SectionTwenty
JF-Expert Member
- Aug 3, 2013
- 675
- 611
- Thread starter
- #121
Kuna jamaa yangu mwaka jana wakati anafanya return july 2021 aliomba aongezewe muda akaonhezewa 30dys.
Kabla ya 30dys kuisha kama siku 5 hivi mtandao wa tra ukaanza kusumbua kila ajiupload unagoma akatoa taarifa ofisi za tra mkoa husika kwa barua na viambatanisho vikapokelewa.
Baada ya 30.07.2021 mtandao ulikaa sawa na kila akienda kufuatilia majibu anaambiwa wametuma makao makuu hawahajibiwa wanasubiri majibu.
Alisubiri hakupewa majibu,cha kushangaza jana kaenda kufanya makadilio akaambiwa alipe adhabu ya kuchelewa kusubmit hiyo return 450,000 ndiyo mambo mengine ya endelee na afisa yuleyule aliyemhudumia mtandao ulipogoma .
Je hatua zipi afuate kupinga hiyo adhabu kwani hakuwahi kupewa notisi ya adhabu hiyo na pia makadirio yake yalikuwa zero na meaka huu ni zero tena kwani amesimamaisha shighuli zake kwa sasa.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kwa faida yako na wengine kwa siku zijazo, ufanyapo au ufanyiwapo ritani yoyote ya kodi ya TRA basi HAKIKISHA UNAPATA ASSESMENT YAKO. Iwe ni return ya kufile online au umefanyiwa na Tax Officer make sure unaiangalia Assesment yako ili kujua kodi iliyotoka na kama kuna Penalty au Interest.
Endapo utabaini kuna kitu chochote kile hakipo sawa na maongezi ya kutumia busara za kibinadamu yameshindikana kukisahihisha basi unaruhusiwa kufile OBJECTION ya hiyo kodi kwenda TRA ili wapitie suala lako kihalali. Note kwamba Objection inaruhusiwa kufanyika ndani ya SIKU 30 tangu tarehe ya kutoka hiyo Assesment.
Ikipita muda huo ndugu yangu kwa kweli hata ukilalamika wakija kwenye base ya sheria ya kupinga kodi utapigwa KO mapema sana.
So hata sasa hivi ukiamua kupinga ni useless tu mkuu, hawatojisumbua maana uko nje ya muda wa kupinga kisheria. Pole!