Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kwa mujibu wa familia, Ulomi aliondoka nyumbani tar.11 December 2024 akidai kupigiwa simu na watu wa TRA kwenda kufuatilia kontena lake bandarini.
Kwa mujibu wa Muliro siku hiyohiyo tar.11 Ulomi alipata ajali ya pilipiki na kukimbizwa kituo cha afya Makuburi (Ubungo External) kisha hospitali ya Mwananyamala.
Kwa mujibu wa Katibu wa Hospitali ya Mwananyamala, walipokea mwili wa Ulomi tar.11 kutoka kituo cha afya Makuburi. Maana yake confirmation of death ilifanyika kituo cha afya Makuburi.
#MaswaliMuhimu:
Nadhani maswali ni mengi kuliko majibu. Kwaheri Ulomi, kama kuna mtu amehusika na kifo chako, Mungu atakulipia. Damu yako haitaenda bure 😭😭
Imeandaliwa Malisa GJ na kuhaririwa na Msanii wa JF
PIA SOMA
- TANZIA - Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala
- Kituo cha Afya Makuburi: Ulomi aliletwa hospitali na Askari
- Kamanda Muliro asisitiza Ulomi amekufa kwa ajali, asema ndugu sio TCRA

- Hao wanaoitwa "Wasamaria wema" waliomuokota Ulomi kwenye ajali na kumkimbiza kituo cha afya Makuburi ni akina nani? Na kwanini wakae kimya? Ina maana hawakuona mitandaoni ndugu wa Ulomi wakihangaika? Kwanini hawakujitokeza waseme "tulimuokota huyu mtu kwenye ajali tukampeleka Mwananyamala?" Au kati yao hakuna mwenye smartphone?
- Kama kweli Ulomi alipata ajali maeneo ya Ubungo External ilikuaje ndugu wakadai simu yake mara ya mwisho imesoma Chang'ombe (Temeke)? Au yeye alipata ajali lakini simu ikaendelea na safari?
- Katibu wa Hospitali ya Mwananyamala anasema mwili wa Ulomi ulipokelewa ukiwa hauna utambulisho wowote, kwahiyo waliuhifadhi kama "unknown case". Lakini familia ya Ulomi imemtafuta ndugu yao kwa siku 5 bila mafanikio. Na hapo Mwananyamala walifika pia. Kwanini hawakuowaoneshwa miili ambayo haijatambulika ili waone kama ndugu yao atakuwemo?
- Je taarifa ya ajali haikutolewa Polisi? Kama ilitolewa, kwanini ndugu wa Ulomi walipoenda kufuatilia Polisi hawakuambiwa kuna ajali ya mtu asiyetambulika, mwili uko Mwananyamala nendeni mkaangalie?
- Polisi wanadai hawakuweza kumtambua kwa majina maana hakua na kitambulisho chochote. Lakini alikua na pikipiki yenye namba za usajili MC 415 DQC. Kwanini hawakuingiza hizo namba kwenye mfumo wa TIRA ili wapate jina la mmiliki wa pikipiki hiyo?
- Lori lililosababisha ajali yake halina dereva au usajili? Polisi wametoa maelezo kana kwamba hawajui wajibu wao muhimu Yani ajali ilihusisha pikipiki yake na Lori halafu hakunataarifa ya ziada whatsoever?