Umalaya ni mbaya sana! Ewe mwanaume mwenye familia, itunze

Umalaya ni mbaya sana! Ewe mwanaume mwenye familia, itunze

Muuza madafu wa Ikulu

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2024
Posts
1,277
Reaction score
2,888
Hiki kisa kimenisikitisha sana.

Kuna jamaa yangu na rafiki yangu kitambo toka 1980's kule Morogoro na tulianza biashara naye za kuuza/kuchukua Sigara kwenye treni kipindi hiko.

Mambo yakatunyookea tukaanza kufanya biashara za Mahindi kwenye mikoa ya Songea na Morogoro. Mwaka 1997 jamaa alioa nami niliona mwaka 1999 kwa kuwa tulikuwa na familia ikabidi kila mtu kuendelea na maisha yake japo mara nyingi huwa tunawasikliana na kushauriana mambo mbalimbali ya kimaisha.

Jamaa aliendelea kiuchumi na kufikia hatua ya kumiliki malori 10 yaliyokuwa yanabeba/safirisha mizigo toka Bandari ya Dar kwenda Zambia, Kongo na nchi nyingine za jirani. Baada ya kutajirika, akaanza tabia ya Umalaya.

Changamoto kubwa aliyokuwa nayo ni kutembea na wanawake wa kawaida yaani wasio wa hadhi yake. Ki kawaida, kwa mwanaume jama umeshindwa kutulia na mkeo. Basi tafuta mwanamke mwenye hadhi sio kuhangaika na wanawake wasio na kipato. Hii ilipelekea kuanguka kiuchumi kwani wanawake waliona ana mali so wakawa wanazaa naye. Sasa ana watoto 15 kwa wanawake 4 tofauti. Yule wa kwanza ana watoto naye wawili tu ila haonwengine ni wanawake wa Kiswahili wa pale Morogoro.

Hata kama dini yake inamruhusu, hakuna mwanamke anayekubali kuolewa mitara na hili alinishirikisha mwenyewe kuwa alishauriwa na shehe mmoja wa BAKWATA Morogoro kuwa anatakiwa amroge nankumshika akili mke yule wa mwanzo ili akubali aone mwanamke mwingine.

Ni kweli alifanikiwa kumshughulikia yule mama wa kichaga kwani amekuwa zumbukuku japo anasema yule mama hajakubali jamaa aone mwanamke mwingine ila yule mama hajitambui na anafanya vitu vya ajabu sana.

Sasa hivi, jamaa kafirisika na amekaa ndani analia tu. Wanawake wamemfirisi kwani alioa mwanamke mmoja polisi na mwingine mama wa nyumbani tu. Hao wote walitaka awajengee nyumba na jamaa aliniambia aliwanunulia kiwanja Morogoro Mjini na kuwajengea nyumba kwa gharama za milioni 60 kila mmoja. Kingine kilichomfanya aukwae umaskini ni gharama kubwa ya ada kwa watoto kwani analipa ada si chini ya milioni 30 kwa mwaka kwa shule asomeshazo watoto na kuna binti mwingine alizaa nje anamsomesha Law school.

Alinieleza hayo akaniomba ushauri na msaada ni kwa namna gani atalipa mkopo wa Tsh 150M toka CRDB ambao aliuchukua kama mkopo wa Kilimo na huko shambani kaambulia gunia 6000 tu za Mpunga ambazo nyingi ni madeni ya watu wengine waliomkopesha.

Enyi wanaume wenzangu, tulieni na wake zenu. Mnaharibu familia na ndoto za watoto wenu. Leo anampeleka mwanaye kweli awe Polisi? Inasikitisha sana.

Mi mwenyewe pamoja na kuuza kwangu madafu, siwezi na sitaruhusu mwanangu awe Polisi.

Dah Inasikitisha sana. Umalaya mbaya sana. Mungu atusaidie.
 

Attachments

  • 20241001_225410.jpg
    20241001_225410.jpg
    397 KB · Views: 4
Back
Top Bottom