual return unatakiwa kuwasilisha kila mwaka Brela. Huwa inagharimu 22,000 tu kwa mwaka.
Nadhani hata kama hufanyi biashara hiki kiwango kwa mwaka huwezi kushindwa kulipia
Ikiwa hujalipa hiyo annual return kwa zaidi ya miaka 9, utaratibu ukoje wa kwepa penati?
 
Naomba unielekeze jinsi ya kujaza makadirio ya kodi online maana nimeingia tovuti ya TRA sioni mahala naweza kujaza hiyo form.please assist
Hayo mambo sio ya kuelekezwa ukiwa mbali, ukilikoroga utalazimika to revise makadirio tena na tena
 
Duuhh..!!Naona inaniomba username na password[emoji15]

Yeah inabidi ucreate kwanza account mkuu ndio uingie, ingia www.brela.go.tz then nenda sehemu ya Online Company Registration halafu chagua sehemu ya create new ORS account, ukimaliza utalog in kwa username utayotumiwa kwenye email yako
 
Malipo ya withholding tax huwa yanaingia kama Credit ambayo inaenda kupunguza Corporate tax yako..

Mfano labda baada ya kuandaa hesabu zako ikaonekana kwamba Corporate Tax yako inapaswa kuwa Milion 1 lakini ukakumbuka kuwa kwa mwaka mzima ulilipia Withholding tax ya 800k.. basi hapa Corporate tax yako itapungua kutoka 1Milioni mpaka 200k..

Na hata kama ukiwa unadaiwa Corporate Tax lakini ukawa mlipaji mzuri wa Withholding Tax basi hiyo pia itakusaidia kupunguza deni lako la Corporate Tax
Hii withholding tax,mpaka uwaambie waiingize kwenye corporate tax??au waobwenyewe wanaweza fanya hivyo??
 
Penalty ya Annual return ya mwaka mmoja ni sh 2500 kwa mwezi zidisha mara idadi ya miezi uliochelewa kufile mpaka sasa
2,500 tu? Kumbe inalipika kabisa. Sasa ni kwanini TRA wao wanafanya Tsh 225,000 kwa mwezi?
 
2,500 tu? Kumbe inalipika kabisa. Sasa ni kwanini TRA wao wanafanya Tsh 225,000 kwa mwezi?

Ndio sheria zilivyowekwa mkuu na watunga sheria wetu.. Brela wana penalty ndogo saaaaaaana compared na TRA
 
Hii withholding tax,mpaka uwaambie waiingize kwenye corporate tax??au waobwenyewe wanaweza fanya hivyo??

Bila kuwa na uelewa unaweza ukashangaa hata wao wanakaa kimya tu, Ndio maana inashauriwa kampuni iwe na Auditor au Consultant ili ikitokea TRA hawajakuambia vitu kama hivyo basi mtu wako akusaidie kupunguza mzigo wa kodi.
 
Ninarun business name, nataka ibadili iwe kampuni kamili sasa. Utaratibu ukoje hapa??
Namaliza ORS online tu au lazima kwenda brela?
 
Mkuu mkali wao hongera Sana KWA kuamua kutega muda wako kutuelimisha.

Ni zipi faida za kuwa na kampuni kwenye maswala ya ulipaji kodi?

Japo kampuni ina compliance nyingi ila Faida zipo upnde wa kodi

1. Kampuni inajikadiria kodi yenyewe, hii inakupa nafasi ya kuamua kodi (corporate tax) kiasi gani ulipe pale mwaka unapoanza

2. Kodi ya kampuni inakadiriwa kulingana na faida utayopata, so unaweza ukawa umeingiza hela nyingi lakini faida ikawa kidogo basi inakupa ahueni ya ulipaji kodi tofauti na wangekua wanachukua kodi kwenye ulichoingiza bila kujali kama ni faida au la

3. Kodi inalipwa na kampuni na sio mtu binafsi (Director au shareholder) means kama wewe ni Director wa kampuni unaweza kuendelea na biashara zako binafsi pembeni pasipo madeni ya kodi ya kampuni yako kukuingilia moja kwa moja

4. Utunzaji wa kumbukumbu sahihi nao ni faida linapokuja suala la kodi za kampuni, kikubwa tu uwe vizuri kutunza nyarak na kumbukumbu za taarifa zako kibiashara
 
Back
Top Bottom