Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Huu ndio ukweli uliotamalaki nchini Tanzania na nje ya nchi na hasa Ulaya na Marekani , Hakika kila penye giza iko namna ya kupata mwanga .
Kwa wale tuliopita vijijini kuna wakati tunachelewa mahali fulani hadi usiku lakini tunalazimika kuendelea na safari kwenye usiku huo wa giza nene lililoambatana na mvua kubwa , kwa uwezo wa kawaida wa macho si rahisi kuona njia unayopita , bali kuna radi zinazopiga , pamoja na hatari ya radi hizo ( wakati mwingine husababisha mauaji ) lakini mwanga wake ndio hutuongoza kuona njia ya kupita
Hukumu hii iliyojaa makandokando kwa viongozi wa Chadema ni kama radi ya usiku katikati ya mvua nzito usiku wa manane .
Kiukweli kwa sasa Chadema inajadiliwa zaidi kote duniani kuliko kabla ya hukumu hii
Ama kwa hakika UTUKUFU WA MUNGU NI WA AJABU SANA !