Umafia katika Usajili: Simba SC yamsainisha Niyonzima kwa Mil.100 huku Yanga FC ikipigwa butwaa

Usajili wa Bongo kama wa kukomoana.
ni kukomoana tu hamna jingine
Ni kukomoana haswa maana fedha ya usajiri hai-reflect hali halisi ya mapato ya club...nadhani kuna haja ya kutunga sheria kwa hili suala la usajiri kama wenzetu yaani ela ya usajiri iambatane na source iwe ni mkopo ama mapato ya club lakini mwisho wa siku kwenye vitabu vya akaunti ionekane
 
Kweli kabisa umetoa wazo zuri sana naunga mkono!!!!!
 
Wameangaika na wangapi? Yanga miaka yote chuo chao cha soka ni Simba. Ila mwaka huu kwa vile ukata umepiga hodi
Shida ya Simba Koko ni mdomo wakati wa usajili, lakini tukifika uwanjani mnamshushia lawama Malinzi. Kwani Hamisi Kiiza si tuliwauzia sisi pia? Yuko wapi?

Sisi Tambwe wetu tunaye na anatupia mijibao na nyinyi ni mashahidi. Endeleeni kupiga mdomo, sisi tunaelekea ubingwa wa 28
 
I wonder, manake hata pale yanga ni mara chache alikuwa akipata full time,mara nyingi hucheza na kutolewa au huingia akitokea bench.
Kamusoko anaweza kucheza sita,Ajib akashuka nane,Ngoma kumi,tisa Chirwa au Tambwe.
Haswaaa
 
Hizo hela zinazoandikwa huwa sio kweli kuna udalali unafanyika mkubwa sana na mchezaji anaambulia hela ndogo tu. Na kwa taarifa TRA wapo tayari kukata kodi ya kutosha kwenye hizo hela mnazodai mchezaji kalipwa. Bora kuacha kutangaza mapato ya MTU hovyohovyo kwa kutafuta sifa za kijinga.
 
Million 100 kwa Niyonzima ni hadithi ya kusadikika. Kwa hiyo hela ya sportpesa itaisha kwenye usajili tu?

TRA kachukueni kodi yetu huko! millioni mia tutapata kodi sii haba. jifunzeni kwa Ronaldo na Messi.
 
Simba wamemsaini nani kutoka yanga!?huyo niyonzima Mwenyewe Ni tetesi tu,yanga ndo huwa mnatabia zakukomoana kwenye mpira,Leo simba wamewafanya mlichokuwa mkifanya mnabaki kulialia tu..!!ajib si mkichukua!?tulieni basi.
Waambie hao yeboyebo wakifanya wao wana ona sawa tumejibu mapigo wanalalamika
 
Umafia tu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya shilingi milioni 100.

Habari zilizopatikana jana jioni zinasema Niyonzima amekubali kujiunga na Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kumpa fedha hizo za usajili.

Kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara, Niyonzima ambaye amebakisha mwezi mmoja kwenye mkataba wake na Yanga, alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Simba SC.

Taarifa zinadai kuwa Simba waliongea na Niyonzima kabla hajaenda Rwanda kujiunga na timu yake ya Taifa, lakini akataka viongozi hao kuwasiliana na wakala wake ambapo Simba walifanya hivyo na kupewa dau walilokuwa wakilitaka.

Aidha, Yanga iliwasiliana na Niyonzima akiwa Rwanda baada ya kusikia Simba wamewasiliana naye na hivyo wakamuahidi ofa nono ili asisajiliwe na Simba.

Baada ya kusikia Yanga wamewasiliana na Niyonzima, Simba walimtuma mtu kwenda Rwanda kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini wakala wake aliwataka wamsubiri Niyonzima Dar es salaam kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Niyonzima alipowasili nchini juzi usiku alipokelewa na kigogo mmoja wa Simba huku Yanga wakiwa hawafahamu kama nyota huyo ametua nchini.

Imeelezwa Yanga walimuandalia nyota huyo dau la milioni 60 ili asaini mkataba wa miaka miwili, lakini tajiri mmoja wa Simba alimuhakikishia kumpa dau la shilingi milioni 100.

Kabla ya kupewa dau hilo, Yanga waliongezea dau lao na kufikia shilingi milioni 80 ambazo hata hivyo, hazikumshawishi Nahodha huyo wa Rwanda kusaini nao mkataba mpya.

Chanzo: Nipashe
Halafu usikute wamemsajili Haruna Lipumba nyie mnaita Haruna Niyonzima, manake hata Buswita tuliambiwa kamwaga wino msimbazi,ngoja tusubiri.
 
Waandishi wa bongo ni makanjanja mno

Umafia tu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya shilingi milioni 100.

Habari zilizopatikana jana jioni zinasema Niyonzima amekubali kujiunga na Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kumpa fedha hizo za usajili.

Kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara, Niyonzima ambaye amebakisha mwezi mmoja kwenye mkataba wake na Yanga, alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Simba SC.

Taarifa zinadai kuwa Simba waliongea na Niyonzima kabla hajaenda Rwanda kujiunga na timu yake ya Taifa, lakini akataka viongozi hao kuwasiliana na wakala wake ambapo Simba walifanya hivyo na kupewa dau walilokuwa wakilitaka.

Aidha, Yanga iliwasiliana na Niyonzima akiwa Rwanda baada ya kusikia Simba wamewasiliana naye na hivyo wakamuahidi ofa nono ili asisajiliwe na Simba.

Baada ya kusikia Yanga wamewasiliana na Niyonzima, Simba walimtuma mtu kwenda Rwanda kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini wakala wake aliwataka wamsubiri Niyonzima Dar es salaam kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Niyonzima alipowasili nchini juzi usiku alipokelewa na kigogo mmoja wa Simba huku Yanga wakiwa hawafahamu kama nyota huyo ametua nchini.

Imeelezwa Yanga walimuandalia nyota huyo dau la milioni 60 ili asaini mkataba wa miaka miwili, lakini tajiri mmoja wa Simba alimuhakikishia kumpa dau la shilingi milioni 100.

Kabla ya kupewa dau hilo, Yanga waliongezea dau lao na kufikia shilingi milioni 80 ambazo hata hivyo, hazikumshawishi Nahodha huyo wa Rwanda kusaini nao mkataba mpya.

Chanzo: Nipashe
 
Kwa habari za michezo hizo za nipashe nizilezile kama za kwenye magazeti ya shigongo Niyonzima kahsamalizana na Yanga kitambo toka jumatano
 
Ni kukomoana haswa maana fedha ya usajiri hai-reflect hali halisi ya mapato ya club...nadhani kuna haja ya kutunga sheria kwa hili suala la usajiri kama wenzetu yaani ela ya usajiri iambatane na source iwe ni mkopo ama mapato ya club lakini mwisho wa siku kwenye vitabu vya akaunti ionekane
Bonge la wazo na hili litafanya vilabu visijiendeshee kisasa zaid kwa kuuza jez na mambo mengine ikiwemo kutafuta wadhamin
 
Kwa habari za michezo hizo za nipashe nizilezile kama za kwenye magazeti ya shigongo Niyonzima kahsamalizana na Yanga kitambo toka jumatano
Endelea kujipa matumaini ila utafahamu hivi punde weka akiba ya maneno!
 
Back
Top Bottom